Tuesday, July 15, 2014


Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo (katikati), ambaye kampuni yake inaandaa tamasha hilo, akizungumza kwenye mkutano huo.

Mkutano ukiendelea...

Sehemu ya mapaparazi waliofika kwenye tukio hilo.

Rais wa Chama cha Ngumi za Kulipwa nchini (T.P.B.O) Yasin Abdallah (katikati) ambao ndiyo wasimamizi wa pambano la Maugo na Mashali katika tamasha hilo, akizungumzia pambano hilo.

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (mwenye miwani) na Mkurugenzi Chuo cha Uandishi wa Habari, Biashara na Utawala cha Mlimani kilichopo Mbezi Kwa-Msuguri jijini Dar, Hassan Ngoma (kushoto kwa Mrisho), wakifuatilia kinachoendelea.

Khalid Chokoraa wa Bendi ya Mapacha Watatu akifuatilia kinachoendelea.

Mwakilishi na Rais wa Bongo Muvi Unity, Steve ‘Nyerere’, akielezea jinsi watakavyowagaragaza wasanii wa Bongo Fleva kwenye pambano la soka.

Mwakilishi wa timu ya Bongo Fleva, Inspector Haruni, akijibu mapigo kwa kueleza jinsi watakavyowararua Bongo Muvi Unity. Kushoto ni mratibu wa tamasha hilo, Luqman Maloto, na Eric Shigongo.

Bondia Mada Maugo akijitapa kumchapa mpinzani wake, Thomas Mashali ‘Simba Asiyefugika’.

Mashali akimjibu Maugo na kujitapa kuendeleza kichapo.

Mbunge Hamisi Kigwangala anayeiwakilisha timu ya wabunge wa Simba akieleza jinsi walivyojiandaa kuwaadabisha wabunge wa Yanga.

Msanii wa filamu, Jacob Steven ‘JB’, ambaye atachapana na msanii mwenzake, Issa Mussa ‘Clouds 112′, akichimba mkwara jinsi atakavyomkalisha msanii huyo.

Shigongo ‘akiwakutanisha’ mabondia wenye upinzani mkali, Mashali (kushoto) na Maugo (kulia).

Clouds 112 (kushoto) akimchimbia mkwara JB ambaye aliishia kumuangalia kidharau na kusema anasubiri siku ya Agosti 8 katika Uwanja wa Taifa.

Sehemu ya wanahabari wakipata maelezo.

WASHIRIKI wa ‘Tamasha la Usiku wa Matumaini’ leo wametambiana kwenye mkutano na vyombo vya habari uliofanyika Hoteli ya Atriums iliyopo Sinza, Afrika-Sana jijini Dar es Salaam.
Katika mkutano huo wa tamasha hilo la burudani mabondia, Mada Maugo na Thomas Mashali, kila mmoja amejitapa kumchakaza mwenzake katika pambano hilo huku Mbunge wa Nzega, Dkt. Hamis Kigwangala, aliyewawakilisha wabunge wa timu ya Simba alijitapa timu yake kuwamaliza Yanga.
Msanii wa Filamu za Maigizo, Issa Mussa ‘Clouds 112′ ambaye katika tamasha hilo atachapana makonde na Jacob Steven ‘JB’ katika mchezo wa ‘boxing’ wote wameahidi kutifuana ‘kinomanoma’.
Rais na mwakilishi wa timu ya Bongo Muvi Unity, Steve Mengere ‘Steve Nyerere’, alitamba timu yake kuigaragaza timu ya Bongo Fleva ambapo mwakilishi wake, Haruni Kahena ‘Inspector Haruni’, alisema wao ndio watakaoibuka kidedea na kuwapiga Bongo Muvi Unity kwa mabao 7-1 kama walivyofanywa Wabrazil na Ujerumani wiki iliyopita kwenye nusu fainali za Kombe la Dunia.
Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika Agosti 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambapo huu utakuwa ni mwaka wa tatu mfululizo kufanyika likiandaliwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd.

(HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS / GPL. )

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog