Monday, July 21, 2014

image_3

 1970462_1454799778083088_1638018053_n
Komweta Hemed Maneti a.k.a Chiriku mwanamuziki wa bendiya Vijana Jazz
1486871_1427285270834539_2027172492_n
Marehemu Hemedi Maneti Ulaya Chiriku aliyekuwa mwamuziki wa bendi ya Vjana Jazz enzi hizo.
…………………………………………………………………………………………
Komweta Hemed Maneti a.k.a Chiriku ni Mtoto wa mwanamuziki wa zamani marehemu Hemedi Maneti Ulaya Chiriku  aliyekuwa akiimba katika bendi ya umoja wa vijana Vijana Jazz enzi hizo ambapo anasema amekuwa kwenye muziki  kwa muda mrefu japokuwa kama ilikuwa kama kujifurahisha, Komweta Hemed  Maneti alianza muziki kama kazi mwezi Agosti mwaka 2013 akiimba katika bendi ya Vijana Jazz  ambayo marehemu baba yake Mzee Hemedi Maneti Ulaya aliitumikia kwa mafanikio enzi za uhai wake.
Komweta Hemed Maneti a.k.a Chiriku amekuwa akijizolea umaarufu mkubwa katika bendi hiyo kwani mashabiki wengi wamekuwa wakimkumbuka marehemu baba yake mara anapoimba jukwaani kwani kwa kiasi kikubwa sauti zinaendana na marehemu baba yake Hemed Maneti, Bendi ya Vijana Jazz imekuwa ikipata umaarufu siku hadi siku katika maonyesho yake yanayofanyika kwenye klabu ya Kilwa Road Pub  Ijumaa, Jumamosi wanapiga Jet Lumo na Jumapili kwenye  ukumbi wa Vijana Hall Kinondoni.

Komweta mpaka sasa ana Nyimbo mbili na zipo mbioni kutoka  akiwa ameimba kwa kushirikiana na  bendi ya Vijana Jazz  mtunzi akiwa ni yeye mwenyewe nyimbo yake Inaitwa (Walimwengu) na nyingine inaitwa (Nitajuaje) ukiwa ni utunzi wa Shomary Ally lakini yeye akiwa mwimbaji kiongozi katika wimbo huo  pamoja naye Julius Mwesiwa.
Wanamuziki wakongwe waliobaki kwenye bendi ya vijana Jazz ambao waliwahi kuimba na marehemu Hemed Maneti ni Shomary Ally,Abdallah Mgonahazeru na Roshy Mselela,  Ndoto za Komweta Hemed ni kuwa mwanamuziki wa kimataifa na kuipepeprusha vema bendera ya Tanzania ndani na nje ya mipaka ya TANZANIA ameolewa na ana mtoto mmoja wa miaka 5 anayeitwa Fahad. Anaongeza kuwa Changamoto za kazi ya muziki na malezi  ni nyingi lakini muhimu ni kujua jinsi gani utapanga ratiba zako vizuri na kuhakikisha unafanya maandalizi mazuri kwa ajili ya mtoto na hili halinishindi natimiza majukumu yangu vizuri kama mama
Ni kweli kwamba mara nyingi nakuwa nafanya kazi siku za wikiendi  hivyo nakosa muda wa kutosha wa kukaa na mtoto ukizingatia  ndiyo siku na yeye anakuwa anapumzika haendi shule, lakini kama mama unatakiwa kujua majukumu ya familia yako ninafurahia maisha na familia yangu na mtoto wangu ni mweye furaha sana ninamshukuru mungu kwa hilo,
hata hivyo siku za  jumatatu zinakuwa zina changamoto kubwa sana hasa katika kumwandalia mahitaji yake  kwa ajili ya kwenda shule kwakuwa nakuwa nimechoka na kazi. 
Mwanamuziki huyo anasema mashabiki wa bendi ya vijana wamempokea vizuri sana kusema kweli anaongeza kuwa “Nashukuru Mungu sana kwa hilo
na hili linajidhihirisha ninapokuwa nafanya shoo zangu…watu hawakai chini mara nyingi wanakuwa wakicheza…”
Anamaliza kwa kusema “Umaarufu wa marehemu baba yake mzee Hemed Maneti upo na siwezi kuuepuka…lakini kubwa watu wananipima kutokana na utendaji na ufanisi wangu wa kazi yangu niwapo jukwaani”.


