Monday, September 7, 2015



Safari ya kuelekea kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya mwaka 2016 nchini Ufaransa imeanza kuiva baada ya timu tatu kukata tiketi ya kufuzu kwenye michuano hiyo baada ya kupata matokeo mazuri katika michezo ya hatua ya makundi iliyopigwa mwishoni mwa wiki.
Moja ya timu ambazo zilijihakikishia tiketi ya kwenda Ufaransa mwakani ni Iceland ambao matokeo ya sare ya bila kufungana dhidi ya timu ya taifa ya Kazakhstan yaliwafanya wafuzu wakiwa wanaongoza kundi lao kwa tofauti ya pointi 7 huku zikiwa zimesalia raundi mbili za mechi hizo za kufuzu.
Katika Kundi hilo la A, Timu ya taifa ya Jamhuri ya Czech nayo ilijihakikishia kufuzu baada ya kushinda mchezo wao dhidi ya Latvia kwa matokeo ya 2-1.
Msimamo wa Kundi A ukionyesha hali halisi ya kundi hilo ambapo Iceland na Jamhuri ya Czech wamejihakikishia kufuzu .
Msimamo wa ‘Kundi A’ ukionesha hali halisi ya kundi hilo ambapo Iceland na Jamhuri ya Czech wamejihakikishia kufuzu.
Timu ya Taifa ya Uholanzi imejiweka katika mazingira magumu ya kufuzu baada ya kufungwa mechi mbili mfululizo na vigogo wa Iceland na Uturuki, matokeo ambayo yamewaacha Waholanzi hao wakiwa kwenye nafasi ya nne.
Timu nyingine ambayo ilitangaza kufuzu kwa michuano hiyo itakayofanyika mwakani ilikuwa England ambayo ushindi wake wa 6-0 dhidi ya San Marino ulitosha kuwafanya wafuzu kama washindi wa ‘Kundi E’ wakiwa wamewazidi wapinzani wao wa karibu Switzerland kwa pointi 6 huku wakiwa na uwiano mzuri wa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.
England nao wana uhakika wa kufuzu wakiwa wanaongoza kundi E.
England nao wana uhakika wa kufuzu ambapo wanaongoza Kundi E.
Nahodha wa England Wayne Rooney katika mchezo dhidi ya San Marino alifikia rekodi ya gwiji Bobby Charlton ya kuwa mfungaji bora wa miaka yote kwenye timu ya taifa akiwa amefunga mabao 49 kati ya Magoli yote 106.
rooney
Rooney anahitaji bao moja zaidi ili kuweka rekodi ya kuwa mfungaji anayeongoza kuifungia timu ya taifa katika miaka yote.

waliotembelea blog