Thursday, November 14, 2013

Kupitia kipindi chake cha ‘In My Shoes’ cha jana, Wema Sepetu alieleza jinsi alivyojisikia baada ya baadhi ya waigizaji wenzie wa Bongo Movie kugoma kuhudhuria msiba wa baba yake, Balozi Isaac Abraham Sepetu, mwishoni mwa mwezi uliopita kwa madai kuwa yeye hakuwa akifanya hivyo kwenye misiba mingine.


“Imeshatokea, wameacha kuja kwenye msiba, ni wao,” alisema Wema. Sio Bongo movie nzima, ni baadhi tu ya watu ambao wanauelewa na upeo mdogo ambao waliamua kutokuja. Lakini niliona Bongo movie wengi, walikuwepo marafiki zangu wengi, akina Batulli, akina Esha, Wolper alikuja, Lulu, JB alikuja, Jokate alikuja, Adam Kuambiana alikuja. Ambaye napenda nimpe my special thanks and appreciation, ambaye alijitolea from the beginning wa msiba mpaka to the end ni Dokta Cheni kwakweli. Dr Cheni, I thank na ntazidi kumshukuru,” alisema.

“Marafiki zangu kama akina Kajala, akina Zamaradi, wale sio marafiki, wale tayari ni ndugu, kwahiyo siwezi kuwaweka kwenye appreciation wala kwenye thanks.”

Katika kipindi hicho pia, Wema alisema yeye na ndugu zake walijua kuwa baba yako ni muumini wa dhehebu la Roman Catholic siku chache kabla ya kufariki dunia.

Balozi Issac Abraham Sepetu (71), alizikwa kikristo katika kijiji cha Mbuzini,mkoa wa Kusini Unguja October 30 ambapo mazishi yake yalihudhuriwa pia na Rais wa Zanzibar,Dk Ali Mohammed Shein pamoja na viongozi wengine.
WAKATI hatima ya kutiwa saini mkataba wa amani kati ya Serikali ya DRC na waasi waliosambaratishwa wa M23 ikiwa haijulikana, uhusiano wa maswahiba wawili wa eneo la Maziwa Makuu, Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Paul Kagame wa Rwanda umetikisika baada ya Museveni kumtaka mwenzake huyo azungumze na waasi.


Ni ushauri kama huo aliopewa Kagame Mei mwaka huu na Rais Jakaya Kikwete ukilenga kuleta na kuimarisha amani Mashariki mwa Congo ndio ulioyumbisha uhusiano kati ya Tanzania na Rwanda, kabla ya Kikwete kuifafanua na kisha kukutana na Kagame jijini Kampala, Uganda Agosti mwaka huu.

 


Kwa mujibu wa mtandao wa AfroAmerica Network, Museveni, baada ya kurejea kutoka kwenye mkutano wa wakuu wa nchi za SADC na zile za Maziwa Makuu (IGGLR) huko Pretoria, Afrika Kusini wiki iliyopita, alimpigia simu Kagame na kumwambia: “Huenda sasa ni wakati muafaka wa kuzungumza na wapinzani wako wenye silaha.”


Chanzo cha habari cha mtandao huo kimemnukuu mmoja kati ya viongozi wa juu wa Jeshi la Rwanda (RDF), akisema Museveni alimwomba Kagame kuzungumza na waasi hao haraka kabla muda haujapita mara tu Rais huyo wa Uganda aliporejea Kampala Alhamisi iliyopita.


Mkutano wa pamoja wa wakuu wa nchi za SADC na ICGLR uliofanyika kuanzia Jumatatu wiki iliyopita chini ya uenyekiti wa marais watatu, Joyce Banda (Malawi, SADC), Museveni (Uganda, ICGLR) na wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, ulitoa wito kwa M23 kuweka silaha chini. Siku mbili baadaye waasi hao wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda, walishindwa vita na kutangaza kuacha uasi.


Kagame hakuhudhuria mkutano huo, badala yake aliwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Louise Mushikiwabo.


“Ni ushauri tu. Nimerejea kutoka kwenye mkutano na SADC uliojadili amani eneo la Maziwa Makuu. Bahati mbaya inaonekana kwamba karibu viongozi wote wanaamini kikwazo kikubwa cha amani ni kuwapo kwa waasi wa Kinyarwanda mashariki mwa DRC.


“Hakika suala hili linapaswa kuzungumzwa kwa njia moja au nyingine. Na viongozi hao wanaamini kwamba hili halitatatuliwa bila serikali ya Rwanda kukaa kwenye meza ya usuluhishi na wapinzani wake wenye silaha. Hata mimi ninaamini hivyo, huenda wakati umefika kwako kuzungumza nao,” alinukuliwa Museveni akimwambia Kagame katika mazungumzo ya simu yaliyodumu kwa takriban dakika 15.


Kagame alijibu: “Sitozungumza na FDLR, washiriki wa mauaji ya kimbari. Never, … , ever. Sitozungumza kamwe na wahalifu.”


Hata hivyo, inadaiwa Museveni alimkumbusha Kagame kuwa si waasi wote wa Rwanda walioko DRC ni wanachama wa FDLR au wahalifu  na kwamba wapo anaoweza kuzungumza nao kwa kuanzia.


Baada ya mazungumzo hayo, Kagame aliitisha mkutano wa dharura na washauri wake wakuu na kuwaeleza walichozungumza na Museveni na kuongeza:


Nimekuwa nikiwaambia mara kwa mara kuwa tuko peke yetu. Hata Yoweri, tuliyemwamini kama rafiki yetu na mwenzetu anatugeuka! Leo anatuambia hiki, kesho anakwenda kukutana na viongozi wengine na kutubadilikia.


Baadaye akawataka washauri hao kuja na mpango mkakati wa nini cha kufanya wakati huu Rwanda ikizidi kutengwa na nchi za Afrika na hata za nje ya Afrika.


Mwanzoni mwa mwezi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry na mwenzake wa Uingereza walimwonya Kagame kuachana mara moja na ushiriki wake kwenye machafuko ya mashariki mwa DRC, ikiwa ni mara ya pili ndani ya mwaka mmoja kwa wakubwa hao kutoa onyo kama hilo.


Wakati hayo yakiendelea, zipo taarifa kwamba Rais Museveni amepanga kutuma ujumbe nchini kuja kuzungumzia mustakabali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwaambia Watanzania kwamba Tanzania haijakiuka chochote katika makubaliano ya msingi, ila wenzetu hao ndio huenda wana ajenda yao.


Kauli ya Kikwete ilihitimisha hali ya wasiwasi wa Tanzania kujitoa EAC na iwapo ujumbe wa Uganda utakuja, itakuwa ni mwendelezo wa kilichofanywa mwishoni mwa wiki na Kenya waliomtuma Waziri wa Mambo ya Nje kuja Dar es Salaam kuweka mambo sawa.


>>>Hali nchini Kenya


Mapema wiki hii, aliyekuwa Mwanasheria wa Serikali ya Kenya, Amos Wako ambaye pia ni Seneta wa Bisia alitoa wito kwa Rais Uhuru Kenyatta kuhakikisha kuwa EAC haisambaratiki, akidai kuwa watakaoumia zaidi ni Wakenya.


Wako aliyekuwa kwenye mkutano wa hadhara pamoja na Mbunge wa Budalangi, Ababu Namwumba, alisema wakati jumuiya ya awali ilipovunjika mwaka 1977, Wakenya wengi waliokuwa wakifanyakazi nje ya nchi ndio walioathirika zaidi.


“Wapo watu mashuhuri kama Raila Odinga na Kalonzo Musyoka wanaokubalika ndani na nje ya nchi ambao kama Uhuru anataka wanaweza kumsaidia kuzungumza na Rais Kikwete wa Tanzania. Hatutaki jumuiya hii ivunjike, si busara hata kidogo,” alisema Wako.
DSC07947 b6a20
Gari namba T606 BJB  lilolokuwa linaelekea Ifunda kutoka stand kuu ya Iringa limepata ajali ya kuligonga Lori namba T 234 CLU Mali ya T.H Clements & Son LTD eneo la Kitwiru, wakati Dereva wake alipojaribu kulipita Lori hilo bila mafanikio   watu watatu wamejeruhiwa.
Picha na Said Ng'amilo.(HD)
DSC07949 8c551
DSC07952 09012
DSC07959 01a00
Bob Junior Sharobaro
Mwanamuziki kwenye muziki wa kizazi kipya Bob Junior hivi karibuni amefunguka na kuweka wazi sababu zilizomfanya aamue kuachana na mke wake.

Katika mahojiano niliyofanya naye kwenye kipindi cha The Takeover, TBC fm, mnamo siku ya Jumanne, Bob Junior alifunguka na kueleza mambo mengi huku akikiri kwamba ni kweli kuwa amemuacha mke wake, "mwanamke anataka kuwa kama mume ndani ya nyumba, 

amefikia hadi hatua haongei na mama yangu mzazi" alisema Bob Junior.

Nilimuuliza pia juu ya idadi ya taraka alizompa, " mimi nimempa taraka tatu maana nimemaliza kabisa" alisema mkali huyo ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake mpya iitwayo Bashasha aliyomshirikisha Vanessa Mdee.

  


Jana tuliweka habari hapa  kuwa actress maarufu Bongo Movies Blandina Chagula(Johari) amekwenda Canada kumfuata mpenzi wake raia wa nchi hiyo na pia kutambulishwa ukweni.  
Habari mpya ni kuwa baada ya kutambulishwa mipango ya ndoa kati ya johari na mzungu huyo itafanyika ili wawili hao waishi kama mke na mume baada ya mzungu huyo kuwa hoi bin taabani kwa penzi la Johari aliyejaaliwa kipaji cha kuigiza.  
Habari za mipango hiyo ya ndoa zimetolewa na Irene Uwoya alipozungumza na paparazi wetu kwa kusema "akitambulishwa kitakachofuata ni ndoa, na kwa jinsi tulivyojadiliana watafanya ndoa mbili moja hapa(Tanzania) na nyingine Canada ili na sisi tulio Dar es salaam tusherehekee ndoa yake kwasababu kama unavyojua ndugu zake, marafiki na watanzania kwa ujumla wanahitaji kuhudhuria ndoa hiyo"  
Uwoya ambaye nae aliolewa na raia wa Rwanda Hamad Ndikumana kwa ndoa ya gharama na mwishowe ndoa hiyo kuwa chali aliendelea kwa kusema "Juzi niliandika kauli ya kumtaka atulie akiwa Canada, sio kwamba Johari hajatulia unajua Johari ni mtu wangu wa karibu kwa hiyo nilikuwa namwambia asipeleke uswahili Canada sio kwa nia mbaya"
Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
SIMBA SC inatafuta kipa mzuri wa kumsajili katika dirisha dogo, wakati huo huo inafikiria kuachana na kipa wake, Mganda, Abbel Dhaira ikibidi mapema iwezekanavyo au mwishoni mwa msimu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, kutokana na kanuni mpya ya usajili wa wachezaji wa kigeni msimu ujao ya wachezaji watatu kutoka watano, hawatahitaji kipa mgeni.
Tunatafuta kipa; Zacharia Hans Poppe amesema wanatafuta kipa wa kusajili dirisha dogo

Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), amesema kwamba kwa sababu hiyo lazima waachane na Dhaira mwishoni mwa msimu, au kama atapata timu hata sasa ambayo itakuwa tayari kuilipa Simba, watamuuza.
Poppe amesema kwa sasa Simba SC tayari inasaka kipa atakayekwenda kuwa pamoja na makipa wa wazawa, Abuu Hasimu na Andrew Ntalla.
“Niseme wazi, tunatafuta kipa. Huu ni mchakato makini sana na hatutaki kurudia kosa. Tunatafuta kipa mzawa, kwanza awe mwaminifu na mwenye uwezo mkubwa,”alisema.
Kuhusu habari kwamba, klabu hiyo inabadilisha benchi la Ufundi, Poppe amesema kwamba huo si ukweli kwa sababu hakuna kikao chochote kilichoketi kujadili suala hilo.
“Ripoti ya kocha (ya mzunko wa kwanza wa Ligi Kuu) ndiyo kwanza inafika leo, wala hakuna kikao kilichoketi kuijadili, sasa hizo taarifa zinatoka wapi?”alihoji Poppe na kuongeza; “Sisi tunajua kuna hizo presha za kufukuza makocha, lakini hatujui haswa zinatoka wapi, mimi ninaomba nyinyi Waandishi muache kuvuruga wakati huu,”alisema.
Wakatu huo huo: Viongozi wa matawi yote Dar es Salaam wanatarajiwa wanatarajiwa kukutana makao makuu ya klabu Ijumaa asubuhi, kujadili marekebisho ya Katiba, mchakato unaoendelea vizuri hivi sasa klabu hiyo.

 Mhandisi Silvan Mloka baba wa mtoto muda mchache akiwa nyumbani kwake kashenye kashai bukoba kabla ya kuelekea morogoro
                                                   mwili wa mtoto  ukitolewa hospital ya mkoa wa kagera
                                                                heshima za mwisho zilitolewa
                                                     jamaa waliokuja kuhaani
 mwili wa mtoto  Alban Silvan Mloka aliezaliwa  25-04-2012 na kufariki 13-11-2013 ghafla, mtoto alikuwa na umri wa mwaka mmoja na miezi saba
                                                                    heshima za mwisho
                                                                                   majonzi....
 mwili wa mtoto ukipakiwa kwenye gari tayari kwa safari ya kuelekea morogoro kwa mazishi
               mama wa mtoto mwenye kitambaa cheupe akisaidiwa kwenda kupanda gari
                              mama wa mtoto mrs mloka yeye ni mwalimu wa shule ya sekondari bilele
                                   wafanyakazi wa Tanroad kagera wakiwa msibani 
 wanafunzi wa shule ya sekondari bilele walifika kumpa pole mwalimu wao aliefiwa na mtoto
 bw mloka na mkewe,ndugu jamaa na marafiki wakiwa kwenye gari tayari kwa safari kuelekea morogoro
 Siku zote sitoacha kumshukuru Mungu kwa kila hatua
ninayopiga katika safari yangu ya Music,na sitokutendea 
haki nisiporudisha shukrani za dhati 

kwa wewe shabiki yangu wa kweli unae 
endele kunipa sapoti inayonifanya nizdi kukaza 
kukutengenezea mambo mazuri zaidi..hii ikiwa ni ziara
 yangu mhimu kabisa nchini Naija,kwa ajili ya kupika kile
 unachkisubilia kwa hamu,my number one remix na
 mwanangu Davido,hii ilikuwa ni jana usiku
 tukiwa studio,hii ni studio ya Davido iliyopo nyumbani
kwake na kkubwa tulichokuwa tunakifanya ni kumalizia kabisa 
audio kabla ya kuingia mzigoni kushoot kideo.......
Davido nyuma ya screen akifanya mambo yake kwa umakini kabisa.....!!!


 Team yote hii ni kuhakikisha kila kitu 
kinaenda sawa kabisa..Babu tale kwa mbali mwenyewe kamechishaa.....!!!

When Skelewu meet Ngololo..stay tuned..we coming baby..WCB for life huny

waliotembelea blog