Saturday, July 26, 2014

Sir Alex Ferguson anatarajiwa kukutana na Meneja mpya wa Man United Louis van Gaal wa Manchester United ambaye kwa sasa yupo kwenye Ziara huko Washington, Marekani.Sir Alex, ambae alistaafu kutoka wadhifa wake wa Miaka 26 kama Meneja Klabu hiyo Mei Mwaka Jana, ataruka kwenda huko Marekani kushuhudia Man United ikicheza na Inter Milan hapo Jumatano na kisha Real Madrid.
Hii Leo Man United ipo Denver kupambana na AS Roma kwenye Mechi ya Kundi A la International Champions Cup.

Kocha Van Gaal kwenye picha na Wafanyakazi wa kitengo cha "Denver fire department" huko kwenye Ziara US.

Van Gaal pia ametoa tiketi kwa ajili ya kiingilio cha leo na kati yao Manchester United v AS Roma

Wakati huo huo Wayne Rooney anaamini Manchester United inaweza kutwaa Ubingwa wa England Msimu ujao chini ya Meneja Louis van Gaal na pia amesema anapenda awe Nahodha wa Timu hiyo.
Man United ambao wako kwenye Ziara ya Mazoezi huko USA, Juzi Jumatano iliichapa LA Galaxy Bao 7-0 huku Rooney akipiga Bao 2 lakini kwenye Mechi hiyo Darren Fletcher ndie aliteuliwa kuwa Nahodha.
Ingawa Msimu uliopita walimaliza Nafasi ya 7 lakini Rooney amesema: “Tunaweza kutwaa Ubingwa. Msimu uliopita ulikuwa mbaya, tunajua hilo, lakini tuaamini tunaweza kuweka mambo sawa. Lazima tuamini tunaweza kuwa Mabingwa!”
Huku Wachambuzi wengi wakidai Robin van Persie ndie atateuliwa Nahodha wa Man United hasa kwa vile ndie alikuwa Nahodha wa Kikosi cha Netherlands chini ya Van Gaal huko Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia, Rooney amesema: “Ni kweli napenda kuwa Nahodha lakini ni uamuzi wa Meneja!”
Vile vile Rooney anamini kuwa Mfumo wa Van Gaal wa kuchezesha Mastraika wawili, kwenye Fomesheni ya 5-2-3 utawanufaisha hasa yeye.

Just a kid: Mourinho says he didn't want to sign Shaw because of his extraordinary wage demands
Mtoto: Mourinho amesema hakutaka kumsajili Shaw kwasababu mshahara wake ni mkubwa sana.

Imechapishwa Julai 26, 2014, saa 7:20 mchana

JOSE Mourinho amesema hakuthubutu kutaka kumsajili Luke Shaw kwasababu mshahara aliohitaji kinda huyo `ungeua umoja' wa timu kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
Shaw mwenye miaka 19, alisaini Manchester United kwa dau la paundi milioni 30 na inasemekana atakuwa analipwa mshahara wa paundi laki moja na elfu 20.
Mourinho alisema kiwango hicho ni kikubwa sana kwa klabu yake.
‘Kama unamlipa mshahara mkubwa kijana mwenye miaka 19 Luke Shaw, tulikuwa tunahitaji nini?, tungekufa' alisema kocha wa Chelsea. "Tungeua umoja na utulivu wetu katika matumizi ya hela. Tungeua umoja kwenye vyumba vya kubadilishia nguo".
"Kwasababu unapomlipa zaidi mtoto wa miaka 19-mchezaji mzuri, wa ajabu-siku inayofuata, mimi na (Mkurugenzi wa Chelsea) bwana Mrs Granovskaia na (mkurugenzi wa ufundi) Michael Emenalo tutagongewa milango na wachezaji wakisema inawezekanaje tumeichezea klabu mechi 200 na kushinda hili na lile, lakini bwana mdogo anatuzidi mshahara?
New mould: Diego Costa, Cesc Fabregas and Filipe Luis joined Chelsea this summer, along with Didier Drogba
Kifaa kipya: Diego Costa, Cesc Fabregas na Filipe Luis wamejiunga na Chelsea majira haya ya kiangazi, sambamba na Didier Drogba.

"Inawezekanaje kijana wa miaka 19 anakuja hapa na kupata hela ambazo hata mimi sipati? ningeua usawa wa timu na nisingeruhusu hilo kutokea".
'Filipe Luis aliichezea Brazil, ameshinda makombe ya Ulaya, alicheza nusu fainali ya UEFA, huyu mchezaji ni bei rahisi kuliko huyu mtoto wa England?
"Sikosoi klabu nyingine kwa kumlipa vile. Lakini kwa klabu yangu, tunaweza kusema ingekuwa mbaya kwetu".
Comparing: Mourinho noted how Filipe Luis cost much less than the 'English young lad' Shaw
 Mourinho alisema inawezekanje Filipe Luis anakuwa na bei rahisi kuliko mtoto wa England, Shaw.

Happy in red and black: Mario Balotelli looks as if he won't be moving from AC Milan this summer
Ana furaha katika rangi nyekundu na nyeusi: Mario Balotelli anaonekana kama vile ataondoka katika klabu ya  AC Milan majira haya ya kiangazi.

Imechapishwa Julai 26, 2014, saa 7:45 mchana

DHAMIRA ya Arsenal kutaka kumsajili Mario Balotelli inaonekana kufa , baada ya Mkurugenzi wa AC Milan,  Adriano Galliani kudai mshambuliaji huyo mtukutu atabakia klabuni hapo.
Mshambuliaji huyo wa kati wa zamani wa Manchester City amekuwa akihusishwa kujiunga na Aserne Wenger na hata Rais wa Ac Milan,  Silvio Berlusconi alikaririwa mapema majira ya kiangazi akisema: 'Nilikuwa namuuza Balotelli kwa timu za England kwa mamilioni ya fedha".
Hata hivyo,  Galliani amejitokeza na kusema hakuna uwezekano wa nyota huyo kutua England kwasababu mshambuliaji huyo mwenye miaka 23 yupo katika mipango ya klabu msimu ujao.
Winner: Balotelli celebrates scoring against England for Italy during the World Cup group stages
Mshindi: Balotelli akishangilia baada ya kufunga bao la ushindi katika mchezo wa kombe la dunia hatua ya makundi dhidi ya England.

'Balotelli kamwe hajawahi kuomba kuuzwa,' Alisema Galliani. 'Kuna asilimia 99.9% ana nafasi ya kubakia hapa, lakini huwezi kujua nini kitatokea".
Japokuwa washika bundiki hawajapoteza nafasi kwasababu Mkurugenzi wa Milan aliwahi kusema hivyo hivyo kuhusiana na Mbrazil Kaka, akisema: 'Ni kweli tutambakisha hapa. Nina asilimia 99.9%, atabakia hapa'.
Lakini Kaka aliondoka na kujiunga na Orlando City kwa mkopo kupitia klabu ya Sao Paulo.
Lakini Wenger alikaririwa akisema anafurahia wachezaji alionao safu ya ushambuliaji na kuonekana kama vile amepiga chini dili la kumsajili Balotelli majira haya ya kiangazi mwaka huu.
Him again: Former Man City star Balotelli (left) has been linked with a move to Arsenal
Yeye tena: Nyota wa zamani wa Man City, Mario Balotelli (kushoto) amekuwa akihusishwa kujiunga na Asernal.

Sir Alex Ferguson anatarajiwa kukutana na Meneja mpya wa Man United Louis van Gaal wa Manchester United ambaye kwa sasa yupo kwenye Ziara huko Washington, Marekani.Sir Alex, ambae alistaafu kutoka wadhifa wake wa Miaka 26 kama Meneja Klabu hiyo Mei Mwaka Jana, ataruka kwenda huko Marekani kushuhudia Man United ikicheza na Inter Milan hapo Jumatano na kisha Real Madrid.
Hii Leo Man United ipo Denver kupambana na AS Roma kwenye Mechi ya Kundi A la International Champions Cup.

Kocha Van Gaal kwenye picha na Wafanyakazi wa kitengo cha "Denver fire department" huko kwenye Ziara US.

Van Gaal pia ametoa tiketi kwa ajili ya kiingilio cha leo na kati yao Manchester United v AS Roma

Wakati huo huo Wayne Rooney anaamini Manchester United inaweza kutwaa Ubingwa wa England Msimu ujao chini ya Meneja Louis van Gaal na pia amesema anapenda awe Nahodha wa Timu hiyo.
Man United ambao wako kwenye Ziara ya Mazoezi huko USA, Juzi Jumatano iliichapa LA Galaxy Bao 7-0 huku Rooney akipiga Bao 2 lakini kwenye Mechi hiyo Darren Fletcher ndie aliteuliwa kuwa Nahodha.
Ingawa Msimu uliopita walimaliza Nafasi ya 7 lakini Rooney amesema: “Tunaweza kutwaa Ubingwa. Msimu uliopita ulikuwa mbaya, tunajua hilo, lakini tuaamini tunaweza kuweka mambo sawa. Lazima tuamini tunaweza kuwa Mabingwa!”
Huku Wachambuzi wengi wakidai Robin van Persie ndie atateuliwa Nahodha wa Man United hasa kwa vile ndie alikuwa Nahodha wa Kikosi cha Netherlands chini ya Van Gaal huko Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia, Rooney amesema: “Ni kweli napenda kuwa Nahodha lakini ni uamuzi wa Meneja!”
Vile vile Rooney anamini kuwa Mfumo wa Van Gaal wa kuchezesha Mastraika wawili, kwenye Fomesheni ya 5-2-3 utawanufaisha hasa yeye.

article-0-1FF9BF7800000578-984_634x412Changamoto ya Ugiriki: Claudio Ranieri anatarajia kuiongoza nchi hiyo katika fainali za mataifa ya Ulaya mwaka 2016 
KOCHA wa zamani wa Chelsea, Claudio Ranieri ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya Taifa ya Ugiriki.
Ranieri katika miaka kumi iliyopita amevuna zaidi ya paundi milioni 10, akilipwa kama fidia ya kufukuzwa kazi, lakini Ugiriki umemteua kuwa kocha mkuu wa nchi hiyo.
Ranieri amesaini mkataba wa miaka miwili na anatarajiwa kulibadili soka la nchi hiyo.
Kocha huyo amefukuzwa mara tano (5) katika miaka 10 iliyopita na kuvuna fidia kubwa ya paundi milioni 10.

waliotembelea blog