Wednesday, December 31, 2014


Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Vinara wa msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Mtibwa Sugar FC wamewaahidi wapenzi wa soka visiwani Zanzibar kufurahia makali yao ya msimu huu watakaposhiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi mwakani.


Mtibwa Sugar FC, mabingwa wa Tanzania Bara 1999 na 2000, ni miongoni mwa timu nne za VPL zilizoalikwa na Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) kushiriki michuano hiyo itakayoanza Januari 1-13 mwakani.
Msemaji wa Mtibwa Sugar FC, Thobias Kifaru, amesema kikosi chao bado kiko Manungu, Turiani, km 100 kutoka mjini Morogoro na muda wowote leo Jumatano kitaanza safari kuelekea Zenj.

"Tumefanya vizuri katika Ligi Kuu ya Vodacom. Wazanzibar watarajie utamu kutoka kwetu. Tunahamishia makali yetu ya Bara huko Zanzibar," amesema Kifaru.
Mbali na timu nne zaa Tanzania Bara. Mtibwa, AzamFC, Yanga SC na Simba SC, timu nyingine nane zimealikwa kushiriki michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya tisa tangu ianzishwe kuenzi Mapinduzi Tukufu ya Zanzibar yaliyofanyika Januari 12, 1964.


Timu hizo ni pamoja na mabingwa watetezi KCC FC ya Uganda, mabingwa wa Zanzibar KMKM, Mafunzo FC, Shaba FC ya Pemba, Police Zanzibar, Mtende Rangers, JKU FC na Ulinzi FC ya Kenya huku mabingwa mara 19 wa Ligi Kuu ya Sudan, El Merrikh wakiomba pia kushiriki.

MOTO WA BURUDANI KUWAKA COCO BEACH MWAKA MPYA


Wapenzi wa burudani ya muziki wa kizazi kipya watapata burudani ya fungua mwaka kutoka kwa magwiji wa muziki wa kizazi kipya ambao wanatamba nchini katika tamasha la wazi la maisha murua na Vodacom katika ufukwe wa Coco beach jijini Dar es Salaam.Baadhi ya magwiji hao ni Profesa J,Temba,Chege,Roma Mkatoliki na wengineo wengi.
Tamasha hili litakalokutanisha magwiji wa bongo fleva ambalo limeanza kuwa gumzo la jiji kutokana na kuwa na burudani za aina mbalimbali kwa ajili ya kukonga nyoyo za wapenzi wa burudani limeandaliwa na Vodacom Tanzania.


MSIMAMO ULIVYO:
PosLogo &TeamPWDLGDPts
1ChelseaChelsea1914412746
2Manchester CityManchester City1913422443
3Manchester UnitedManchester United1910631436
4SouthamptonSouthampton1910361733
5ArsenalArsenal199641133
6West Ham UnitedWest Ham United19946731
7Tottenham HotspurTottenham Hotspur19946031
8LiverpoolLiverpool19847128
9Swansea CitySwansea City19847128
10Newcastle UnitedNewcastle United19757-626
11Stoke CityStoke City19748-225
12EvertonEverton19568-221
13Aston VillaAston Villa19568-1121
14SunderlandSunderland193115-1120
15Queens Park RangersQueens Park Rangers195311-1318
16West Bromwich AlbionWest Bromwich Albion194510-1017
17Hull CityHull City19379-816
18Crystal PalaceCrystal Palace19379-1016
19BurnleyBurnley19379-1516
20Leicester CityLeicester City193412-1413

waliotembelea blog