Thursday, September 3, 2015


D3A_1635
Huyu ni mwimbaji Mrembo kutoka Mauritius aliyefanya watu waenjoy zaidi kwa kutoa burudani kwenye stage
Ni utaratibu ulioanza mwaka 2014 kwa kampuni ya Multichoice kukutana na Waandishi wa habari/Watangazaji kutoka nchi mbalimbali za Afrika kuonyesha na kuyazungumzia kwa upana vipindi na mengine mengi yanayopatikana kupitia bidhaa yake ya DStv.
Tamasha hili linafanyika kwa wiki nzima kwenye kisiwa cha Mauritius kuanzia September 1 -6 likiitwa MultiChoice Africa Content Showcase Extravaganza ambalo mwaka huu limehudhuriwa na Waandishi mbalimbali wakiwemo wa Tanzania pamoja na mastaa kutoka nchi mbalimbali wakiwemo Genevieve Nnaji, Ramsey Noah na Mr. Flavour wa Nigeria.
D3A_1656
MC alikua IK na Eku
D3A_1726
Moja ya vitu alivyozungumza C.E.O wa MultiChoice Tim Jackobs ni kwamba kampuni hiyo itaendelea kutoa huduma kwa ubora na kuendeleza malengo yake makubwa ya kuhakikisha kila mteja anapata zaidi ya matarajio yake kwenye TV.
D3A_2127
D3A_2150
D3A_2390
Ramsey na Genevieve kwenye meza moja wakienjoy show
D3A_2401
D3A_2418
Mwigizaji Desmond Elliot
D3A_2431
Ramsey
D3A_2447


Dereva mahiri wa mbio za magari ya Formula 1 Lewis Hamilton amekuwa akihusishwa kutoka kimapenzi na Rihanna kwa zaidi ya mwezi sasa, toka zile picha za wao kuonekana pamoja katika tamasha linalofanyika kila mwaka Barbados ziingie katika headlines, wengi wamekuwa wakiamini kuwa kuna kitu kinaendelea.
Hamilton na Rihanna wamekuwa karibu kwa muda sasa, kiasi kwamba watu wanaofuatilia nyendo za mastaa hao, wanahisi huenda wakawa wanatoka kimapenzi, kwani hakuna mmoja kati yao aliyekuwa ameweka wazi kama wako katika mahusiano ya kimapenzi au urafiki wa kawaida.
Rihanna-and-lewis-Hamilton
Hii ni moja kati ya picha zilizozua utata wa ukaribu wao katika tamasha Barbados
“Unajua nimefahamiana na Rihanna kwa kipindi kirefu kidogo, tumekuwa marafiki kwa muda mrefu wakati mwingine tumekuwa tukiongozana mara kwa mara”>>> Lewis Hamilton
Licha ya Lewis Hamilton ambaye amewahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi ya on-off na muimbaji Nicole Scherzinger kwa takribani miaka saba, anakanusha kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Rihanna



Drogba ni mmoja wa mastaa wakubwa Afrika na hata soka la Ulaya, Novemba mwaka huu anatarajia kuzindua kitabu kitakachozungumzia maisha yake kwa ujumla.
DDD
Akiwa na miaka yake 37 mshambuliaji huyo ameahidi kutoa kitabu hicho ambacho kitazungumzia pia na maisha yake akiwa Ufaransa, umuhimu wa elimu, jinsi ya kutafuta mafanikio katika maisha.
Pia kitazungumzia maisha yake ya kawaida na ya nje ya uwanja hasa akiwa na klabu yake ya


Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, ambayo ni mdhamini mkuu wa Ligi Kuu ya mpira wa miguu Tanzania bara leo imekabbidhi vifaa kwa timu zinazoshiriki ligi hiyo yenye thamani ya shilingi milioni 490,00,000.
Akikabidhi vifaa hivyo leo jijini Dar es salaam, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twisa alsiema kuwa kwa mara nyingine tena katika kuhakikisha ligi ya soka nchini inaenda vizuri Vodacom inakidhi vifaa mbalimbali vy a ligi ambavyo ni jezi za kawaida, jezi za mechi, viatu na vifaa vingine vinayohitajika.

Vijana wakitambulisha jezi mpya za nyumbani na ugenini za timu ya African Sport ya Tanga na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni 4.9 kwa msimu wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/2016 zilizokabidhiwa rasmi leo na mdhamini mkuu wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania.