Legend: Mourinho (left) brought Drogba to the club in 2004 from Marseille, and his faith paid off
Gwiji: Mourinho (kushoto) alimleta Drogba Chelsea mwaka 2004 kutokea klabu ya Marseille.

Imechapishwa Julai 21, 2014, saa 6:35 mchana

NDOTO ya Didier Drogba kurudi tena Chelsea inatarajia kukamilika wiki hii.
Mazungumzo ya kumpa mkataba wa mwaka mmoja wa ukocha na mshambuliaji wa akiba yamekuwa yakiendelea vizuri na kuelekea kukamilika na gwiji huyo wa darajani mwenye miaka 36 ataungana na kocha wake wa zamani, Jose Mourinho.
Inafahamika kuwa Drogba ameshawatumia ujumbe baadhi ya wachezaji wenzake wa zamani wa Chelsea akieleza kuwa anarudi darajani.
Elsewhere: The 36-year-old has interest from clubs in Qatar while Juventus continue to flirt with the idea
Nyota huyo mwenye miaka 36 amezivutia klabu kadhaa nchni Qatar, wakati Juventus wakipambana namna ya kuinasa saini yake.

Chelsea inataka kupunguza wachezaji wenye umri mkubwa kwenye kikosi chake, lakini inatambua mchango wa Drogba nje na ndani ya uwanjani.
Wanaamini kuwa uzoefu wa mshambuliaji huyo utakuwa na ushawishi mkubwa katika benchi la ufundi na atatoa msaada kwa nyota mpya, Diego Costa.
Chelsea wametumia vizuri majira haya ya kiangazi na wataendelea kuongeza wachezaji, lakini wamempoteza Samuel Eto`o na Demba Ba, wakati Romelu lukaku anaweza kujiunga na  Everton licha ya awali kuwepo kwa mipango ya kumrudisha.
Kuwa kocha mchezaji kutasaidia kwenda na sheria ya matumizi ya fedha kwasababu mshahara wake utaingia kwenye bajeti ya makocha.
Drogba alisaini kwa mara ya kwanza Chelsea miaka 10 iliyopita na kuondoka mwaka 2012.
Kuthibitisha kuondoka kwake, Drogba aliiambia tovuti ya klabu kuwa: "Nataka kumaliza tetesi zote na kuthibitisha kwamba naondoka Chelsea. Yamekuwa maamuzi magumu kwangu kufanya na ninajivunia kwa kile tulichopata".
"Lakini muda wa changamoto mpya kwangu umefika. Kama sehemu ya timu nimesaidia sana na kushinda kila kombe lililowezekana".
Milking the applause: Drogba shows his appeciation to the fans during his last game at Stamford Bridge in blue
Drogba alipokuwa akiwashukuru mashabiki wa Chelsea katika mchezo wake wa mwisho ndani ya dimba la  Stamford Bridge. 

KUFURU REAL MADRID!, DILI LA JAMES RODRIGUEZ KUTUA BERNABEU WIKI HII LAKAMILIKA!

Deal me in: Colombia World Cup ace James Rodriguez is set to sign for Real Madrid on Wednesday+9
Anatua Bernabeu: Mchezaji wa Colombia aliyeng`ara kombe la dunia na kutwaa tuzo ya mfungaji bora, James Rodriguez anatarajia kujiunga na Real Madrid jumatano.

Imechapishwa Julai 21, 2014, saa 5:56 asubuhi

NYOTA wa kombe la dunia, James Rodriguez, jumatano ya wiki hii atasaini mkataba na Real Madrid utakaogharimu ada ya uhamisho ya paundi milioni 60.
Rodriguez alikuwa nchini Hispania jana jumapili akitokea kwao Colombia na anaelekea katika klabu ya Manaco ambapo ataaga wiki hii kabla ya kurudi tena mjini Madrid kusaini mkataba wa miaka sita.
Rais wa Real Madrid , Florentino Perez yuko Marekani kusini kwa masuala ya kibishara, lakini anarejea wiki hii kuhakikisha kuwa mabingwa hao wa Ulaya wanatumia zaidi ya paundi milioni 80 kwa kumuongeza Rodriguez baada ya kumsajili Toni Kroos kutoka Bayern Munich wiki iliyopita kwa dau la paundi miliobi 20. 
Golden boy: Rodriguez is due to sign a six-year contract with the La Liga giants this week
Kijana wa dhahabu: Rodriguez anatarajia kusaini mkataba wa miaka sita wiki hii na miamba ya La Liga.
Keep it up: Real will be hoping the 21-year-old attacking midfielder can replicate his World Cup form
Endelea hivyo hivyo: Real wanaamini nyota huyo mwenye miaka 21 anaweza kuonesha kiwango chake cha kombe la dunia 
Big move: Rodriguez was in Spain on Sunday on his way back from Colombia to Monaco+9
Uhamisho mkubwa: Rodriguez alikuwa Hispania akitokea Colombia na anakwenda Monaco kuaga.

Msimu uliopita, mchezaji Gareth Bale alisajiliwa kwa dau la paundi milioni 85 ambapo Real Madrid walimuuza Mesut Ozil kwenda Asernal kusaidia kupata hela ya kulipa mkwanja huo.
Usajili huu mwingine mkubwa majira haya ya kiangazi, unaweza kusababisha angalau mchezaji mmoja au watatu kuondoka ili kupata hela.
Manchester United wanaiwinda saini ya Angel Di Maria licha ya msimamo wa kocha Carlo Ancelotti kutaka Muargentina huyo abaki klabuni hapo.
Kuvunja benki ili kumnunua Rodriguez kunaweza kuwashawishi zaidi Madrid kumuuza Sami Khedira na kushuka dau walililotaja la paundi milioni 20.



Aliyekuwa mkufunzi wa timu ya soka ya Brazil Luiz Felipe Scolari
Brazil inatarajiwa kumtangaza mkufunzi wake mpya katika mkutano na wanahabari siku ya jumanne kufuatia kujiuzulu kwa kocha wa timu hiyo Luiz Felipe Scolari.
Scolari mwenye umri wa miaka 65 aliiongoza Brazil katika semi fainali za kombe la dunia ambapo timu hiyo ilipata kichapo kibaya cha mabao masaba kwa moja dhidi ya mabingwa wa kombe la Dunia Ujerumani.
Aliyekuwa kocha wa timu hiyo ambaye aliiongoza timu hiyo kati ya mwaka 2006 na 2011 huenda akarejea na kuchukua kazi hiyo.
Wengine wanaopgiwa debe kuchukua kazi hiyo ni mkufunzi wa kilabu ya Corinthians Tite,Mkufunzi wa kilabu ya Sau Paulo Muriciy Ramalho na Vanderlei Luxembourg ambaye aliwahi kuifunza timu hiyo kutoka mwaka 1998 hadi mwaka 2000.


s9
Na Shaffih Dauda
KOCHA wa Timu ya taifa ya Tanzania, Mholanzi, Mart Nooij aliamua kuwaanzisha washambuliaji wanne katika mechi dhidi ya Msumbuji, kuwania kupangwa hatua ya makundi ya kusaka tiketi ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika, AFCON, mwakani nchini Morroco.
Mbwana Ally Samatta, Thomas Ulimwengu, John Bocco `Adebayor` na Mrisho Ngassa, wote kwa pamoja walianza katika sare ya 2-2 ndani ya uwanja wa Taifa, jinini Dar es salaam dhidi ya `Black Mambas`.
Lengo la Nooij lilikuwa ni kushambulia kwa nguvu ili kupata mtaji mkubwa wa mabao kabla ya mechi ya marudiano itakayopigwa wiki mbili zijazo mjini Maputo nchini Msumbiji.
Lakini kwa mtazamo wangu, niliona mapungufu juu ya namna kocha Nooij alivyowapanga washambuliaji hawa. Ulimwengu na Ngassa walicheza pembeni, Samatta na Bocco walisimama katikati.
Mimi naona ingekuwa na tija kama Thomas angecheza katikati kuliko kucheza pembeni ili kupata ubora wa timu.
Kwa timu ilivyoanza yeye alikuwa kulia, katikati alikuwa Mbwana Samatta na John Bocco, kushoto alicheza Mrisho Ngassa na wakawa wanabadilishana.
Lakini mimi naona ingekuwa na tija zaidi kama Thomas Ulimwengu angesimama katikati na John Bocco, halafu samata akawa anashambulia kutoka pembeni upande wa kushoto, halafu Mrisho Ngassa ashambulie kutoka kulia. Kwasababu kwa aina ya uchezaji wa Ulimwengu, walipokuwa wanamuweka pembeni walikuwa wanampatia ugumu.
Alikuwa analazimika apige chenga, apige pasi kutoka eneo alipo, lakini yeye sio aina ya mchezaji wa hivyo vitu, yeye sio mtu wa vitu, yeye ni mtu wa kuwekewa mpira ili awe na chaguo moja tu,  kupiga au kupasia karibia na goli ili kumpa mwenzie afunge, na hapo unaweza kuona ubora wa Thomas Ulimwengu.
Kama Ulimwengu angekuwa katikati ingekuwa ni vizuri zaidi kucheza mipira mirefu waliyokuwa wanacheza akina `Cannavaro` dakika za kipindi cha kwanza. Mara nyingi mipira hii mabeki wa Msumbiji walikuwa wanaicheza, kwasababu John Bocco pamoja  na umbile kubwa, mrefu, lakini sio mzuri kupambana, ni mwepesi, kwahiyo ni mara mia nane angekuwepo Thomas Ulimwengu, kwasababu ni mtu mwenye nguvu na jinsi mwili wake ulivyo angeweza kupambana nao na kutoa mianya kwa akina Ngassa, Samatta au Bocco mwenyewe kufungwa.
Hii ni kwasababu mabeki wa  Msumbiji wangelazimika kuokoa mipira hovyo, na ingedondoka maeneo ambayo wengine wangeokota baada ya mikikimikiki ya Ulimwengu.
Pix-3
Halafu kingine, ile mipira, Ulimwengu angekimbia nayo katoka katikati na kutanua kwenda pembeni. Hii ingetoa nafasi kwa akina Ngassa au Samatta kutegemeana mpira unaenda upande upi.
Mabeki wangelazamika kwenda kukimbiza na kuacha nafasi katikati, na kwasababu yeye ana kasi angewahi ile mipira na kupiga krosi ambazo zingeweza kufungwa na wenzake  kwasababu katikati pale pangeachwa wazi kutokana na mebeki kwenda pembeni kumkimbiza Ulimwengu.
Lakini ilikuwa ni ngumu kwa Ulimwengu kutokea pembeni na kupiga mipira vizuri kwasababu yeye hana uwezo wa kumiliki mpira vizuri, sio mtu wa kuchezea mpira kama akina Ngassa au Samatta mwenyewe.
Unajua Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta, John Bocco wote ni washambuliaji wa kati, lakini wanatofautiana  ujuzi na aina ya uchezaji.
Kama mimi ningekuwa kocha na ningetaka kuwatumia wote kwa wakati mmoja, mara mia nane, huyu Thomas Ulimwengu angesimama katikati, halafu Jonh Bocco au Samatta angeenda pembeni.
Lakini mimi ningependa zaidi Mbwana Samatta atokee pembeni upande wa kushoto, kwasababu ana uwezo, ana kasi, na anaweza kupiga chenga na kutafuta `engo` ya kupiga mpira. Anaweza kupiga chenga, akarudi na kuuzungusha.
Kuthibitisha pointi yangu hiyo, kuna wakati Samatta alikwenda pembeni, alipiga pasi mbili ambazo almanusura zisababishe goli. Alipiga krosi moja ambayo alipigwa kichwa na John Bocco, lakini kipa akacheza.

Akapiga krosi nyingine ambayo beki alitoa ikawa kona. Kwahiyo,  kwayeye kucheza pembeni ilikuwa na faida zaidi kuliko Thomas Ulimwengu.


Khamis Mcha `Vialli` akiwa katika harakati za kufunga katika mechi ya jana dhidi ya Msumbiji


KUTOKANA na kambi iliyowekwa mjini Gaborone nchini Botswana kwa wiki mbili na baadaye mjini Tukuyu mkoani Mbeya, Watanzania wengi walikuwa na matumaini ya kuibuka na ushindi dhidi ya Msumbiji.
Matumaini haya hayakuwa kwa mashabiki tu, hata kwa  benchi la ufundi, viongozi wa soka na wachezaji wote.
Taifa stars jana ililazimishwa sare ya mabao 2-2 na Msumbiji katika mechi ya kuwania kupangwa hatua ya makundi kusaka tiketi ya kucheza fainali za mataia ya Afrika, AFCON, mwakani nchini Morocco.
Mechi hii ilipigwa ndani ya dimba la Taifa jijini Dar es salaam. Wakati mashabiki wakisubiri kuona Stars iliyosheheni wachezaji wote wanaocheza ligi ya ndani na nje ya nchi inafunga mabao, dakika 45 za kipindi cha ziliisha kwa suluhu pacha.
Dakika ya 47 kama sinema vile, Kevin Yondani alimfanyia madhambi mchezaji wa Msumbiji na mwamuzi kutoa penati iliyofungwa na Elias Gasper Pelembe.
Pelembe alifunga bao lake la 10 katika mechi 49 alizoichezea Msumbiji tangu aitwe kwa mara ya kwanza mwaka 2004.
Ni mchezaji anayecheza ligi ya Afria kusini tangu mwaka 2007 alipojiunga na timu ya Supersport United akitokea klabu ya Despotive Maputo.
 Msimu wa 2007/2008 alitwaa ubingwa na klabu ya Supersport United na kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa msimu huo. Alikaa klabuni hapo kwa misimu mitatu na baadaye akasajiliwa na matajiri wa Mamelod Sundowns.
1 (1)
Samir Hajji Nuhu na Khamis Mcha ‘Vialli’ wakimpongeza Gaudence Mwaikimba (katikati) baada kufunga moja ya bao  katika mchezo wa ligi kuu msimu ulipoita ndani ya Uwanja wa Azam Complex 

Baada ya bao hilo, kwa dakika kadhaa, kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij akatafakari na kumuita kijana mmoja wa Kizanzibar na kumueleza jambo la kufanya. Kijana huyu ni Khamis Mcha `Vialli`.
Nooij alimpumzisha Mrisho Ngassa na kumuingiza Mcha aliyeisawazishia Taifa stars bao katika dakika ya 65.
Pia Mcha alifunga bao la pili na la kuongoza kwa mkwaju wa penati baada ya Mbwana Samatta kuangushwa ndani ya eneo la hatari.
Mtandao huu ukaona kufurahia kiwango cha Mcha pekee haitoshi, bali kuna haja ya kujua baadhi ya mambo kuhusu mchezaji huyu mwenye kipaji kikubwa cha soka.

HIVI UNAJUA KWANINI KHAMIS MCHA `VIALLI` ALIENDA KUPIGA PENATI?

Katika mahojiano maalumu na mtandao huu, Mcha alieleza kuwa yeye ni mpigaji mzuri wa penati na amekuwa akifanya vizuri tangu utotoni.
Mcha anasema katika mazoezi ya timu ya Taifa, anapiga sana penati na wenzake wote wanamuamini sana. Ilipotokea penati, hakuona shida kuuchukua mpira na kwenda kupiga.
Mcha anasema baada ya kushika mpira, nahodha wa Taifa Stars,  Nadir Haroub `Cannavaro` akamuonesha ishara ya kumuuliza unapiga?. Anasema alimjibu kwa ishara pia kuwa, ndiyo kamanda!.
Kijana huyu anaendelea kueleza kuwa Thomas Ulimwengu akamtazama na kumwambia, usiogope mwana! . Anasema hakuwa na wasiwasi hata kidogo kwasababu anajua namna ya kupiga na wenzake wanamuamini kwa umahiri wake. Kweli bila kufanya makosa akauzamisha mpira nyavuni.
IMG_3409
SASA SWALI LIKAJE, KWANI MCHA KAANZA KUPIGA PENATI LINI?
Mchezaji huyu mwenye kipaji anasema kuwa alianza kupiga penati zamani sana. Tangu aanze kucheza mpira wa mashindano, ameshapiga penati zaidi ya ishirini na ametia kambani zote na kukosa mbili tu.
Alikosa penati kwenye mechi baina ya Zanzibar Heroes na Kenya kwenye mashindano ya CECAFA nchini Uganda na akakosa penati ya pili kwenye mechi moja ya Azam fc.
Mcha ni mahiri kupiga penati, lakini kijana huyu ni muislam. Waumini wote wa dini ya kiislam wapo katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

KWANI KHAMIS MCHA `VIALLI` YUPO KATIKA MFUNGO?,

 Mchezaji huyu anasema yupo katika mfungo na anasema siku moja kabla ya mechi ya jana mwalimu aliwataja wachezaji watakaoanza katika kikosi cha kwanza na wachezaji wa akiba. Anasema wakati Nooij anataja kikosi cha kwanza, hakusikia jina lake, lakini likasikika katika majina ya wachezaji wa akiba.
Anasema mchezaji anapokuwa kwenye orodha ya wachezaji wa akiba,a naweza kucheza au asicheze katika mechi. Sasa yeye alishika mawili. Cha ajabu, Mcha anasema angeanza mechi ya Msumbiji asingefunga, na alifunga kwasababu alianzia benchi.

MCHA AMEIFUNGIA MABAO MANGAPI TAIFA STARS?

Nyota huyu anasema ni mara ya kwanza kuifungia Stars katika mechi ya mashindano. Lakini amefunga mabao manne mpaka sasa.
Bao moja alifunga katika mechi ya kirafiki baina ya Taifa stars na Namibia iliyomalizika kwa sare ya 1-1 mjini Windhoek. Mcha alifunga bao hilo baada ya kupiga mpira wa kona ulizama moja kwa moja nyavuni.
Bao lingine alifunga katika mechi ya kirafiki dhidi ya Botswana mjini Gaborone ambapo Stars ililala mabao 4-2. Hii ilikuwa mechi ya mwisho ya Stars kujipima ubavu kabla ya mechi ya jana.
Kwahiyo, mpaka sasa Mcha ameifungia Stars mabao manne baada ya kufunga mawili dhidi ya Msumbiji.
Kwa upande wa timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, Mcha anasema mpaka sasa ameifungia mabao 9.
13

BAO LAKE LA KUSAWAZISHA DHIDI YA MSUMBIJI ANALIELEZEAJE?

Mcha anasema kuwa goli alilosawazisha jana linafanana sana na lile alilofunga dhidi ya Botswana. Anafafanua kuwa kule Botswana alirushwa mpira na Oscar Joshua ambapo John Bocco akauparaza kwa kichwa na ukamkuta sehemu nzuri aliyounganisha moja kwa moja mpaka nyavuni kwa mguu wa kushoto.
Katika mechi dhidi ya Msumbiji, Mcha anasema Erasto Nyoni alirusha mpira ambao John Bocco aliruka juu na beki wa Msumbiji lakini hakugusa mpira na yeye akaunganisha moja kwa moja kama alivyofanya Botswana.

MAJINA KAMILI YA MCHEZAJI HUYU NI YAPI?
Nyota huyu anasema yeye anaitwa Khamis Mcha Khamis.
KWANINI ANAITWA VIALLI?
Mcha anasema utotoni alikuwa anacheza timu ya Kwahani ya Zanzibar. Kuna mchezaji mmoja wa timu ya wakubwa alikuwa anaitwa Shomary na ndiye alimpa jina la Vialli.
Mchana anasema wakati akiwa mtoto alikuwa anapenda kunyoa kipara. Sasa Shomary kila akimuona uwanjani, alikuwa anasema vipi bwana wewe! Unapenda kunyoa kipara kama Gianluca Vialli.
Gianluca Vialli ni mchezaji wa zamani wa Italia aliyekuwa anaichezea klabu ya Juventus.
Kutokana na kitendo cha Shomary kumuita Mcha Vialli, kilisababisha jina hilo liwe maarufu na kutumiwa na wengi. Na hapo ndipo Khamis Mcha `Vialli` likaanza kutumika zaidi.
Lakini unaweza kujiuliza, kwanini Mcha hanyoi kipara tena? Mfungaji huyu wa mabao mawili ya Stars anasema baba yake mzazi, Khamis Mcha alimkataza kunyoa kipara.
Mzee Mcha alimwambia mwanae kuwa kunyoa kipara ni `staili` ya vijana wahuni, kwahiyo akamtaka mtoto wake kuachana na unyoaji wa aina hiyo.
Mcha anasema siku zote yeye ni msikivu, alimsikiliza baba yake na kuamua kuacha kunyoa kipara kwasababu baba hataki na hapendi.

KWANI BABA YAKE, MZEE MCHA KHAMIS ALIKUWA MCHEZAJI?
Mcha anasema baba yake ni mtu wa mpira. Enzi zake alicheza timu ya Kmkm na baadaye Miembeni, zote za visiwani Zanzibar.

JE, KHAMIS MCHA ALIANZIA SOKA WAPI?

Mzanzibar huyu anasema alianzia soka katika timu ya Kwahani, akajiunga na Mbuyuni, baadaye Tembo, (zote za Zanzibar).
Baada ya kutoka Tembo alijiunga na Miembeni ambayo baadaye ilibadilishwa jina na kuitwa Zanzibar Ocean View.

Alipotoka katika timu hiyo akajiunga na Azam fc ambapo amecheza misimu mitatu na msimu ujao unakuwa wa nne.

Sunday, July 20, 2014

TAIFA STARS VS BLACK MAMBAS KATIKA PICHA ILIKUWA HIVI UWANJA WA TAIFA...

3m
Mbwana Samatta akiwatoka mabeki wa timu ya taifa ya Msumbiji. 
 Mshambuliaji nyota wa Taifa Stars, Mbwana Samatta akiwa katikati ya mabeki wa timu ya taifa ya Msumbiji. 
Mshambuliaji wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Thomas Ulimwengu akimtoka beki wa Msumbiji, Zainadine Junior katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, wa kuwania tiketi ya Fainali za Afrika zitakazofanyika nchini Morocco mwakani. Timu hizo zilitoka sare ya 2-2. 
 Thomas Ulimwengu  akichuana na beki wa Msumbiji, Josemar Machaisse.
 Huniwezi…Mshambuliaji wa Taifa Stars, Thomas Ulimwengu akimtoka beki wa Msumbiji, Zainadine Junior.
 Mshambuliaji wa Stars, Khamis Mcha akiwa katika harakati za kufunga goli.
 Golikipa wa Stars, Deogratius Munishi akishangilia balo la pili la 
Taifa Stars kwa kuonyesha fulana yake iliyokuwa ikisomeka ‘Sisi ni Watoto wa Rais Kikwete’.

waliotembelea blog