Wednesday, July 16, 2014


On the move: Chelsea midfielder John Obi Mikel has been linked with a transfer to an Italian club
Anatimka zake: Kiungo wa Chelsea, John Obi Mikel anahusishwa kuhamia klabu za Italia.

Imechapishwa Julai 16, 2014, saa 12:08 asubuhi

KLABU ya Chelsea wanatarajia kumuuza kiungo wao raia wa Nigeria, John Obi Mikel, huku kukiwa na taarifa kuwa klabu za Italia zimekubali kutoa ofa ya paundi milioni 5.
Mikel alianza katika mechi 11 tu za ligi kuu msimu uliopita   na alipata upinzani mkubwa kutoka kwa Nemanja Matic, Willian na Ramires.
Kitendo cha kiungo Cesc Fabregas kujiunga na klabu hiyo kutokea katika klabu ya Barcelona kwa dau la paundi milioni 30 kunazidi kufinya nafasi ya Mikel msimu ujao.
New boy: Cesc Fabregas has joined Chelsea from Barcelona in a £30million move this summer
Kijana mpya: Cesc Fabregas amejiunga na Chelsea majira haya ya kiangazi kutokea klabu ya Barcelona.

Mikel, aliyecheza katika mechi zote za Nigeria katika fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 nchini Brazil na kufika hatua ya pili na kupigwa na Ufaransa, amesema kuondoka kwake si kwasababu ya kuwasili kwa Fabregas.
Alisema: "Sina tatizo na kusajiliwa kwa Fabregas," alisema. "Tulikutana mara kwa mara. Hata hivyo hatuchezi nafasi moja".
Wakatai huo huo, beki wa Chelsea, Patrick van Aanholt amethibitisha kuondoka klabuni hapo na anaweza kurithi nafasi ya mchezaji aliyesajiliwa na Newcastle Daryl Janmaat katika klabu ya Feyenoord.
Mholanzi huyo mwenye miaka 23 alijiunga na akademi ya Chelsea mwaka 2009 akitokea PSV Eindhoven, lakini amecheza mechi mbili tu na alitumia msimu uliopita kucheza kwa mkopo katika klabu ya Vitesse.
Van Aanholt ameichezea Uholanzi katika mechi mbili na ameiwakilisha nchi hiyo katika ngazi zote kuanzia miaka 16.
On his way: Patrick van Aanholt has been linked with a move to Feyenoord in Holland +
Anasepa zake: Patrick van Aanholt  anahusishwa kujiungga na  Feyenoord ya nchini Uholanzi.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog