Tuesday, April 7, 2015
1:13 AM
Unknown
Maandamano ya Wanamichezo wa timu mbili za Wakaguzin na Wadhibiti wa hesabu za Serekali wa Zanzibar na Tanzania wakipita kwa maandamano wakati wa ufunguzi wa michezo yao iliofanyika uwanja wa amaan Zanzibar timu ya CAG Tanzania imeshinda mchezo wa mpira kwa mabao 7--0.

Maandamano ya Wanamichezo wa timu mbili za Wakaguzin na Wadhibiti wa hesabu za Serekali wa Zanzibar na Tanzania wakipita kwa maandamano wakati wa ufunguzi wa michezo yao iliofanyika uwanja waAamaan Zanzibar timu ya CAG Tanzania imeshinda mchezo wa mpira kwa mabao 7--0.
Wafanyakazi wa Afisi ya CAG Zanzibar wakifuatilia michezo hiyo wakiwa jukwaani amaan
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serekali Tanzania Profesa Mussa Juma Asad akiwa na Maofisa wa CAG wakati akiendea kuzindua rasmin michezo hiyo iliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar
Maofisa wa CAG Zanzibar na Tanzania wakiwaenda uwanjani kwa ajili ya uzinduzi wa michezo hiyo
1:11 AM
Unknown
Na Faustine Ruta, Geita
Kikundi mahiri cha KAPOTIVE Star Singers kutoka Mjini Bukoba leo kimefanya Tamasha kubwa la Pasaka kwenye Mji wa Geita katika Ukumbi wa GEDECO na kushuhudiwa na Umati wa Watu wengi zikiwemo Kwaya mbalimbali za hapa Geita na Waumini mbalimbali na kuifurahia Pasaka hiyo ambayo ni Alama ya Ukombozi wa Mwanadamu dhidi ya Dhambi kupitia kifo na Ufufuko wa Yesu Kristo. Wana'KAPOTIVE walisindikizwa na kwaya ya Mt. Thomas wa Aquino na Aaron Entertainment wa hapo Geita. Watu walivutiwa sana na kiwango cha juu ya kikundi cha KAPOTIVE mpaka wengine wakadiriki kusema sio kutoka Bukoba.Kwaya Mt. Thomas wa Aquino ikitoa burudani kwenye Tamasha la Pasaka- Geita.
Baadhi ya masista waliohudhuria tamasha hilo.
Kiongozi wa Kikundi cha Kapotive Star Singers Bukoba Ndg Andrew Kagya wakati wa Kutambulisha Kikundi hicho cha Kapotive kwa Wakaazi waliojitokeza katika Ukumbi wa GEDECO wakati wa Tamasha hilo la Pasaka leo Jumapili.
Watu hawakuweza kujizuia na kuanza kujimwaga kwa muziki wa Yesu, palikuwa hapatoshi!!!!Vijana machachari wa Kapotive Star Singers, Denis Deus na Claudius Mutabuzi wakilikamatilia jukwaa kwa mbwembwe zote ilimradi kuwakamata watazamaji waliofurika ukumbi wa GEDECO.
Hii ni hatari "ebye'hatari"!!!
Lazima nichukue kumbukumbu hizi, hawa vijana si wa kawaida, ndivyo anavyoonekana kusema mama huyo.
Kazi ndo imekamata kisawasawa.
Kinyumbani zaidi, empundu nengoma tuteere!!!
Kwaya ya Mt. Aquino walitoa zawadi ya kipekee kwa Kapotive Star Singers, hapa mwenyekiti wao akiwa na baadhi ya wana'KAPOTIVE.
Mambo si ndo hayo!!!!
Mayahudi wakiwa kazini!!!!
Yesu akiwa tayari ametundikwa Msalabani katika Igizo hilo kwenye Ukumbi wa GEDECO mjini Geita leo wakati wa Tamasha la Sikukuu ya Pasaka leo Jumapili

1:08 AM
Unknown
Na Faustine Ruta, Bukoba
Kundi zima la Yamoto Band punde walitinga Katika Kituo cha Radio Kasibante 88.5 Bukoba kuongea moja kwa moja na Wakaazi wa Bukoba juu ya Shoo ya yao inayotarajiwa kufanyika Usiku huu katika Ukumbi wa Burudani wa Lina's Night Bukoba. Bendi inayokuja kasi hapa Nchini inayoundwa na Vijana Machachari kama Aslay, Becka, Bella na Maromboso wameteta na Wanabukoba kwamba waje kwa wingi katika Ukumbi huo wa Lina's wajionee walichokuja nacho kipya katika Pasaka hii ya pili maana kwa sasa watawasha Moto wa Uhakika na Watatoa Burudani Live jukwaani na wamekuja wamejipanga wakiwa na Vijana wengine ambao ni Maalum kwa Kuliteka Jukwaa kwa mapigo ya Live"
Mtandao huu wa jamii murua kwa habari tamu za Michezo na Burudani pia umeweza kuzinyaka za haraka haraka kwamba baada ya Shoo ya leo katika Ukumbi wa Lina's Kesho Jumatatu watatoa Burudani pia huko Biharamulo kwa kiingilio cha 10,000/ siku ambayo ni Karume Day" ya jumanne tarehe 07/04/2015. Kiingilio cha Shoo ya leo ya Lina's kwa kawaida ni Tsh 10,000/ na VIP ni Tsh.15,000/-
Wasanii wa Kikundi cha Yamoto Band wakiwa Katika Studio za Radio Kasibante 88.5 FM kuteta na Mashabiki wao na kuwajuza Kile walichokuja nacho kwa mara nyingine na kwa mwaka huu mpya wa 2015.
Wasanii wa Yamoto Band wakiwa wanaimba moja ya Wimbo wao mpya wa "Nitakupwelepweta" katika Studio za Kasibante 88.5 FM
Jonathan Mwanga maarufu kwa Jina la Jerry ambae ndie muhusika Mkuu wa Show itakayofanyika baadae usiku huu aliyewaleta kwa mara ya pili Yamoto Band hapa Bukoba nae alikuwa Sambamba na Wasanii hao wanaokuja kwa kasi hapa Nchini.
Usiku huu Moto wa Yamoto band Kuwaka!!
Pamoja sana..!
Mtangazaji wa Radio Kasibante FM 88.5 Jerome akiwa live kwenye kipindi na Vijana wa Yamoto Band
Slay akiongea moja kwa moja na Mashabiki wake kupitia Radio Kasibante 88.5 FM Bukoba leo hii jioni

Subscribe to:
Posts (Atom)