Tuesday, January 14, 2014


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeteua maofisa wanaoanza leo kukagua viwanja 19 vitakavyotumika kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
Ukaguzi huo pia unahusisha viwanja ambavyo Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ilizuia mechi za VPL na FDL kuchezwa mpaka hapo vitakapokuwa vimefanyiwa marekebisho ili kukidhi sifa za kutumiwa kwa mechi hizo.
Viwanja vinavyokaguliwa ni Ali Hassan Mwinyi (Tabora), CCM Kirumba (Mwanza), Jamhuri (Dodoma), Jamhuri (Morogoro), Kaitaba (Bukoba), Kambarage (Shinyanga), Kumbukumbu ya Karume (Musoma) na Kumbukumbu ya Samora (Iringa).
Kumbukumbu ya Sokoine (Mbeya), Lake Tanganyika (Kigoma), Mabatini (Pwani), Majimaji (Songea), Mbinga (Mbinga), Mkwakwani (Tanga), Mwadui (Shinyanga), Wambi (Mufindi, Iringa), Sheikh Kaluta Amri Abeid (Arusha), Umoja (Mtwara) na Vwawa (Mbozi).
Vyama vya mpira wa miguu vya mikoa husika na mameneja wa viwanja husika wanatakiwa kuwapa ushirikiano wakaguzi hao kutoka TFF.

Uwanja wa Kaitaba nao ni moja ya uwanja utakaokaguliwa na maofisa hao kutoka TFF
Waamuzi wa mtanange wa VPL wakiucheki sawasawa uwanja wa Kaitaba katika mechi zilizopita za msimu wa kwanza.


KUNDI C la Orange CHAN 2014, Mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza ndani ya Nchi zao, zimecheza Mechi zake kwa Ghana kuifunga Congo 1-0 na Libya kuibamiza Ethiopia Bao 2-0.
Shujaa wa Ghana ni Theophilus Anobaah aliefunga Bao katika Dakika ya 35.
Katika Mechi iliyofuata ya Kundi C, Libya iliichapa Ethiopia Bao 2-0 kwa Bao z a Elmutasem Abushnaf kwenye Dakika ya 4 na Bao la Dakika ya 83 la Abdulsalam Omar.
Jumanne leo zipo Mechi mbili za Kundi D kati ya Congo DR v Mauritania na Gabon v Burundi.
CHAN 2014
RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi Januari 11
South Africa 3 v  Mozambique 1
Mali 2  v Nigeria 1
Jumapili Januari 12
Zimbabwe 0 v Morocco 0
Uganda 2 v Burkina Faso 1
Jumatatu Januari 13
Ghana 1 v Congo 0
Libya 2 v Ethiopia 0
Jumanne Januari 14
18:00 Congo DR v Mauritania [Peter Mokaba Stadium]
21:00 Gabon v Burundi [Peter Mokaba Stadium]
Jumatano Januari 15
18:00 South Africa v Mali [Cape Town Stadium]
21:00 Nigeria v Mozambique [Cape Town Stadium]
Alhamisi Januari 16
18:00 Zimbabwe v Uganda [Athlone Stadium]
21:00 Burkina Faso v Morocco [Athlone Stadium]
Ijumaa Januari 17
1800 Ghana v Libya [Free State Stadium]
2100 Ethiopia v Congo [Free State Stadium]
Jumamosi Januari 18
18:00 Congo DR v Gabon [Peter Mokaba Stadium]
21:00 Burundi v Mauritania [Peter Mokaba Stadium]
Jumapili Januari 19
20:00 Nigeria v South Africa [Cape Town Stadium]
20:00 Mozambique v Mali [Athlone Stadium]
Jumatatu Januari 20
20:00 Burkina Faso v Zimbabwe [Athlone Stadium]
20:00 Morocco v Uganda [Cape Town Stadium]
Jumanne Januari 21
20:00 Ethiopia v Ghana [Free State Stadium]
20:00 Congo v Libya [Peter Mokaba Stadium]
Jumatano Januari 22
20:00 Burundi v Congo DR [Peter Mokaba Stadium]
20:00 Mauritania v Gabon [Free State Stadium]
ROBO FAINALI
Jumamosi Januari 25
18:00 [Mechi Na 26] Mshindi Kundi B v Wa Pili Kundi A [Cape Town Stadium]
21:30 [Mechi Na 25] Mshindi Kundi A v Wa Pili Kundi B [Cape Town Stadium]
Jumapili Januari 26
18:00 [Mechi Na 28] Mshindi Kundi D v Wa Pili Kundi C [Peter Mokaba Stadium]
21:30 [Mechi Na 27] Mshindi Kundi C v Wa Pili Kundi D [Free State Stadium]
NUSU FAINALI
Jumatano Januari 29
18:00 [Mechi Na 29] Mshindi Mechi Na 25 v Mshindi Mechi Na 28 [Free State Stadium]
21:30 [Mechi Na 30] Mshindi Mechi Na 27 v Mshindi Mechi Na 26 [Free State Stadium]
Jumamosi Februari 1
18:00 Mshindi wa Tatu [Cape Town Stadium]
21:00 Fainali [Cape Town Stadium]

Cristiano Ronaldo, na mkewe  Irina Shayk.
Mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo jana usiku alinyakua tuzo ya mchezajii bora wa soka wa fifa wa mwaka 2013 na kuwashinda Lionel Messi wa Barcelona na Frank Ribery wa Bayern Munich.
Ronaldo ambaye alinyakuwa tuzo hiyo ya mchezaji bora wa dunia kwa mara kwanza mwaka 2008 alitangazwa kunyakua tuzo mwaka 2013 baada ya kupigiwa kura na makocha, manahodha na waandishi wa habari.
Kwa mujibu wa matokeo Ronaldo alipata kura 1365 akimshinda Messi aliyepata kura 1,205 na Ribery akiambulia kura 1,127.
Kwa upande wa wanawake golikipa wa Ujerumani Nadine Angerer alinyakuwa tuzo ya fifa ya mchezaji bora wa soka kwa upande wanawake huku aliyekuwa kocha wa Bayern Munich Jupp Heynckes akinyakua tuzo ya kuwa kocha bora wa
dunia
 
.
PLAYER WINNING YEARS
Lionel Messi '09, '10, '11, '12
Johan Cruyff '71, '73, '74
Michel Platini '83, '84, '85
Marco van Basten '88, '89, '92
Alfredo Di Stefano '57, '59
Franz Beckenbauer '72, '76
Kevin Keegan '78, '79
K-H. Rummenigge '80, '81
L. Ronaldo '97, '02
Cristiano Ronaldo '08, '13
Cristiano Ronaldo akimwaga machozi mara tu baada ya kutajwa kuwa ndie mshindiCristiano Ronaldo
Pele nae machozi Mhhh.........Lionel Messi,na mkewe  AntonellaPele, Sepp Blatter PeleThe FIFA "dream team" with the best goal keeper, defenders, midfielders and forwards stands on the stage at the FIFA Ballon d'Or 2013 Gala in ZurichBrazilian super model Adriana Lima, right, and Jerome Valcke FIFA General Secretary, participate in the FIFA Ballon d'Or 2013 galaZlatan Ibrahimovic
Sweden's Zlatan Ibrahimovic displays the Puskas award for the best goal at the FIFA Ballon d'Or 2013 Gala in Zurich
Jupp Heynckes - best world coach


