Thursday, November 21, 2013

Muonekano mpya wa Staa wa Bongo Movies,Vincent Kigosi’Ray’ umezua utata baada ya

mashabiki wake kuponda tattoo zake alichora huku wengine wakimpongeza kuwa amependeza.
Umechukiza vibaya mno delphinamkamba Acha Uswahili piga Kazi Kaka!!! Mbona Marehem Kanumba Alisemwa SN??? AU Umesahau Superstar Jalala!???? Kanumba alisemwa sana Lkn Aliyaacha YA ulimwengu Akapiga Kazi Ndio maana mpaka Leo Katangulia Mbele YA Haki Lkn Kazi Zake Zinakubalika.Then kwa Ushaur Wangu Wenzio Wanapambana Na Kusaka Kitu Gani Wazidishe Waachengue Mashabiki wewe Uko Busy Na Mapenzi Hyo Sio kaka NI Ushaur Tuu Kaka Kwakua nA kukubali Unawafanya Watu Tuliokua Tunakuheshim Tukushushe Thaman Achana Na Hivyo Vitu kaka!!Au Chagua mmoja umtambulishe ili Heshima Iwepo Wasikushushe Thaman Bwana!

• kennedymathew Tatoo hazijakaa vizuri. 2d • shadyasuleiman You look like shoga meen 1d
sherrylishizers Hujapendezaaaaa mfashist Yani mwili kama daftari la stadi za kazi lol.....punguza hayo madude asee
bawilid Tatoo aikupendezi ata,,,,,remain the way u r
wengine walimpongeza • evanbluetooth Unastahili kuwa Best Actor Tanzania kuanzia xaxa mpaka mika 4 ijayo....u got something special work on that Broda.. 4d • shollah I like u bt the way u luk i dn 3d • storycreator11j Ni kazi tu na kutaka kuwa tofauti ndicho kilichokuweka hvyo sio mbaya!! Big up! 2d • violethduncun Fanya kitu roho inataka big up 2d

                        Bw. Barack Obama akiwa na jamaa zake.
Mwanamuziki Nguza Viking na mwanaye Johnson Nguza 'Papii Kocha'.
Ile hukumu ya rufaa ya mwanamuziki Nguza Viking na mwanaye Johnson Nguza 'Papii Kocha' imewarejesha jela maisha baada ya hoja za serikali za kukazia hukumu kuzidi zile za upande wa utetezi.Babu Seya na Papii Kocha walihukumiwa kifungo cha maisha jela mwaka 2004 baada ya kupatikana na hatia ya kuwanajisi watoto wa Shule ya Msingi, Mashujaa, Sinza jijini Dar ambapo wamekuwa wakikata rufaa mara kwa mara lakini wakagonga mwamba. Hukumu hii ya rufaa ndiyo ya mwisho kusikilizwa


WANARIADHA kutoka nchi 21 wanatarajiwa kushiriki mbio ndefu za Uhuru, Uhuru Marathon, zinazotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Desemba 8, mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo, Katibu wa Kamati ya Uhuru Marathon, Innocent Melleck alisema, kujitokeza kwa wanariadha kutoka mataifa mbalimbali kumeongeza hamasa kubwa ya mbio hizo.
Melleck alisema, wanariadha kutoka mataifa hayo ndio ambao wamejiandikisha mpaka sasa na wanaamini wengi wataendelea kujitokeza ili kufanikisha lengo lake.
Alitaja nchi wanazotoka wanariadha waliojiandikisha mpaka sasa ni Tanzania, Uganda, Kenya, Afrika Kusini, Ethiopia, Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Malawi na Marekani.
Wanariadha wengine wanatoka Ujerumani, Jamaica, Urusi, China, Japan, Venezuela, Comoro, Nigeria, Italia, Canada, Madagascar na Uturuki.

“Hii ni faraja kubwa kwetu, kwani inaonyesha kwa kiwango kikubwa lengo letu la kupigania amani, umoja na mshikamano miongoni mwetu linakubalika na watu wengi duniani,” alisema.
Aidha Melleck alise,a usajili bado unaendelea kwa wale wanaotaka kushiriki ambapo fomu zitakazotolewa kwa mshiriki wa kilomita 3 atalipa Sh 100,000 yule wa kilomita 5 Sh 2,000 na washiriki wa kilomita 21 na 42 watalipia Sh 6,000.
“Tunachukua nafasi hii pia kuziomba kampuni au taasisi mbalimbali zinazotaka kudhamini mbio hizo zijitokeze na kufanya hivyo, kwani nafasi bado ipo na tukumbuke bila amani hakuna chochote kinachoweza kufanyika,” alisema.

















Mwanamziki mashuhuri Tanzania, anayejulikana kama Afande Sele Amejiunga na M4C, kwa kuingia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo. Mji wa morogoro ulirindima vifijo wakati Afande akizunguka na Msafara wa Piki Piki kuwaaga rasmi wale wasio na misimamo thabiti Kisiasa, kama inavyoonekana katika picha. kwa upande mwingine wapenzi wa CCM walionekana kuwa nahofu na uchungu, na walihisi sasa mambo yanazidi kuwa magumu sana kwao.

Kata ya mafiga wa upande wake ilionekana kutekwa kabisa na CHADEMA, huku katika mkutano wa Ndani Afande Sele alichaguliwa kushika nafasi ya Uenyekiti wa kata hiyo, katika kipindi hiki cha kushusha chama kwa wananchi (Program ya Chadema ni msingi), ambayo imekuwa mwiba mkali kwa CCM.
Ay-na-Msanii-aliyemsani-kwenye-lebo-yake-ya-Unity-Entertainment-Fezza


AY amesema kampuni yake ya Unity Entertainment haimsimamii tena aliyekuwa mwakilishi wa Tanzania kwenye shindano la Big Brother Africa The Chase, Feza Kessy.
AY amekiambia kipindi cha Mambo Mseto cha Radio Citizen jana kuwa hajawahi kukutana na Feza tangu arejee kutoka kwenye shindano hilo.
“Tangu ameenda Big Brother na akarudi hatujawahi kukutana face to face,” alisema AY.
“Kulikuwa na vitu kidogo ambavyo viko nje ya kikawaida kama unafanya kazi na artist vinatakiwa vifanyike. Kwahiyo tukaona labda alikuwa anatafuta tu opportunity fulani ya kukamilisha mambo fulani. Katika policy zetu za kampuni ni kuwa hatufanyi kazi kwa njia hiyo, kwahiyo tuliamua kumweka pembeni.”
AY amesema tayari alishaongea na Feza na kumtakia kila lakheri kwenye kila jambo atakalolifanya.

“Hata yeye mwenyewe tu nilimwambia namtakia kila lakheri, cha msingi atumie hiyo opportunity aliyoipata sasa hivi ili kufanya mambo mengine kama washiriki wengine wanavyoenda katika Big Brother.”

waliotembelea blog