Wanamitindo wakipita kuitambulisha jezi mpya za nyumbani na ugenini za timu ya Majimaji na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni 4.9 kwa msimu wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/2016 zilizokabidhiwa rasmi leo na mdhamini mkuu wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania, Boniface Wambura(kushoto) na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa(watano toka kushoto)akiwa kwenye picha na mwakilishi wa timu ya Azam FC pamoja na wanamitindo waliokuwa wakiitambulisha jezi mpya za nyumbani na ugenini na vifaa mbalimbali vya timu ya Azam FC vyenye thamani ya shilingi Milioni 4.9 kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/2016.Vifaa hivyo vilikabidhiwa leo jijini Dar es Salaam na mdhamini mkuu wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania, Boniface Wambura(kushoto) na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa(watano toka kushoto)akiwa kwenye picha na mwakilishi wa timu ya Coastal Union pamoja na wanamitindo waliokuwa wakiitambulisha jezi mpya za nyumbani na ugenini na vifaa mbalimbali vya timu hiyo vyenye thamani ya shilingi Milioni 4.9 kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/2016.Vifaa hivyo vilikabidhiwa leo jijini Dar es Salaam na mdhamini mkuu wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania,Boniface Wambura(kushoto) na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa(watano toka kushoto)akiwa kwenye picha na mwakilishi wa timu ya Mbeya FC pamoja na wanamitindo waliokuwa wakiitambulisha jezi mpya za nyumbani na ugenini na vifaa mbalimbali vya timu hiyo vyenye thamani ya shilingi Milioni 4.9 kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/2016.Vifaa hivyo vilikabidhiwa leo jijini Dar es Salaam na mdhamini mkuu wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania,Boniface Wambura(kushoto) na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa(watano toka kushoto)akiwa kwenye picha na mwakilishi wa timu ya Yanga sports club ya jangwani jijini Dar es salaam pamoja na wanamitindo waliokuwa wakiitambulisha jezi mpya za nyumbani na ugenini na vifaa mbalimbali vya timu hiyo vyenye thamani ya shilingi Milioni 4.9 kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/2016.Vifaa hivyo vilikabidhiwa leo jijini Dar es Salaam na mdhamini mkuu wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania,Boniface Wambura na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanamitindo waliokuwa wakizitangaza jezi mpya za timu 16 zitakazoshiriki katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/2016 wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa jezi hizo na vifaa mbalimbali vyenye thamni ya zaidi ya shilingi milioni 4.9 na mdhamini mkuu wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania kwa timu zote zitakazoshiriki katika ligi hiyo.
“Tunajisikia furaha kukabidhi vifaa hivi siku ya leo tukiwaa tunatekeleza matakwa ya mkataba wa udhamini, ni imani yetu kwamba timu zitakazoshiriki lii zimejiandaa vya kutosha kwa msimu mpya 2015/2016” Alisema Twissa.

Twissa alisema Vodacom inaendelea kudhamini ligi kuu kwa sababu soka ni mchezo unaopendwa sana hapa nyumbani ukiwa na washabiki wengi hivyo inapenda kuona wananchi ambao baadhi yao ni wateja wake wanapata buruddaniya mchezo waupendao pia siku zote inaamini kuwa michezo ni ajira kubwa duniani kote, ikiendelezwa inaweza kubadilisha maisha ya watu wengi na taifa kunufaika kwa mapato makubwa ya kodi kutoka sekta hii.

Aliwataka wadhamini wengine kujitokeza ili kuboresha zaidi ligi ya Tanzania na kuongeza maslahi kwa wachezaji wanaoshiri katika ligi “Tukiunganisha nguvu timu zetu zinaweza kuwa na wachezaji wa kimataifa pia ni muhimu kwa wadau mbalimbali kuanza kuwekeza katika timu za vijana chipukizi kwa kuwa vipaji vinaanza ngazi ya chini ambako vinapaswa kuibuliwa na kuendelezwa” Alisema Twissa.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura aliishukuru Kampuni ya Vodacom na kuvitaka vilabu vinavyoshiriki ligi kuu ya Vodacom kuheshimu chapa ya mdhamini wakati wote wa ligi.

“Ninatoa mwito kwa vilabu vyote kutumia jezi zenye nembo ya mdhamini katika kuhakikisha ligi inafanikiwa kama inavyotakiwa” alisema.

Aliongeza kuwa TFF isingependa kutumia kanuni na sharia kuadhibu klabu inayokwenda kinyume, bali kila klabu izingatie masharti ya madhamini kama ambavyo anavyotimiza haki yake ya kuwapatia vifaa.

Alisema ligi ya mwaka huu itakuwa bora kutokana na maandalizi yote kukamilika mapema pia timu zitakazoshiriki zimejiandaa vya kutosha kuhakikisha ligi inakuwa na msisimko na ushindani mkubwa.

NIGERIA KUWASILI KESHO USIKU
Timu ya Taifa ya Nigeria (Super Eagles) inatarajiwa kuwasili kesho alhamis saa nne usiku kwenye uwanja wa JK Nyerere jijini Dar es salaam kwa usafiri wa ndege binafsi tayari kwa mchezo dhidi ya Tanzania siku ya jumamosi uwanja wa Taifa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Nigeria (NFF), kupitia kwa Toyin Ibitoye msafara huo unatarajiwa kuwa na wachezaji 23 pamoja na viongozi wa benchi la ufundi linaloongozwa na kocha mkuu Sunday Oliseh pamoja na viongozi wengine waandamizi wa shirikisho hilo.

Nigeria inatarajiwa kufanya mazoezi siku ya ijumaa saa 10 jioni katika uwanja wa Taifa, ikiwa ni mazoezi mepesi ya kuelekea kwenye mchezo huo.

KOZI YA LESENI B ZANZIBAR YAFUTWA

Kozi ya makocha wa CAF ya Leseni B iliyokua ifanyike kwa muda wa wiki tatu mwezi Septemba mwaka huu kisiwani Zanzibar sasa imefutwa kufuatia kupeleka mpira mahakamani.
Sasa kozi hiyo itafanyika tena pindi kesi ya mpira itakapoondelewa mahakamani. Kumekua na hali ya kutokuelewana kwa uongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu kisiwani Zanzibar (ZFA) hali iliyopelekea uongozi wa ZFA kupelekwa mahakamani.

Kwa mujibu wa kanuni za FIFA, masuala ya mpira wa miguu hayapaswi kupelekwa mahakamani.

waliotembelea blog