Sir
Alex Ferguson anatarajiwa kukutana na Meneja mpya wa Man United Louis
van Gaal wa Manchester United ambaye kwa sasa yupo kwenye Ziara huko
Washington, Marekani.Sir Alex, ambae alistaafu kutoka wadhifa wake wa
Miaka 26 kama Meneja Klabu hiyo Mei Mwaka Jana, ataruka kwenda huko
Marekani kushuhudia Man United ikicheza na Inter Milan hapo Jumatano na
kisha Real Madrid.
Hii Leo Man United ipo Denver kupambana na AS Roma kwenye Mechi ya Kundi A la International Champions Cup.
Kocha Van Gaal kwenye picha na Wafanyakazi wa kitengo cha "Denver fire department" huko kwenye Ziara US.
Van Gaal pia ametoa tiketi kwa ajili ya kiingilio cha leo na kati yao Manchester United v AS Roma
Wakati huo huo Wayne Rooney anaamini Manchester United inaweza kutwaa Ubingwa wa England Msimu ujao chini ya Meneja Louis van Gaal na pia amesema anapenda awe Nahodha wa Timu hiyo.
Man United ambao wako kwenye Ziara ya Mazoezi huko USA, Juzi Jumatano iliichapa LA Galaxy Bao 7-0 huku Rooney akipiga Bao 2 lakini kwenye Mechi hiyo Darren Fletcher ndie aliteuliwa kuwa Nahodha.
Ingawa Msimu uliopita walimaliza Nafasi ya 7 lakini Rooney amesema: “Tunaweza kutwaa Ubingwa. Msimu uliopita ulikuwa mbaya, tunajua hilo, lakini tuaamini tunaweza kuweka mambo sawa. Lazima tuamini tunaweza kuwa Mabingwa!”
Huku Wachambuzi wengi wakidai Robin van Persie ndie atateuliwa Nahodha wa Man United hasa kwa vile ndie alikuwa Nahodha wa Kikosi cha Netherlands chini ya Van Gaal huko Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia, Rooney amesema: “Ni kweli napenda kuwa Nahodha lakini ni uamuzi wa Meneja!”
Vile vile Rooney anamini kuwa Mfumo wa Van Gaal wa kuchezesha Mastraika wawili, kwenye Fomesheni ya 5-2-3 utawanufaisha hasa yeye.

0 maoni:
Post a Comment