Pele
 Roy Hodgson


Kiasi ya watu 200 kutoka Sudan Kusini wamefariki leo Jumanne katika ajali ya feri katika Mto Nile wakati wakikimbia mapigano katika mji wa Malakal.
Südsudan Kämpfe Flüchtlinge in Bor Wananchi wa Sudan kusini wakikimbia mapigano
Taarifa zinazopatikana kutoka Sudan Kusini zinasema watu kati ya 200 na 300, ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto wamekufa maji katika ajali hiyo ya feri. Chombo hicho kilikuwa na watu wengi kuliko uwezo wake, amesema msemaji wa jeshi Philip Aguer.
Ameongeza kuwa wote wamefariki. Walikuwa wakikimbia mapigano ambayo yalizuka tena katika mji wa Malakal.
Mapigano yanaendelea
Mapigano yameendelea katika maeneo mbali mbali leo(14.01.2014) katika Sudan ya kusini . Mapigano makali yameripotiwa kutokea katika mji wa Malakal, mji mkuu wa jimbo linalotoa mafuta kwa wingi la Upper Nile, wakati waasi walipofanya mashambulizi mapya kuukamata mji huo, ambao umekuwa ukibadilisha udhibiti mara mbili kati ya waasi na jeshi la serikali tangu mzozo huo kuanza Desemba 15 mwaka jana nchini Sudan Kusini.
Konflikt im Südsudan Regierungssoldaten 25.12.2013Wanajeshi wa serikali wakipambana na waasi
Kuna mapigano mapya ndani na nje ya mji wa Malakal, amesema mkuu wa misaada ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Sudan kusini Toby Lanzer, na kuongeza kuwa kituo cha jeshi la kulinda amani limefurika karibu mara mbili ya idadi ya watu wanaohitaji hifadhi, kutoka 10,000 hadi 19,000.
Jeshi limeripoti kutokea mapigano makali kusini mwa mji wa Bor, wakati serikali ilitaka kuudhibiti tena mji wa huo kutoka kwa waasi, mji mkubwa pekee ambao bado uko katika udhibiti wa waasi.
Hata hivyo amekataa madai ya waasi kuwa wamekamata tena bandari ya Mongola katika mto Nile, mji iliyopo kati ya mji wa Bor na mji mkuu Juba.
Pia amethibitisha kuwa kumekuwa na mapigano makali kusini mwa mji mkuu, katika mji wa Rajaf jana.
Malakal in Südsudan Mji wa Malakal
Miili yatapakaa barabarani
Wakati huo huo miili kadha ya watu , ikiwa ni pamoja na miili ambayo imeharibika imetapakaa barabarani kutoka uwanja wa ndege hadi katika mji mkuu wa jimbo linalotoa mafuta kwa wingi nchini Sudan kusini la Unity. Nyumba na majengo mbali mbali pamoja na maduka yamechomwa moto ama kuharibiwa na kumekuwa na uporaji mkubwa, huku magari yaliyoharibiwa na kuchomwa moto yakifuka moshi.
Matokeo ya vita mjini Bentiu na uharibifu uliotokea katika taifa hilo jipya duniani yanaonekana wazi, wakati jeshi la serikali likiendelea kupambana na wanajeshi ambao walilitumikia jeshi hilo mwezi mmoja uliopita, ambao hivi sasa wanaitwa waasi.
Hayo yakiendelea viongozi wa Japan na Ethiopia wamezitaka pande zinazopigana nchini Sudan Kusini kutia saini makubaliano ya kusitisha mapigano ambayo yamesababisha maelfu ya watu kuuwawa.
"Tumekubaliana kuwa usitishaji wa uhasama nchini Sudan Kusini na mapatano ya kitaifa ni muhimu sana," waziri mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn, amesema katika mkutano wa pamoja na waandishi habari akiwa na mwenzake wa Japan, Shinzo Abe.
Äthiopien Ministerpräsident Hailemariam Desalegn Waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn
Matamshi hayo yamekuja huku mazungumzo ya amani mjini Addis Ababa kati ya pande hasimu nchini Sudan kusini yakiendelea mjini Addis Ababa. Ethiopia na Japan zimesema zinataka uthabiti nchini Sudan Kusini, nchi ambayo imepata uhuru mwaka 2011 kutoka Sudan.


Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier amesema ujenzi wa makaazi ya walowezi unaoendelezwa na Israel unahujumu mazungumzo ya kutafuta amani Mashariki ya kati.
Waziri huyo wa mambo ya nje wa Ujerumani alikuwa Israel jana kwa ziara ya siku moja ili kuzungumzia mchakato wa kupatikana suluhu ya amani kwa mzozo wa muda mrefu wa mashariki ya kati siku ambayo ilitawaliwa zaidi na mazishi ya aliyekuwa waziri mkuu wa Israel Ariel Sharon.
Steinmeier alikutana na mpatanishi mkuu wa Israel Tzipi Livni kisha kuhudhuria mazishi ya Sharon kabla ya kusafiri hadi Ramallah kukutana na rais wa mamlaka ya ndani ya Palestina Mahmud Abbas.
Ujenzi usiwe kikwazo
Akizungumza na waandishi habari baada ya kukutana na Abbas,Steinmeier alisema mazungumzo yanayoendelea kati ya Palestina na Israel yaliyofufuliwa mwezi Julai mwaka jana, hayapaswi kutatizwa na matangazo ya kila mara kutoka Israel ya kujenga makaazi mapya ya walowezi katika ukingo wa magharibi na mashariki mwa Jerusalem.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Wiki iliyopita, siku chache tu baada ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry kuzuru Mashariki ya kati ili kupiga jeki mchakato wa kupatikana amani,Israel ilitangaza mipango ya kujenga makaazi mapya 1800 na kuzua shutuma kali kutoka Marekani na Umoja wa Ulaya.
Steinmeier amesema wakati ni sasa kwa pande zote mbili kujizatiti ili ipatikane suluhu la kudumu.
Mpatanishi mkuu wa Palestina Saeb Erakat amesema nchi yake inafanya kila iwezalo kufanikisha mchakato huo wa amani na kuitaka Ujerumani na umoja wa Ulaya kuishinikiza Israel kuhusu ujenzi huo tete.
Sehemu ya makaazi ya walowezi yanayojengwa na Israel Sehemu ya makaazi ya walowezi yanayojengwa na Israel
Ujerumani imekuwa ikichukulika mshirika wa karibu wa Israel kutoka bara Ulaya tangu kukamilika kwa vita vikuu vya pili vya dunia lakini katika kipindi cha hivi karibuni imekuwa kitoa shinikizo kwa waziri mkuu wa isreal Benjamin Netanyahu kujizuia kuendelea na ujenzi katika maeneo yanayozozaniwa ya Palestina ili kutotatiza juhudi za kutafuta amani Mashariki ya kati zinazoongozwa na Marekani.
Baada ya kufanya mazungumzo na viongozi wa Palestina,Steinmeier alirejea Jerusalem alikoandaliwa dhifa ya chakula cha jioni na mwenzake wa Israel Avigdor Lieberman na baadae kurejea Ujerumani.
Mwezi ujao Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anatarajiwa kwenda Israel kujibu mualiko wa waziri mkuu Benjamin Netanyahu na kushiriki katika mazungumzo ya pamoja kati seikali hizo mbili.


Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya FIFA ya mchezaji bora wa mwaka Ballon d'Or. Ujerumani ilinyakua tuzo tatu, wakati Jupp Heynckes na Silvia Neid wakishinda tuzo ya makocha bora
Nadine Angerer akiibuka mchezaji bora mwanamke. Katika sherehe za kila mwaka za Ballon d'Or mjini Zurich, Shirikisho la Soka Ulimwenguni - FIFA lilimtaja Cristiano Ronaldo kama mchezaji bora ulimwenguni katika msimu wa mwaka wa 2012/2013. Mreno huyo alipigiwa kura na kumpiku nyota wa Barcelona Muargentina Lionel Messi na Mfaransa Frank Ribery wa Bayern Munich. Kama Messi angeshinda, tuzo hiyo ingekuwa yake ya tano mfululizo.
“Namshukuru kila mmoja, wachezaji wenzangu, timu ya taifa na familia yangu, kila mtu hapa” alisema Ronaldo aliyebubujikwa machozi.
“Sina maneno mengine ya kuielezea hali hii” aliongeza. CR7 alishinda tuzo hiyo ya FIFA ya mchezaji bora ulimwenguni mara ya mwisho katika mwaka wa 2008.
Jupp Heynckes aliwabwaga Jurgen Klopp na Alex Ferguson kwa kunyakua tuzo ya kocha bora wa mwaka Jupp Heynckes aliwabwaga Jurgen Klopp na Alex Ferguson kwa kunyakua tuzo ya kocha bora wa mwaka
Mfaransa Franck Ribery alipigiwa upatu kushinda tuzo hiyo, kufuatia jukumu lake alilotekeleza katika klabu yake ya Bayern Munich, kushinda taji la Bundesliga, DFB Pokal na Champions League katika msimu wa 2012/2013. Pia alinyakua tuzo ya Shirikisho la Soka Ulaya – UEFA, mchezaji bora wa msimu wa 2012/2013.
Mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi pia alikuwa kwenye orodha hiyo. Nyota huyo wa Barca alishinda mataji ya Ballon d'Or kwa miaka mitano mfululizo.
Ujerumani yashinda mataji matatu
Jupp Heynckes, kocha wa Bayern Munich katika msimu uliotangulia, alinyakua tuzo ya FIFA ya Kocha Bora wa Mwaka baada ya kuiongoza timu yake katika kutwaa mataji matatu.
Kocha mwenzake Mjerumani ambaye anaiongoza timu ya taifa ya wanawake Silvia Neid, alishinda tuzo hiyo kwa mara ya pili kwa upande wa wanawake. Aliishukuru FIFA kwa “kuitambua kandanda ya wanawake”.
Uwanjani katika soka la wanawake, mlinda lango wa Ujerumani na nahodha wa timu ya taifa Nadine Angerer, ambaye ni mchezaji bora wa mwaka barani Ulaya, alimpiku Mbrazil Marta na Abby Wambach wa timu ya taifa ya Marekani.
Mwandishi: Bruce Amani/DW/AFP/DPA
Mhariri: Mohammed Khelef

