Tuesday, April 7, 2015

Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama na mkewe wakimkaribisha jukwaani Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe pichani kulia ni Askofu David Mwasota wa Kanisa la Naioth Gospel Assembly

Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama akizungumza jambo na Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe,kati ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Fenella Mukangara (kulia), Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angella Kairuki.

Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akiwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Fenella Mukangara (kulia), Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angella Kairuki na Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama na Mkewe.

Askofu David Mwasota wa Kanisa la Naioth Gospel Assembly akisoma hotuba amempongeza Mhe. Bernard Membe kwa kujumuika na Watanzania katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka ililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe ambaye alikuwa mgeni rasmi akiongea katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka ililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015. Pembeni ni Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe ametoa rai kwa viongozi wa dini zote pamoja serikali kuhimiza vijana waipende dini ili kudumisha amani, utulivu na uadilifu.Mhe Membe amesema hayo wakati akihubutibi maelefu wa watu waliohudhuria Tamasha la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
Askofu David Mwasota wa Kanisa la Naioth Gospel Assembly akisoma hotuba amempongeza Mhe Bernard Membe kwa kujumuika na Watanzania katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka.Katika Tamasha hilo la Pasaka, Kampuni ya Msama Promotions, ambao ndio waandaji wa Tamasha hilo, wamemtunuku Mhe. Rais Jakaya Kikwete kwa mchango wake katika kukuza tasnia ya Sanaa nchini.

Tuzo ya heshima ilitolewa kwa Rais Mstaafu, Mhe. Ali Hassan Mwinyi.

Mhe Bernard Membe alitunukiwa tuzo kwa mchango wake kwa shughuli za kijamii.Tuzo zimetolewa kwa vyombo mbalimbali vya habari nchini kwa michango yao katika kutangaza Tamasha la Pasaka.
Viongozi wa Serikali waliohudhuria Tamasha hilo ni pamoja na Mhe. Fenella Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Angela Kairuki, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, na Mhe. Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.Tamasha hilo lilihudhuriwa na viongozi wa kidini wakiwemo, Askofu David Mwasota wa Kanisa la Naioth Gospel Assembly na Mchungaji Mwasota.

Tamasha la Pasaka lilianzishwa rasmi mwaka 2000 na huwashirikisha Waimbaji wa Nyimbo za Injili kutoka nchini na nje ya nchi ambapo mwaka huu limewashirikisha waimbaji kutoka hapa nchini, Afrika Kusini, Uingereza na Zambia.


Mgeni rsami Mh.Membe akimkabidhi tuzo ya heshima Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Fenella Mukangara kwa niaba ya Rais Mstaafu, Mhe. Ali Hassan Mwinyi.

Mhe Bernard Membe alitunukiwa tuzo kwa mchango wake kwa shughuli za kijamii.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akinyanyua juu tuzo aliyotunukiwa kwa mchango wake mkubwa kwa shughuli mbalimbali za kijamii.

Keki ikikatwa kwa pamoja kama sehemu ya ishara ya amani na upendo.

Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akishirikiana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Fenella Mukangara (kulia) na Mchungaji Mwasota kukata keki. Aanayeshudia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angella Kairuki.

Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akimlisha keki Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Fenella Mukangara


Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akimlisha keki Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama na mkewe.


Sehemu ya umati wa Watu waliohudhuria Tamasha la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.

Sehemu ya umati wa watu



Kwaya ya Kijitonyama wakiimba katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.

Sehemu ya umati wa watu

Waimbaji wa Kwaya ya Kijitonyama jukwaani

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog