Ana furaha katika rangi nyekundu na
nyeusi: Mario Balotelli anaonekana kama vile ataondoka katika klabu ya
AC Milan majira haya ya kiangazi.
Imechapishwa Julai 26, 2014, saa 7:45 mchana
DHAMIRA ya Arsenal kutaka kumsajili Mario Balotelli inaonekana kufa , baada ya Mkurugenzi wa AC Milan, Adriano Galliani kudai mshambuliaji huyo mtukutu atabakia klabuni hapo.
Mshambuliaji huyo wa kati wa zamani wa Manchester City amekuwa akihusishwa kujiunga na Aserne Wenger na hata Rais wa Ac Milan, Silvio
Berlusconi alikaririwa mapema majira ya kiangazi akisema: 'Nilikuwa
namuuza Balotelli kwa timu za England kwa mamilioni ya fedha".
Hata hivyo, Galliani amejitokeza na
kusema hakuna uwezekano wa nyota huyo kutua England kwasababu
mshambuliaji huyo mwenye miaka 23 yupo katika mipango ya klabu msimu
ujao.
Mshindi: Balotelli akishangilia baada ya
kufunga bao la ushindi katika mchezo wa kombe la dunia hatua ya makundi
dhidi ya England.
'Balotelli kamwe hajawahi kuomba
kuuzwa,' Alisema Galliani. 'Kuna asilimia 99.9% ana nafasi ya kubakia
hapa, lakini huwezi kujua nini kitatokea".
Japokuwa washika bundiki hawajapoteza
nafasi kwasababu Mkurugenzi wa Milan aliwahi kusema hivyo hivyo
kuhusiana na Mbrazil Kaka, akisema: 'Ni kweli tutambakisha hapa. Nina
asilimia 99.9%, atabakia hapa'.
Lakini Kaka aliondoka na kujiunga na Orlando City kwa mkopo kupitia klabu ya Sao Paulo.
Lakini Wenger alikaririwa akisema
anafurahia wachezaji alionao safu ya ushambuliaji na kuonekana kama vile
amepiga chini dili la kumsajili Balotelli majira haya ya kiangazi mwaka
huu.
Yeye tena: Nyota wa zamani wa Man City, Mario Balotelli (kushoto) amekuwa akihusishwa kujiunga na Asernal.
0 maoni:
Post a Comment