Tuesday, July 23, 2013


 Dakari katika hospitali ya mnazi mmoja akitoa huduma ya kwanza kwa majeruhi wa ajali ya gari iliopinduka ikiwa katika msafara wa maziko ya Marehemu waliokufa Dafur, ajali hiyo imetokea baada ya kupinduka gari waliokuwa wamepanda wakienda makaburini kwerekwe. 
 Majeruhi wa ajili yagari ya jeshi wakiwa katika hospitali ya mnazi mmoja wakisubiri huduma ya kwanza baada ya kufikisha hospitali hapo. kwa matibabu. 

 Daktari katika hospitali ya mnazi mmoja akitowa huduma ya kwanza kwa majeruhi wa ajali waliofikishwa hospitalini hapo kwa matibabu. 




Makaktari katika ya Hospitali ya mnazi mmoja wakiandaa vifaa kwa ajili ya kutowa huduma ya kwanza katika hospitali kuu ya mnazo mmoja kwa matibabu, ajali hiyo imetokea maeneo ya mwankwerekwe sokoni. 


clip_image002

Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva ambaye anafanya Vizuri sana na Stayle yake ya Bongo Bolingo Hamisi Ramadhani Muite H-BABA. Ameamua kutoa kauli yake juu ya swala zima la Kufuturisha ambalo limechukua nafasi katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani,

H-Baba ameamua kutoa kauli hiyo baada ya kuona watu wanafanya mambo hayo kinyume na Taratibu za Misingi ya Dini, 
"Nawapongeza kwa wale wanaoenda kufuturisha watoto Yatima na waendao kufuturisha Misikitini nawapa pongezi sana kwasababu wanapata dhawabu kubwa sana kuliko wale wanaoalika watu wasioeleweka majumbani kwao alfu wanafuturisha alfu usifanye hivyo kutaka sifa unawaita wandishi wa habari nyumbani kwako ili watu wajue, inakuwa siyo swala la msingi.
clip_image001
Sisi watoto wa kiislamu sifa na Mwezi wa Ramadhani ni vitu viwili tofauti tusitake sifa kuonekana wasafi au kuonekana Bora katika kipindi hiki, inabidi sisi wote turudi nyuma na kuacha maovu yetu yote tulikua tukifanya, kama unafanya jambo lako nenda  msikitini utawakuta watu ambao wako pale kwa ajili ya swala toa msaada wako pale au futurisha pale, Utapata dhawabu kubwa sana.
Lakini uanapokuwa nyumbani kwako ukaalika wasanii wenzako watakuja lakini kumbuka wengine  hawajafunga,  mwingine katoka bar, Mwingine kasuka, Mwingine kavaa Heleni mwingine kavaa hiki na hiki haiswii kwa sisi watoto wa Kiislamu, Tusitake sifa sisi wasanii tumekuwa wataka sifa.
Leo umesikia Flani kafuturisha eti na wewe kesho yake unaamka na mimi nafuturisha jamani tusifanye kama kamchezo huu ni mwezi wa Ramadhani tuache sifa, Mimi mbona nimefuturisha nani anae jua? kufuturisha ni wewe na ndugu zako na marafikizako wa karibu, siyo leo nafuturisha Mwandishi Flan Njoo unipige picha njoo unimulike Watanzania waone, wewe ndugu yangu mambo hayaendi ivyoo bwana haiswii maana lazima tambiane ukweli unapofanya jambo baya mwezi huu wa ramadhani
clip_image001[4]
Kwanza wewe Mtoto wa kiume Haujaoa unalala na mwanamke haujamuoa je inaswii..? pia mtoto wa kike unalala na mwanamume hajakuoa je inaswii..?jamani tusichezee Dini hiki siyo kipindi cha kufanya mabo yetu kutafuta sifa,huu ni muda wa kutubu, muda wa kumrudia mola pia ni muda wa kujisafisha.
Me nimeoa mke wangu ananipikia ftari vizuri nafunga na mpaka kwa sasa kishavu kinatoka,Nafuturisha watu wanakuja kwangu wanafuturu lakini siyo kwa sifa sasa mnaita mpka TV, Magazeti na Redio aaah jamani nani wewe? sifa za nini kipindi hiki ? unatubu nini sasa? jamani wasanii wenzangu nawasii tuache sifa namaliza kwa kusema KWA ALLAH HAKUNA SIFA" alisema H-BABA
Unaweza kuona Video H-BABA akiwa anaongea... 