Wamisri wameanza kuteremka vituoni kutoa maoni yao kuhusu katiba mpya, hatua inayoangaliwa kama kipimo cha umashuhuri wa jeshi lililomng'owa madarakani Mohammed Mursi, huku tayari kukiwa na taarifa za mashambulizi.
Wamisri wanapiga foleni wakisubiri kupiga kura
Jenerali Abdel Fatah al-Sisi, makamo waziri mkuu, waziri wa ulinzi na mtu pekee mwenye usemi katika nchi hiyo yenye wakaazi wengi zaidi miongoni mwa nchi za ulimwengu wa Kiarabu amewatolea wito wapiga kura milioni 53 "wateremke kwa wingi" vituoni na wapige kura ya "ndio".
Amesema pia atapigania kiti cha urais baadaye mwaka huu, ikiwa "umma utamtaka afanye hivyo" na kama jeshi litamuunga mkono.
Katiba mpya imetungwa na tume iliyoteuliwa na serikali ya mpito iliyoundwa na Jenerali al-Sisi tangu Julai tatu mwaka jana, baada ya kutangaza kupinduliwa na kukamatwa Mohamed Mursi, rais wa kwanza ambaye si mwanajeshi, aliyechaguliwa kwa njia za kidemokrasia nchini Misri.
Tangu wakati huo, na wakijivunia uungaji mkono wa wananchi walio wengi, utawala unaoongozwa na jeshi unamkandamiza kila unayemfikiria kuwa ni mfuasi wa Mohammed Mursi na hasa wale wa chama chake cha Udugu wa Kiislam.
Zaidi ya waandamanaji elfu moja wameuwawa miezi ya hivi karibuni na wafuasi wa Mursi kutiwa ndani kwa maelfu ingawa baadhi wanaendelea kuandamana kila kukicha huku Udugu wa Kiislam ukitoa wito wa kususiwa kura ya maoni ya katiba.
Ulinzi umeimarishwa
Wanajeshi wanalinda usalama katika kituo cha kupiga kura
Sambamba na hayo mashambulizi yameongezeka ikiwa ni pamoja na mjini Cairo, huku wanamgambo wa itikadi kali wanaoshirikiana na al-Qaida waakidai kuhusika. Lakini serikali imekuwa ikiwatuhumu Udugu wa Kiislam kupanga mashambulizi kama hayo na imelitangaza kuwa ni miongoni mwa makundi ya kigaidi.
Leo asubuhi, muda mfupi kabla ya kura ya maoni kuanza, bomu limeripuliwa karibu na korti moja mjini Cairo, lakini hakuna aliyejeruhiwa. Baada ya mashambulizi hayo, watu kadhaa walikusanyika mbele ya korti hiyo wakionyesha mabango yenye picha za Jenerali al-Sisi.
Ili kulinda amani wakati wa zoezi hili la kura ya maoni litakalodumu siku mbili, serikali ya mpito imewaweka wanajeshi kati ya laki moja na 60 elfu na laki mbili kote nchini Misri.
Polisi na wanajeshi wamewekwa karibu na kituo cha kupiga kura katika shule moja mjini Cairo ambako akinamama kadhaa wamepanga foleni kusubiri kupiga kura.
Kura ya Maoni kama njia ya Kuhalalishwa
Mkuu wa vikosi vya wanajeshi,jenerali Al Sisi
Baadhi ya mashirika ya haki za binaadamu yanaikosoa kura hii ya maoni inayofanyika katika hali ya woga na kukandamizwa upande wa upinzani, lakini idadi kubwa ya wananchi wanaonyesha kuunga mkono utawala mpya na Jenerali al-Sisi ambaye picha zake zimetundikwa katika kila pembe ya mji mkuu.
Kwa maoni ya wataalamu, utawala mpya unaiangalia kura hii ya maoni kama njia ya kuhalalishwa kupitia vituo vya uchaguzi kile ambacho wapinzani wanakiita "mapinduzi ya kijeshi".
Mwandishi: Hamidou Oummilkheir/AFP/dpa
Mhariri: Mohammed Khelef


.Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo ilithibitisha kumtimua kocha huyo na kushukuru kwa mchango wake pamoja na jopo la wasaidizi wake kwa kazi walioifanya katika kipindi chote na kuwatakia kila la heri. Kwasasa timu hiyo itakuwa chini ya kocha wa muda Mauro Tassotti wakati ukifanyika mchakato wa kutafuta kocha mpya atakayeziba nafasi ya Allegri. Barbara ambaye ni binti wa mmiliki wa klabu hiyo Silvio Berlusconi alimshambulia waziwazi Allegri mara baada ya kipigo kutoka kwa Sassuolo kuwa kulitakiwa kufanyika mabadiliko ya haraka kutokana na matokeo mabovu ya timu hiyo.
HATIMAYE klabu ya AC Milan imeamua kumtimua kocha wake Massimiliano Allegri ikiwa ni siku moja baada ya kipigo cha mabao 4-3 kutoka kwa Sassuolo ambao wamepanda ligi msimu huu. Milan kwasasa inashika nafasi ya 11 katika Serie A wakiwa nyuma ya vinara Juventus kwa alama 30 na alama 20 nyuma ya Napoli ambao wanashika nafasi ya tatu ambayo ni ya mwisho kwa timu zinafuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya
  

waliotembelea blog