Anatimka zake: Kiungo wa Chelsea, John Obi Mikel anahusishwa kuhamia klabu za Italia.
Imechapishwa Julai 16, 2014, saa 12:08 asubuhi
KLABU ya Chelsea wanatarajia kumuuza kiungo wao raia wa Nigeria, John Obi Mikel, huku kukiwa na taarifa kuwa klabu za Italia zimekubali kutoa ofa ya paundi milioni 5.
Mikel alianza katika mechi 11 tu za ligi kuu msimu uliopita na alipata upinzani mkubwa kutoka kwa Nemanja Matic, Willian na Ramires.
Kitendo cha kiungo Cesc Fabregas
kujiunga na klabu hiyo kutokea katika klabu ya Barcelona kwa dau la
paundi milioni 30 kunazidi kufinya nafasi ya Mikel msimu ujao.
Mikel, aliyecheza katika mechi zote za
Nigeria katika fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 nchini Brazil na
kufika hatua ya pili na kupigwa na Ufaransa, amesema kuondoka kwake si
kwasababu ya kuwasili kwa Fabregas.
Alisema: "Sina tatizo na kusajiliwa kwa Fabregas," alisema. "Tulikutana mara kwa mara. Hata hivyo hatuchezi nafasi moja".
Wakatai huo huo, beki wa Chelsea,
Patrick van Aanholt amethibitisha kuondoka klabuni hapo na anaweza
kurithi nafasi ya mchezaji aliyesajiliwa na Newcastle Daryl Janmaat katika klabu ya Feyenoord.
Mholanzi huyo mwenye miaka 23 alijiunga na akademi ya Chelsea mwaka 2009 akitokea PSV Eindhoven, lakini amecheza mechi mbili tu na alitumia msimu uliopita kucheza kwa mkopo katika klabu ya Vitesse.
Van Aanholt ameichezea Uholanzi katika mechi mbili na ameiwakilisha nchi hiyo katika ngazi zote kuanzia miaka 16.
+
Anasepa zake: Patrick van Aanholt anahusishwa kujiungga na Feyenoord ya nchini Uholanzi.