Mrembo na mwanamuziki wa kike nchini, Linah Sanga amezikanusha ripoti zilizosambazwa leo kuwa amebakwa na rapper Kimbunga na kudai kuwa ameshangazwa mno na taarifa hizo. 

Taarifa hizo zimeanza kusambazwa leo mchana baada ya akaunti ya Facebook inayoonekana kuwa ya rapper Kalapina yenye jina ‘KalApina Kikosi Cha Mizinga’ kuandika: 
 

bikira maria Picha juu ni ya Kanisa la Kikatoliki la Saint Benedict, lililopo Ubiaja, Esan Kusini Mashariki ya Jimbo la Edo nchini Nigeria.
Waumini wa Kanisa hilo wanasema kwamba waliiona kitu kinachofanana na Bikira Maria kwenye ukuta wa Kanisa hilo mnamo siku ya Jumapili July 21.
bikira maria.2Waumini hao walifanikiwa kuchukua picha....
Je unaiona? Je inahitaji maelezo ya ziada juu ya hili?
Angalia na picha hapo juu...?


l

WAKATI miili ya wanajeshi saba ikiwa imeagwa jana katika Viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania, imeelezwa kuwa kundi la Janjaweed linaloungwa mkono na serikali ya Sudan ndilo lililowavamia na kuwaua askari hao nchini humo  na kuwajeruhi wengine 17 .

Wanajeshi hao wa Tanzania ambao walikuwa ni sehemu ya Jeshi la Kulinda Amani la Umoja wa Mataifa (Unamid), walifanyiwa unyama huo Julai 13, mwaka huu katika eneo la kusini mwa Darfur, nchini Sudan.

Kiongozi wa moja ya makundi ya wapiganaji la Sudan Liberation Movement (SLM), Minni Mannawi ameibuka na kuwatuhumu wanamgambo wa Janjaweed wanaoungwa mkono na serikali ya nchi hiyo na ametaka ufanyike uchunguzi wa kimataifa.

Katika mahojiano yake na Gazeti la Sudan Tribune alipokuwa anahudhuria mkutano wa majadiliano kuhusu namna ya kupata amani ya kudumu nchini Sudan uliofanyika jijini Geneva Uswisi wiki iliyopita, alikanusha kuwa kundi lake linahusika na shambulio hilo.
 


“Tuna uhakika shambulio lililofanywa dhidi ya walinzi wa amani wa Unamid liliandaliwa na kutekelezwa na Janjaweed, tuko tayari kutoa ushirikiano kwa chombo maalum cha kimataifa kitakachoundwa kufanya uchunguzi kuhusu tukio hili…Nashauri serikali (ya Sudan) isishiriki katika uchunguzi kwa sababu itaficha ukweli,” alisema Mannawi.

Aliongeza kuwa wanamgambo hao waliowashambulia wanajeshi wa kulinda amani hivi sasa wanakabiliwa na ukata wa hali ya juu na kukosa vifaa kwa sababu serikali haina tena uwezo wa kuwahifadhi, hivyo wameamua kufanya matukio ya uporaji kukidhi mahitaji yao.
 

Msemaji wa Katibu Mkuu wa UN, Martin Nesirky alisema wameanza kufanya uchunguzi wao binafsi. Taarifa ya UN ilieleza juzi kuwa mashuhuda wamekuwa wakieleza mauaji hayo yamefanywa na kundi linaloungwa mkono na serikali ya Sudan.

Wakati huo huo, majeshi ya Nigeria yamejitoa kulinda amani Darfur. Hazikutolewa sababu za kufanya hivyo japokuwa UN imethibitisha.


Mnamo tarehe 21/07/2012 majira ya saa 23:30hrs huko kijiji cha Nkwangu wilaya ya Chunya mkoa wa Mbeya, Seni s/o Sandu, miaka 20, Msukuma, mkulima na mkazi wa Nkwangu aliuawa kwa kupigwa fimbo kichwani na Tolo s/o Seko, miaka 20, Msukuma, mkulima na mkazi wa Nkwangu.
Chanzo ni ugomvi wa kumgombania msichana aitwaye Holo d/o Kulwa, miaka 16, Msukuma mkulima na mkazi wa Nkwangu.


