Tuesday, July 15, 2014



Mshambuliaji mpya Yanga, Geilson Santana Santos ‘Jaja’ awasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo tayari kuitumikia klabu yake akitokea nchini kwao Brazi


Mshambuliaji mpya Yanga, Geilson Santana Santos ‘Jaja’ awasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo tayari kuitumikia klabu yake akitokea nchini kwao Brazi


BAADA kukirejesha Kikosi cha Netherlands kwao baada Fainali za Kombe la Dunia toka huko Brazil, Kocha mpya Louis van Gaal Leo hii anatarajiwa kutua Klabu yake Mpya Manchester United Jijini Manchester huku ikiwepo shauku kubwa ya kuleta Wachezaji wapya.
Anga za Uhamisho huko Ulaya sasa zimejaa mategemeo makubwa kuwa kuanza kazi rasmi kwa Van Gaal huko Old Trafford kutashuhudia Mabingwa hao wa zamani wakiongeza Wachezaji wao wapya baada kuwaunua Anders Herrera kutoka Athletic Bilbao na Luke Shaw kutoka Southampton.
Wachezaji wapya wanaohusishwa sana Man United ni Kiungo wa Chile, Arturi Vidal, anaechezea Juventus ya Italy, Thomas Vermaelen, Nahodha wa Arsenal, na Wachezaji Watatu waliokuwepo kwenye Kikosi cha Netherlands huko Brazil chini ya Van Gaal, Daley Blind, Bruno Martins Indi na Stefan De Vrij.
Popular: Van Gaal looks towards a crowd of Holland fans after helping his country finish third in BrazilIshu ya Vidal imeongezeka nguvu hasa baada ya Mchezaji huyo mwenyewe kukiri anaihusudu Man United na pia sababu ya Mchezaji wa Man United, Patrice Evra kwenda Juve, kitu ambacho kinaonekana kulainisha ujio wa Vidal huko Old Trafford.
Kuhusu Thomas Vermaelen, Nahodha huyo wa Arsenal anaaminika anataka kuihama Klabu yake kwa kukosa Namba na zipo taarifa ameshaafikiana maslahi binafsi na Man United na kinachochelewesha ni upande wa Arsenal ambao wanaitaka Man United waongeze Dau na pia Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, kutaka kupata mbadala wake kabla hajaruhusu aondoke.
Tetsi zaidi za Wachezaji hao wapya kwenda au kutokwenda Man United zitapatikana mara baada ya Louis van Gaal kutambulishwa rasmi huko Old Trafford hapo Alhamisi.
Ijumaa, Van Gaal na Kikosi chake cha Man United kitaruka kwenda California kupiga Kambi ya Mazoezi kabla ya kucheza Mechi yao ya Kwanza ya Ziara yao huko Marekani hapo Julai 23.


Semina na mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness test) kwa waamuzi wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na baadhi ya wale wa daraja la kwanza wenye kiwango cha juu (elite) itafanyika jijini Dar es Salaam.
Waamuzi 30 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar watashiriki kwenye semina hiyo itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia Julai 21 hadi 26 mwaka huu.
Mkufunzi wa FIFA kwa Kanda ya Kusini mwa Afrika, Carlos Henriques kutoka Afrika Kusini ndiye atakayeendesha semina hiyo akisaidiwa na Watanzania Charles Mchau kutoka Kilimanjaro, Juma Ali David (Zanzibar), Joan Minja (Dar es Salaam) na Riziki Majala (Pwani).
Waamuzi na waamuzi wasaidizi wa FIFA watakaoshiriki semina hiyo ni Ferdinand Chacha (Mwanza), Hamisi Chang’walu (Dar es Salaam), Israel Mujuni (Dar es Salaam), Jesse Erasmo (Morogoro), John Kanyenye (Mbeya), Josephat Bulali (Zanzibar), Kinduli Ali (Zanzibar), Oden Mbaga (Dar es Salaam), Ramadhan Ibada (Zanzibar), Samwel Mpenzu (Arusha) na Waziri Sheha (Zanzibar).


Kwa upande wa waamuzi wa daraja la kwanza ni Abdallah Kambuzi (Shinyanga), Agnes Pandaleo (Arusha), Ahamada Simba (Kagera), Arnold Bugado (Singida), Charles Simon (Dodoma), Dalila Jafari (Zanzibar), Frank Komba (Pwani), Helen Mduma (Dar es Salaam), Issa Bilali (Zanzibar) na Issa Haji (Zanzibar).
Wengine ni Janeth Balama (Iringa), Jonesia Rukyaa (Kagera), Lulu Mushi (Dar es Salaam), Martin Saanya (Morogoro), Mary Kapinga (Ruvuma), Mbaraka Haule (Zanzibar), Mfaume Ally (Zanzibar), Mohamed Mkono (Tanga) na Soud Lila (Dar es Salaam). 
Washiriki wa semina hiyo na wakufunzi wanatakiwa kuwasili jijini Dar es Salaam, Julai 20 mwaka huu.


Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo (katikati), ambaye kampuni yake inaandaa tamasha hilo, akizungumza kwenye mkutano huo.

Mkutano ukiendelea...

Sehemu ya mapaparazi waliofika kwenye tukio hilo.

Rais wa Chama cha Ngumi za Kulipwa nchini (T.P.B.O) Yasin Abdallah (katikati) ambao ndiyo wasimamizi wa pambano la Maugo na Mashali katika tamasha hilo, akizungumzia pambano hilo.

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (mwenye miwani) na Mkurugenzi Chuo cha Uandishi wa Habari, Biashara na Utawala cha Mlimani kilichopo Mbezi Kwa-Msuguri jijini Dar, Hassan Ngoma (kushoto kwa Mrisho), wakifuatilia kinachoendelea.

Khalid Chokoraa wa Bendi ya Mapacha Watatu akifuatilia kinachoendelea.

Mwakilishi na Rais wa Bongo Muvi Unity, Steve ‘Nyerere’, akielezea jinsi watakavyowagaragaza wasanii wa Bongo Fleva kwenye pambano la soka.

Mwakilishi wa timu ya Bongo Fleva, Inspector Haruni, akijibu mapigo kwa kueleza jinsi watakavyowararua Bongo Muvi Unity. Kushoto ni mratibu wa tamasha hilo, Luqman Maloto, na Eric Shigongo.

Bondia Mada Maugo akijitapa kumchapa mpinzani wake, Thomas Mashali ‘Simba Asiyefugika’.

Mashali akimjibu Maugo na kujitapa kuendeleza kichapo.

Mbunge Hamisi Kigwangala anayeiwakilisha timu ya wabunge wa Simba akieleza jinsi walivyojiandaa kuwaadabisha wabunge wa Yanga.

Msanii wa filamu, Jacob Steven ‘JB’, ambaye atachapana na msanii mwenzake, Issa Mussa ‘Clouds 112′, akichimba mkwara jinsi atakavyomkalisha msanii huyo.

Shigongo ‘akiwakutanisha’ mabondia wenye upinzani mkali, Mashali (kushoto) na Maugo (kulia).

Clouds 112 (kushoto) akimchimbia mkwara JB ambaye aliishia kumuangalia kidharau na kusema anasubiri siku ya Agosti 8 katika Uwanja wa Taifa.

Sehemu ya wanahabari wakipata maelezo.

WASHIRIKI wa ‘Tamasha la Usiku wa Matumaini’ leo wametambiana kwenye mkutano na vyombo vya habari uliofanyika Hoteli ya Atriums iliyopo Sinza, Afrika-Sana jijini Dar es Salaam.
Katika mkutano huo wa tamasha hilo la burudani mabondia, Mada Maugo na Thomas Mashali, kila mmoja amejitapa kumchakaza mwenzake katika pambano hilo huku Mbunge wa Nzega, Dkt. Hamis Kigwangala, aliyewawakilisha wabunge wa timu ya Simba alijitapa timu yake kuwamaliza Yanga.
Msanii wa Filamu za Maigizo, Issa Mussa ‘Clouds 112′ ambaye katika tamasha hilo atachapana makonde na Jacob Steven ‘JB’ katika mchezo wa ‘boxing’ wote wameahidi kutifuana ‘kinomanoma’.
Rais na mwakilishi wa timu ya Bongo Muvi Unity, Steve Mengere ‘Steve Nyerere’, alitamba timu yake kuigaragaza timu ya Bongo Fleva ambapo mwakilishi wake, Haruni Kahena ‘Inspector Haruni’, alisema wao ndio watakaoibuka kidedea na kuwapiga Bongo Muvi Unity kwa mabao 7-1 kama walivyofanywa Wabrazil na Ujerumani wiki iliyopita kwenye nusu fainali za Kombe la Dunia.
Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika Agosti 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambapo huu utakuwa ni mwaka wa tatu mfululizo kufanyika likiandaliwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd.

(HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS / GPL. )


Nervous: Scolari sings the national anthem before their third place play-off against HollandKocha wa Brazil Luiz Felipe Scolari amelaumiwa kwa kichapo ilichopata Brazil Ripoti nchini Brazil zinasema kuwa kocha wa timu ya taifa ya Brazil,Luiz Felipe Scolari, ameacha kazi kama meneja wa timu hiyo. Scolari alilaumiwa pakubwa sana kwa timu ya Brazil kupata kichapo kibaya ilipocheza na Ujerumani ambao wameibuka mabingwa wa kombe la dunia mwaka huu. Kichapo hicho kilikuja wakati wa mechi ya nusu fainali dhidi ya Ujerumani. Taarifa rasmi huenda ikatolewa baadaye leo na shirikisho la soka la Brazil.Luiz Felipe Scolari

Luiz Felipe Scolari  kwenye wasiwasi kubwa baada ya kupoteza kwa kufungwa bao  3-0 l kutoka kwa Holland juzi jumamosi.

Scolari aliwaongoza Brazil na waliambulia nafasi ya Nne katika Michuano ya fainali za kombe la Dunia 2014

Scolari kwenye majanga ya kufungwa mara kwa mara kwenye mechi zao za mwisho, Mikono kichwani hana hili wala lile!!!

Mashabiki wa Brazil wakimshukuru kocha wao Scolari kwa kuwa nao tangu 2002 lakini sasa wanataka apotee katika Klabu hiyo baada ya kuona wanaambulia vichapo mwishoni mwa Kombe la Dunia 2014 huko kwao Brazil.


Final showing: Nike's ties with Manchester United will end after the coming seasonManchester United leo hii imetangaza kufikia makubaliano na Kampuni ya Adidas ya Miaka 10 ya Jezi na Vifaa vya Michezo ambapo watalipwa Pauni Milioni 750 na hii ndio Dili kubwa Duniani kwa Mikataba ya aina hiyo.
Mkataba wa pande hizo mbili utaanza Msimu wa Mwaka 2015/16 na kila Mwaka Man United italipwa Pauni Milioni 70 ikiipita Real Madrid ambayo ilikuwa ikizoa Pauni Milioni 31 kwa Mwaka pia kutoka kwa Adidas.

Msimu huu unaokuja, wa 2014/15, Man United itamaliza Mkataba wa kuvaa Jezi za Nike ambazo wamekuwa nazo kwa Miaka 13 hadi sasa.


ANGALIA WALIVYOWAZIDI WENZAO!

TIMU
KAMPUNI
KWA MWAKA
MIAKA
JUMLA
Manchester United
Adidas
£70m
10 years
£700m
Real Madrid
Adidas
£31m
8 years
£248m
Chelsea
Adidas
£30m
10 years
£300m
Arsenal
Puma
£30m
5 years
£170m
Barcelona
Nike
£27m
10 years
£270m
Liverpool
Warrior
£25m
6 years
£150m
Manchester City
Nike
£12m
6 years
£72m


Washambuliaji Thomas Ulimwengu na Mbwana Samata wa klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wanawasili nchini keshokutwa alfajiri (Julai 16 mwaka huu) kwa ajili ya mechi dhidi ya Msumbiji (Mambas).
Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika (AFCON) kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Mambas itachezwa Jumapili (Julai 20 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ulimwengu na Samata watawasili saa 12 asubuhi kwa ndege ya EgyptAir wakitokea Tunisia ambapo timu yao ya TP Mazembe imepiga kambi kwa ajili ya mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imepiga kambi Tukuyu mkoani Mbeya ikijiandaa kwa mechi hiyo itakayochezeshwa na mwamuzi Mahmoud Ashour kutoka Misri.

Stars itarejea jijini Dar es Salaam siku ya Ijumaa (Julai 18 mwaka huu) kwa ajili ya mechi hiyo wakati Mambas nao wanatarajiwa kutua siku hiyo hiyo. Mechi ya marudiano itachezwa kati ya Agosti 1 na 3 mwaka huu nchini Msumbiji.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

waliotembelea blog