WAYNE Rooney amempagawisha Kocha Louis van Gaal
mazoezini. Wakati kikosi cha Manchester United kikiwa kwenye maandalizi
ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu England huko Marekani, straika
Rooney alionyesha maajabu mazoezini na kumfanya kocha kupagawa.
Kocha Van Gaal alimkimbilia Rooney na kumkumbatia
baada ya straika huyo kufunga moja kwa moja kwa mpira wa kona aliopiga
mazoezini juzi Alhamisi.
Baada ya kuonyesha kiwango hicho kwa kupiga kona
na kutinga moja kwa moja wavuni, Van Gaal hakuna njia nyingine iliyobora
kumpongeza mchezaji huyo zaidi ya kumfuata na kumkumbatia.
Akiwa hana siku nyingi kwenye kikosi hicho cha Man
United, tayari Van Gaal amejikusanyia mashabiki wengi kutokana na
kufurahishwa na mbinu zake mazoezini.
Kwenye mazoezi ya juzi Van Gaal alikuwa akiwanoa
wachezaji wake namna ya kupiga mipira iliyokufa ndipo Rooney alipopiga
kona na kwenda moja kwa moja wavuni. Kocha Van Gaal anaonekana kuwa na
bahati ya mastaa wake kufanya maajabu ndani ya uwanja baada ya straika
wake mwingine, Robin van Persie kufunga kwa kichwa kwa staili ya ajabu
kwenye fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil mwaka huu wakati Uholanzi
ilipoichapa Hispania mabao 5-1 mwezi uliopita.
Mwanzoni ilidhaniwa kwamba Rooney angekuwa kwenye
wakati mgumu chini ya Van Gaal, lakini kwa sasa mambo yamekuwa tofauti
na staa huyo anaonekana kuelewana na kocha wake mpya tangu alipotua
kwenye kikosi hicho cha Old Trafford.
Man United inafanya mazoezi California na Alfajiri
ya leo Alhamisi ilitarajiwa kumenyana na LA Galaxy kwenye mchezo wao wa
kwanza wa kirafiki wa kujiandaa na msimu mpya.
Man United ambayo ilidai kwamba mwaka huu itafanya
usajili utakaovunja rekodi ya uhamisho Uingereza ni miongoni mwa timu
zitakazocheza Kombe la Chevrolet linalozishirikisha pia Washington DC,
Detroit, AS Roma, Inter Milan na Real Madrid.
0 maoni:
Post a Comment