Sunday, June 28, 2015


Morgan Schneiderlin atakuwa ni wa pili kusajiliwa na klabu ya Manchester United Msimu 2015/2016 na atajiunga na Mashetani wekundu wiki ijayo Jumatano Dirsha la Usajili litakapofunguliwa rasmi.  Manchester United wamekamilisha usajili huo kwa kutoa kitita cha £25million kwa Morgan Schneiderlin – na taarifa zaidi kutoka Klabuni humo zinadai kuwa usajili unaendelea na ambao wamewaweka kwenye anga zao ni Kipa Jasper Cillsessen pamoja mchezaji wa Bayern Munich Bastian Schweinsteiger.
Kipa Jasper Cillsessen


Mshambuliaji Samuel Eto’o amejiunga na klabu ndogo ya Antalyaspor iliyopanda kucheza Ligi Kuu ya Uturuki msimu huu.
Makao makuu ya klabu hiyo ni mji wa Antalya ambao Yanga iliwahi kuweka kambi miaka miwili iliyopita. Kabla ya kutua hapo, Eto’o amewahi kuichezea klabu ya FC Barcelona ya Hispania, kabla ya Inter Milan ya Italia, Chelsea ya England na Everton ya England.


Paraguay wameifunga Brazil usiku huu kwa Mikwaju ya Penati (3-4) kwenye Michezo ya Copa America na Sasa kukutana uso kwa Uso na Argentina Nusu Fainali.Robinho akishangilia bao lake la dakika ya 15 kipindi cha kwanza kwa kuipatia bao 1-0 dhidi ya Paraguay baada ya kupata pasi safi kama kona kutoka kwa Dani Alves. 
Mpaka mapumziko Brazil ilikuwa ikiongoza kwa bao 1-0 dhidi ya Paraguay. Derlis González dakika ya 72 kipindi cha pili aliisawazishia bao kwa mkwaju wa penati na mtanange kumalizika dakika 90 kwa 1-1 na Mikwaju kupigwa.Shabiki wa Brazil wakiwa tayari kuangalia kipute!Brazil v Paraguay


HUKU ikishuhudiwa na  wachezaji wake wa kigeni Donaldo Ngoma na Joseph Tetteh Zutah waliowasili Dar es Salaam leo, Yanga ilijukuta ikitoka sare ya bila kufungana na Sports Club Villa ya Uganda kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwenye mechi hiyo maalumu kwa ajili ya kupinga mauji ya albino na mgeni rasmi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Saidi Mecky Sadiki, Yanga ilipoteza nafasi nyingi za kufunga kwenye mchezo huo.
Washambuliaji wa Yanga wakiongozwa na Amisi Tambwe na Simon Msuva walishindwa kufurukuta mbele ya ukuta thabiti wa Sports Club Villa ambao ni mabingwa wa Uganda.
Yanga iliwachezesha wachezaji wake wapya iliowasajili msimu huu kama vile winga Deus Kaseke aliyetoka Mbeya City, Malimi Busungu aliyetoka Mgambo JKT na chipukizi Godfrey Mwashuiya aliyesajiliwa wakati wa dirisha dogo walishindwa kabisa kuipenya na kushuhudia wakipoteza nafasi kadhaa za kufunga hasa kipindi cha kwanza.
Malimi Busungu alikosa bao la wazi kwenye dakika ya 31 baada ya kupokea pasi nzuri ya winga Goefrey Mwashuiya, lakini mpira aliopiga ulitoka pembeni kidogo ya Yanga la Sports Club Villa na dakika ya 39 Amis Tambwe alikosa bao la wazi akiwa ambeki peke yake na kipa wa Villa Sebweto Nicholaus.



Kwenye mechi hiyo timu zote zilifanya mabadiliko kadhaa kwa Yanga kuwapumzisha Malimi Busungu na kumuingiza Kpah Sherman na Nadir Haroub’Cannavaro’ alitoka baada ya kuumia na kuingia Pato Ngonyani.
Huku Villa ikiwatoa Kasule Abdulkarim na kumuingiza Dua Abeid na kisha kumtoa Kazibente James na kumuingiza Kamazi Dennis.
Hata hivyo Yanga walipata penalti kwenye dakika ya 79 baada ya Deus Kaseke kuangushwa kwenye eneo la hatari lakini Simon Msuva alipaisha penalti hiyo na kuinyima Yanga ushindi kwenye mechi hiyo ya kujipima nguvu kujiandaa na mashindano ya kombe la Kagame.
Yanga mpaka sasa imecheza michezo miwili ya kujipima nguvu ambapo wiki hii iliifunga klabu ya daraja la kwanza ya Friends Rangers kwa mabao 3-2 kwenye mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.

waliotembelea blog