Sunday, July 13, 2014


Uholanzi yaibana Brazil 3-0 na kutwaa nafasi ya tatu katika kombe la dunia.
Uholanzi ilimaliza katika nafasi ya tatu katika kombe la dunia huko Brazil baada ya kuchomeka msumari wa moto ndani ya kidonda cha wenyeji walipowalaza mabao 3-0 mjini Brasilia siku ya jumamosi.
Mashabi wa Brazil waliwazomea wachezaji wao akiwemo kocha Luiz felipe Scolari kwa utendakazi duni katika mechi hizi mbili za mwisho Brazil ilipofungwa mabao 10 nayo ikifunga moja.
Brazil ilifungua mechi hii kwa kasi lakini ikafungwa bao la kwanza kunako dakika ya pili ya mechi hiyo kupitia kwa mkwaju wa penalti uliopigwa na Robin va Persie.
Scolari atakuwa na wakati mgumu kuandikisha kandarasi mpya
Nahodha Thiago Silva alimtega Arjen Robben nje ya eneo lakini refarii kutoka Algerian Djamel Haimoudi akaamua kumwadhibu kwa kadi ya njano na penalti dakika mbili tu baada ya mechi hiyo kuanza badala ya kumwonesha kadi nyekundu .
Mashambulizi ya Uholanzi yalizaa matunda kunako dakika ya 15 ya mechi hiyo David Luiz alipookoa mkwaju uliokuwa unaelkea wavuni kwa kichwa lakini ukamwangukia Daley Blind naye akaurejesha humohumo .
Brazil imefungwa mabao 10 katika mechi mbili
Kila mtu uwanjani alifurahia Brazil walipofanya mashambulizi kwenye lango la Uholanzi lakini kila mara walipofika katika eneo walikosa makali na kushindwa kupenyeza safu ya ulinzi ya Uholanzi.
Uholanzi walisalia kulinda ngome yao na kila walipopata fursa walitekeleza mashambulizi kwa lango la Selecao ambao walionekana imara tofauti kabisa na timu iliyodenguliwa 7-1 na Ujerumani juma lililopita huko Belo Horizonte.
Hata hivyo Georginio Wijnaldum aliifungia Uholanzi bao la tatu kwa nunge na kumpa kocha Louis va Gaal kwaheri na nishani ya shaba kutoka kwa fifa.
David Luiz alisababisha Brazil kufungwa tena
Kwa upande wake Scolari alisalia na maswali mengi bila majibu baada ya safu yake ya ulinzi kuvuja mabao 10 katika mechi mbili.
Bila shaka atakuwa na kibarua kigumu akijaribu kuiokoa kibarua chake kisiote nyasi punde baada ya kipenga cha mwisho cha kombe la dunia huko Maracana jumapili julai tarehe 13 .

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog