Monday, July 21, 2014


s9
Na Shaffih Dauda
KOCHA wa Timu ya taifa ya Tanzania, Mholanzi, Mart Nooij aliamua kuwaanzisha washambuliaji wanne katika mechi dhidi ya Msumbuji, kuwania kupangwa hatua ya makundi ya kusaka tiketi ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika, AFCON, mwakani nchini Morroco.
Mbwana Ally Samatta, Thomas Ulimwengu, John Bocco `Adebayor` na Mrisho Ngassa, wote kwa pamoja walianza katika sare ya 2-2 ndani ya uwanja wa Taifa, jinini Dar es salaam dhidi ya `Black Mambas`.
Lengo la Nooij lilikuwa ni kushambulia kwa nguvu ili kupata mtaji mkubwa wa mabao kabla ya mechi ya marudiano itakayopigwa wiki mbili zijazo mjini Maputo nchini Msumbiji.
Lakini kwa mtazamo wangu, niliona mapungufu juu ya namna kocha Nooij alivyowapanga washambuliaji hawa. Ulimwengu na Ngassa walicheza pembeni, Samatta na Bocco walisimama katikati.
Mimi naona ingekuwa na tija kama Thomas angecheza katikati kuliko kucheza pembeni ili kupata ubora wa timu.
Kwa timu ilivyoanza yeye alikuwa kulia, katikati alikuwa Mbwana Samatta na John Bocco, kushoto alicheza Mrisho Ngassa na wakawa wanabadilishana.
Lakini mimi naona ingekuwa na tija zaidi kama Thomas Ulimwengu angesimama katikati na John Bocco, halafu samata akawa anashambulia kutoka pembeni upande wa kushoto, halafu Mrisho Ngassa ashambulie kutoka kulia. Kwasababu kwa aina ya uchezaji wa Ulimwengu, walipokuwa wanamuweka pembeni walikuwa wanampatia ugumu.
Alikuwa analazimika apige chenga, apige pasi kutoka eneo alipo, lakini yeye sio aina ya mchezaji wa hivyo vitu, yeye sio mtu wa vitu, yeye ni mtu wa kuwekewa mpira ili awe na chaguo moja tu,  kupiga au kupasia karibia na goli ili kumpa mwenzie afunge, na hapo unaweza kuona ubora wa Thomas Ulimwengu.
Kama Ulimwengu angekuwa katikati ingekuwa ni vizuri zaidi kucheza mipira mirefu waliyokuwa wanacheza akina `Cannavaro` dakika za kipindi cha kwanza. Mara nyingi mipira hii mabeki wa Msumbiji walikuwa wanaicheza, kwasababu John Bocco pamoja  na umbile kubwa, mrefu, lakini sio mzuri kupambana, ni mwepesi, kwahiyo ni mara mia nane angekuwepo Thomas Ulimwengu, kwasababu ni mtu mwenye nguvu na jinsi mwili wake ulivyo angeweza kupambana nao na kutoa mianya kwa akina Ngassa, Samatta au Bocco mwenyewe kufungwa.
Hii ni kwasababu mabeki wa  Msumbiji wangelazimika kuokoa mipira hovyo, na ingedondoka maeneo ambayo wengine wangeokota baada ya mikikimikiki ya Ulimwengu.
Pix-3
Halafu kingine, ile mipira, Ulimwengu angekimbia nayo katoka katikati na kutanua kwenda pembeni. Hii ingetoa nafasi kwa akina Ngassa au Samatta kutegemeana mpira unaenda upande upi.
Mabeki wangelazamika kwenda kukimbiza na kuacha nafasi katikati, na kwasababu yeye ana kasi angewahi ile mipira na kupiga krosi ambazo zingeweza kufungwa na wenzake  kwasababu katikati pale pangeachwa wazi kutokana na mebeki kwenda pembeni kumkimbiza Ulimwengu.
Lakini ilikuwa ni ngumu kwa Ulimwengu kutokea pembeni na kupiga mipira vizuri kwasababu yeye hana uwezo wa kumiliki mpira vizuri, sio mtu wa kuchezea mpira kama akina Ngassa au Samatta mwenyewe.
Unajua Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta, John Bocco wote ni washambuliaji wa kati, lakini wanatofautiana  ujuzi na aina ya uchezaji.
Kama mimi ningekuwa kocha na ningetaka kuwatumia wote kwa wakati mmoja, mara mia nane, huyu Thomas Ulimwengu angesimama katikati, halafu Jonh Bocco au Samatta angeenda pembeni.
Lakini mimi ningependa zaidi Mbwana Samatta atokee pembeni upande wa kushoto, kwasababu ana uwezo, ana kasi, na anaweza kupiga chenga na kutafuta `engo` ya kupiga mpira. Anaweza kupiga chenga, akarudi na kuuzungusha.
Kuthibitisha pointi yangu hiyo, kuna wakati Samatta alikwenda pembeni, alipiga pasi mbili ambazo almanusura zisababishe goli. Alipiga krosi moja ambayo alipigwa kichwa na John Bocco, lakini kipa akacheza.

Akapiga krosi nyingine ambayo beki alitoa ikawa kona. Kwahiyo,  kwayeye kucheza pembeni ilikuwa na faida zaidi kuliko Thomas Ulimwengu.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog