Uholanzi yaibana Brazil 3-0 na kutwaa nafasi ya tatu katika kombe la dunia.
Uholanzi ilimaliza katika nafasi
ya tatu katika kombe la dunia huko Brazil baada ya kuchomeka msumari wa
moto ndani ya kidonda cha wenyeji walipowalaza mabao 3-0 mjini Brasilia
siku ya jumamosi.
Mashabi wa Brazil waliwazomea wachezaji wao
akiwemo kocha Luiz felipe Scolari kwa utendakazi duni katika mechi hizi
mbili za mwisho Brazil ilipofungwa mabao 10 nayo ikifunga moja.
Brazil
ilifungua mechi hii kwa kasi lakini ikafungwa bao la kwanza kunako
dakika ya pili ya mechi hiyo kupitia kwa mkwaju wa penalti uliopigwa na
Robin va Persie.
Scolari atakuwa na wakati mgumu kuandikisha kandarasi mpya
Nahodha Thiago Silva alimtega Arjen Robben nje
ya eneo lakini refarii kutoka Algerian Djamel Haimoudi akaamua
kumwadhibu kwa kadi ya njano na penalti dakika mbili tu baada ya mechi
hiyo kuanza badala ya kumwonesha kadi nyekundu .
Mashambulizi ya Uholanzi yalizaa matunda kunako
dakika ya 15 ya mechi hiyo David Luiz alipookoa mkwaju uliokuwa unaelkea
wavuni kwa kichwa lakini ukamwangukia Daley Blind naye akaurejesha
humohumo .
Brazil imefungwa mabao 10 katika mechi mbili
Kila mtu uwanjani alifurahia Brazil walipofanya
mashambulizi kwenye lango la Uholanzi lakini kila mara walipofika katika
eneo walikosa makali na kushindwa kupenyeza safu ya ulinzi ya Uholanzi.
Uholanzi walisalia kulinda ngome yao na kila
walipopata fursa walitekeleza mashambulizi kwa lango la Selecao ambao
walionekana imara tofauti kabisa na timu iliyodenguliwa 7-1 na Ujerumani
juma lililopita huko Belo Horizonte.
Hata hivyo Georginio Wijnaldum aliifungia
Uholanzi bao la tatu kwa nunge na kumpa kocha Louis va Gaal kwaheri na
nishani ya shaba kutoka kwa fifa.
David Luiz alisababisha Brazil kufungwa tena
Kwa upande wake Scolari alisalia na maswali mengi bila majibu baada ya safu yake ya ulinzi kuvuja mabao 10 katika mechi mbili.
Bila shaka atakuwa na kibarua kigumu akijaribu
kuiokoa kibarua chake kisiote nyasi punde baada ya kipenga cha mwisho
cha kombe la dunia huko Maracana jumapili julai tarehe 13 .