Mtuhumiwa amekamatwa na taratibu za kumfikisha mahakamani zinaandaliwa.


Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishna msaidizi wa polisi diwani athumani anatoa wito kwa jamii kutojichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha sheria na kudhibiti hasira zao kwa kuyatatua matatizo ya kimapenzi kwa njia ya mazungumzo ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.
ASKARI mmoja wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Mkoani Kilimanjaro, Fidelis Mwaliyatabu, amefariki dunia papo hapo na wengine tisa akiwamo Mkuu wa Kikosi hicho kujeruhiwa vibaya baada ya gari lao kupinduka katika kijiji cha Kilingi, wilaya ya Siha, wakati wakienda kuzima vurugu za wananchi.
Ajali hiyo ilitokea wakati kikosi hicho kikielekea katika kijiji cha Karansi kwa ajili ya kukabiliana na wananchi waliokuwa wakiandamana kupinga wenzao waliokamatwa usiku wa manane baada ya kuvamia mashamba mali ya Shirika la Roho Mtakatifu-Kilasara.
Taarifa kutoka kijijini humo zilieleza kwamba wanakijiji waliamua kuandamana baada ya wenzao watano kukamatwa na Jeshi la Polisi nyakati za usiku kwa mahojiano kutokana na kukabiliwa na tuhuma za kushawishi wanakijiji wenzao kuvamia maeneo ya Shule ya Kilasara na kusababisha hasara kubwa kwa shule hiyo.
Kufuatia kukamatwa kwa watuhumiwa hao, wanakijiji waliamua kuaandamana hadi katika kituo cha polisi ili kuwatoa wenzao hali ilisababisha jeshi hilo kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya, jambo ambalo lilishindikana kutokana na wingi wa watu walikuwa wanaandamana.
Inadaiwa kuwa wananchi hao walijikusanya na walianza kuandamana kuanzia majira ya saa 7 usiku kuelekea kituo cha polisi ili kuwatoa wenzao walikuwa wanashikiliwa.
Wananchi wanaoshikiliwa na jeshi hilo ni John Sokoine, Abeli Solomoni, Christopher Solomon na aliyetambuliwa kwa jina moja tu la Julius. Wote walikamatwa usiku wa kuamkia jana.
Mnamo Juni 11, mwaka huu majira ya mchana wananchi wa kijiji hicho walivamia eneo lenye ukubwa wa hekta mbili na kufyeka mazao mbalimbali yaliyokuwa shambani hapo kwa madai kuwa wamiliki wa shule hiyo wamechukua eneo hilo kinyume cha taratibu.
Kwa upande wake, Mkuu wa Shirika la Roho Mtakatifu, Kanda ya Afrika, Padri Jerome Okama, aliushutumu uongozi wa kijiji hicho kwa kuvifumbia macho vitendo vya wananchi kujichukulia sheria mkononi wakati wakitambua kuwa eneo hilo lenye ukubwa wa hekta 8.9 linamilikiwa na shirika hilo kihalali.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Robert Boaz, akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu kutoka wilayani humo jana jioni, alisema askari hao walipata ajali hiyo majira ya saa 6.45 mchana katika kijiji cha Kilingi nje kidogo ya mji wa Sanya Juu.
Alisema askari hao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC na wengine wamelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Ugonjwa wa Kifua Kikuu ya Kibong'oto ilioyopo wilayani Siha na kwamba watano kati yao hali zao ni mbaya.
Alitaja gari la Polisi lililopinduka na kuua kuwa ni Toyota Land Cruiser lenye namba PT 2070 lililokuwa likiendeshwa na Sajenti Herman Dancan. Chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na kuacha njia na kupinduka.
Aliwataja waliojeruhiwa katika ajali hiyo kuwa ni Mkuu wa FFU mkoani hapa, ASP Nonino, Renatus Misigalo, Alfonce Joseph, Koplo Elifuraha Lenare, Peter Albert, Bashiri Yusuph, George Mwakyusa na Gaspar Mwapunda.
Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Kibong'oto.

waliotembelea blog