Rooney na Welbeck wakipongezanaWelbeck ndie aliyeanza kuifungia bao la mapema dakika ya 13 United
Asubuhi hii Manchester United waliifunga LA Galaxy Bao 7-0 Uwanjani Rose Bowl, Pasadena, California mbele ya Mashabiki 86,432 katika Mechi ya kwanza chini ya Meneja wao mpya Louis van Gaal na kutwaa Kombe la Chevrolet.
Dakika ya 13 Danny Welbeck ameifungulia mlango wa mabao Man United baada ya kupata pasi kuoka kwa Juan Mata na bao hilo likiwa la Mbali kama yadi 25.
Wayne Rooney aliwapatia bao la pili kupitia kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 41 baada ya Valencia kufanyiwa ndivyo sivyo eneo la penati.
Dakika za mwishoni dakika ya 45 Wayney Rooney aliwafungia United bao la tatu na kufanya mtanange kwenda mapumziko zikiwa 3-0 dhidi ya Wenyeji La Galaxy.Rooney akikatiza mbele kipa wa LA Galaxy na kufunga bao!Wayney Rooney akichonga penati katika kipindi cha kwanzaRooney aki[pongezwa.
Kipindi cha pili dakika ya 63 Reece James aliwafungia bao la 4 United na kufanya 4-0 baada ya kupata mpira kutoka kwa Ashley
Young.
Reece James aliwafungia bao la tano na kufanya 5-0 dhidi ya LA Galaxy katika dakika ya 84 ya Mchezo kipindi cha pili dakika zikiyoyoma.
Dakika ya 88 Ashley Young anaifungia bao la sita na kufanya 6-0 dhidi ya LA Galaxy baada ya kupata mpira kutoka kwa Ander Herrera.Herrera aliongoza sana kwa kutoa mapande kwa wenzakeNani akibanwa James akipongezwa kwa kufunga bao la pili
Dakika ya 90 Ashley Young anaifungia bao tena United katika dakika za lala salama baada ya kupewa pasi na Ander Herrera.
Nyota wa mchezo huo alikuwa ni Mchezaji mpya wa Man United Ander Herrera alietanda katikati ya Uwanja na kutoa pasi murua. Mechi inayofuata kwa Man United ni hapo Jumamosi Julai 26 dhidi ya AS Roma Sports Authority Field, Denver ikiwa ni Mechi ya Kundi A kugombea International Champions Cup
Wafungaji: Welbeck, 13', Rooney (pen) 41, 45, James, 62, 84, Young 88, 90.

0 maoni:
Post a Comment