Tuesday, January 14, 2014


.Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo ilithibitisha kumtimua kocha huyo na kushukuru kwa mchango wake pamoja na jopo la wasaidizi wake kwa kazi walioifanya katika kipindi chote na kuwatakia kila la heri. Kwasasa timu hiyo itakuwa chini ya kocha wa muda Mauro Tassotti wakati ukifanyika mchakato wa kutafuta kocha mpya atakayeziba nafasi ya Allegri. Barbara ambaye ni binti wa mmiliki wa klabu hiyo Silvio Berlusconi alimshambulia waziwazi Allegri mara baada ya kipigo kutoka kwa Sassuolo kuwa kulitakiwa kufanyika mabadiliko ya haraka kutokana na matokeo mabovu ya timu hiyo.
HATIMAYE klabu ya AC Milan imeamua kumtimua kocha wake Massimiliano Allegri ikiwa ni siku moja baada ya kipigo cha mabao 4-3 kutoka kwa Sassuolo ambao wamepanda ligi msimu huu. Milan kwasasa inashika nafasi ya 11 katika Serie A wakiwa nyuma ya vinara Juventus kwa alama 30 na alama 20 nyuma ya Napoli ambao wanashika nafasi ya tatu ambayo ni ya mwisho kwa timu zinafuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya
  

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog