Mwimbaji
kutokea muziki wa dansi, Christian Bella ameongea kwenye AMPLIFAYA ya
Clouds FM July 8, 2015 na kuthibitisha kwamba kukosa tuzo sehemu yoyote
au kwenye tuzo zozote haitampelekea yeye kujiondoa kushirikishwa kwenye
tuzo.
Anaamini
kuna vitu vingine vinatokea kwa binadamu..’Cha muhimu nini unafanya na
jamii inapokea kazi yako vipi waliopata tunawapa hongera ukiangalia
vizuri kuna mapungufu ambayo yalionekana live kwangu mimi nachukulia
powa kwasababu sio mara yangu ya kwanza mimi katika mambo ya tuzo
sinanga hiyo sifa kwamba mimi wananipanga tuzo hapana lakini najitahidi
sana kufanya muziki mzuri aina muziki ninayoufanya ni kufurahisha watu
wote’- Christian Bella
‘Wao
wakijaji kwamba labda kuna vitu gani ili msanii apate kwasababu huwezi
kumpa msanii tuzo eti mwandishi bora wakati hajaandika nyimbo yoyote au
huwezi kuwa mwimbaji bila kuwa na hits haujafanya chochote umetoa nyimbo
haijakubali no mwimbaji bora au mtumbuizaji bora inategemea
alichokifanya mwaka uliopita umezunguka wapi na wapi ili upate hiyo tuzo
unavyoniambia mimi ni dancer bora itabidi nioneshe mwaka jana nilifanya
vitu vya maajabu hata wewe ni dancer bora lakini kama haujafanya kitu
una tuzo siwezi kuwaingilia kitu kabisa’- Christian Bella
‘Siwezi
kuwainglia mambo ya tuzo waendele tu na idea zao wanachokifanya mimi
bella sio lazima tuzo lakini mashabiki wanavyokubali kazi zangu ndio
napata furaha sana wakitoa tuzo na wasipotoa siwezi kujitangaza mara ooh
bella sijui hivi na hivi kuhusu tuzo hapana naomba tu makampuni
yaongezeke ili yawe yanatoa tuzo’- Christian Bella.