Friday, October 9, 2015


Theo Walcott aitanguliza England mbele.Theo akishangilia goli lake usiku huuTheo Walcott kaifungia England bao dakika ya 45 na kuongoza kwa bao 1-0 dhidi timu ya Estonia, Bao la pili limefungwa na Raheem Sterling dakika ya 85 na mtanange kumalizika kwa bao Bao 2-0 England wakiibuka na Ushindi.Sir Bobby Charlton akipata picha ya pamoja na Wayne Rooney baada ya kupewa kiatu cha dhahabu kwa kuvunja rekodi ya mabao 49


Sunderland imemteua Sam Allardyce kuwa Meneja wao mpya kwa Mkataba wa Miaka Miwili.
Sunderland wamekuwa hawana Meneja tangu Jumapili iliyopita baada ya Dick Advocaat kutimka akiiacha Klabu hiyo ikiwa Nafasi ya Pili toka mkiani mwa Ligi Kuu England.
Advocaat, Raia wa Holland mwenye Miaka 68, aliteuliwa kushika wadhifa wa Umeneja wa Sunderland Mwezi Machi wakati Timu ikiwa hatarini kushuka Daraja Msimu uliopita.
Baada ya kuinusuru kutoshuka Daraja, Advocaat alikuwa ndio amemaliza Mkataba wake lakini akaongeza Mkataba wa Mwaka mmoja ambao ungembakisha hadi mwishoni mwa Msimu huu wa 2015/16.
Katika Kipindi cha Miaka Minne, Sunderland wameajiri Mameneja 6.

Mameneja waliopita katika kipindi hicho ni Steve Bruce, alietimuliwa Novemba 2011, Martin O'Neill, Paolo di Canio, Gus Poyet, Advocaat na sasa Sam Allardyce.
Allardyce, mwenye Miaka 60 na maarufu kama Big Sam, amekuwa hana kazi tangu mwishoni mwa Msimu uliopita baada ya Mkataba wake na West Ham kumalizika.
Mara baada kutua Sunderland, Allardyce alikiri ana kazi ngumu kwa kusema: “Ni wazi ni kazi yenye changamoto kubwa. Lakini nategemea kuirekebisha Timu na kuleta mafanikio anayotaka kila Mtu.”
Big Sam ashawahi kuichezea Sunderland kati ya Mwaka 1980 na 1981 na sasa ameweka Historia ya kuwa Mtu wa Kwanza kuwahi kuwa Meneja wa Klabu mbili zenye upinzani wa Jadi, Sunderland na Newcastle.
Mechi ya kwanza kwa Allardyce kama Meneja wa Sunderland ni Ugenini na West Bromwich Albion hapo Oktoba 17 na ya kwanza Uwanja wa Nyumbani Stadium of Light ni hapo Oktoba 25 dhidi ya Newcastle.


Sam Allardyce:Kazi ya Umeneja
1989–1991 West Bromwich Albion (Msaidizi)
1991–1992 Limerick (Meneja Mchezaji)
1992 Preston North End (Meneja wa Muda)
1994–1996 Blackpool
1997–1999 Notts County
1999–2007 Bolton Wanderers
2007–2008 Newcastle United
2008–2010 Blackburn Rovers
2011–2015 West Ham United
2015– Sunderland



Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kinachodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premieum Lager kimewasili salama katika mji wa Blantyre nchini Malawi jioni ya leo tayari kwa mchezo wa marudiano siku dhidi ya wenyji siku ya jumapili.
Stars inayonolewa na makocha wazawa Charles Boniface Mkwasa na Hemedi Morocco iliondoka leo kwa usafiri wa shirika la ndege la Fastjet na kuwasili jiji la Lilongwe saa 4 asubuhi kabla ya kuanza safari ya bus kuelekea Blantayre iliyochukua takribani masaa 3.
Wachezaji wote wapo katika hali nzuri kuelekea katika mchezo wa marudiano dhidi ya Malawi siku ya Jumapili ambapo Stars itashuka dimbani kusaka matokeo mazuri yatakayoiwezesha kufuzu kwa hatua ya pili, katika mchezo wa awali uliochezwa jijini Dar es salaam, Stars iliibuka na ushindi wa mabao 2- 0.
Stars inatarajiwa kufanya mazoezi kesho jioni katika uwanja wa Kamuzu Banda uliopo Blantyre, uwanja ambao utatumika kwa mchezo wa siku ya Jumapili.

Kuelekea mchezo huo wa marudiano, Kocha wa Stars Charles Mwasa amesema vijana wake wote wapo katika hali nzuri kiafya, kifikra na morali ni ya hali ya juu kuelekea kwenye mchezo huo.
Katika hatua nyingine mabus mawili yenye washabiki wa Stars Supporter yako njiani kuelekea nchini Malawi kwa ajili ya kuipa sapoti timu ya Taifa (Taifa Stars) katika mchezo huo wa Jumapili.


Jurgen Klopp amekubali kuwa Meneja wa Liverpool kwa Mkataba wa Miaka Mitatu ambao anatarajiwa kuusaini Leo na Ijumaa kuanuliwa rasmi kama Meneja ,pya.
Klopp, Mjerumani mwenye Miaka 48, anamrithi Brendan Rodgers aliefukuzwa Jumapili iliyopita baada ya kudumu Miaka 3 ½ lakini Msimu huu Timu inasuasua na ipo Nafasi ya 10 kwenye Ligi Kuu England.
Klopp amekuwa hana kibarua tangu Mei alipoondoka Klabu ya Germany Borussia Dortmund baada ya kukaa nayo kwa Miaka 7.
Akiwa Liverpool, Klopp atakuwa nao Wasaidizi wake walewale aliokuwa nao Dortmund ambao ni Zeljko Buvac na Peter Krawietz.
Mechi ya kwanza ya Klopp akiwa na Liverpool, ambayo imeshinda Mechi 4 tu kati ya 11 iliyocheza Msimu huu, itakuwa ni ya Ligi Ugenini huko White Hart Lane Jijini London dhidi ya Tottenham hapo Oktoba 17.
Kwa sasa Ligi imesimama kupisha Mechi za Kimataifa na itarejea kilingeni hiyo hiyo Oktoba 17.

Klopp, ambae baada ya kustaafu uchezaji wake wa Soka akichezea Mainz ya Germany maisha yake yote ya Soka, alianzia kazi ya Umeneja akiwa hapo hapo Mainz na kisha kuhamia Borussia Dortmund.
Akiwa na Dortmund Klopp aliweza kutwaa Ubingwa wa Bundesliga mara 2, Mwaka 2011 na 2012, pamoja na DFB-Pokal Mwaka 2012, DFL-Supercup kwenye Miaka ya 2008, 2013 na 2014 na pia kuifikisha Klabu hiyo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI Mwaka 2013.
Klopp amewahi kutwaa Tuzo ya Meneja Bora wa Germany mara mbili katika Miaka ya 2011 na 2012.


Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) leo limeingia mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya shilingi milioni mia nne hamsini (450,000,000), na kituo cha luninga cha Star Tv kurusha matangazo ya Ligi Daraja la Kwanza nchini (FDL).
Akiongea na waandishi wa habari wakati wa kusaini mkataba huo, Rais wa TFF Jamal Malinzi aliishukuru kampuni ya Sahara Media Group kwa kuamua kuwekeza katika mpira wa miguu nchini kwa kuamua kuonyesha ligi daraja la kwanza.
Malinzi ameviomba vilabu vya FDL kutumia udhamini huo kama chachu ya mafanikio na kufanya vizuri katika ligi hiyo itakayotoa timu tatu za kupanda Ligi Kuu ya Vodacom (FDL) msimu ujao.

Aidha Malinzi amewaomba wamiliki wa viwanja vinavyotumika kwa michezo ya FDL kuviweka katika hali nzuri ya matunzo ili mechi zinazochezwa katika viwanja hivyo ziweze kuwa nzuri kiufundi na muonekano wa kwenye Luninga.
Jumla ya udhamini wa Ligi Daraja la Kwanza kwa sasa ni shilingi bilioni moja na milioni mia tatu hamsini (1,350,000,000) ikiwa ni udhamini wa milioni mia tisa (900,000,000) kutoka StarTimes mdhamini mkuu wa FDL na milioni mia nne hamsini (450,000,000) kutoka StarTv.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Sahara Media Group, Samwel Nyala ameishukuru TFF kwa kuwapa nafasi hiyo ya haki za matangazo kampuni yake kwa michezo ya Ligi Daraja la kwanza nchini (FDL).
Katika kuhakikisha michezo hiyo inaonekana kwa wingi zaidi, Nyala alisema watafungua mkondo (Channel) ya Star Sports Plus itakayokua itakayokuwa inaonyesha michezo tu ikiwemo ligi daraja la kwanza (FDL).



Jioni ya October 7 klabu ya Liverpool ya Uingereza ilitangaza rasmi kuingia mkataba wa miaka mitatu na kocha Jurgen Klopp na kujiunga na klabu hiyo, taarifa zilizotoka  Ijumaa ya October 8 ni kuwa atatambulishwa mbele ya waandishi wa habari pamoja na kufanya mahojiano na waandishi wa habari.
2D3BB6EF00000578-3266211-image-a-31_1444388005147
Jurgen Klopp aliwahi kuwa kocha wa Borussia Dortmund ya Ujerumani kabla ya mwishoni mwa msimu uliyomalizika kuacha kazi na kukaa bila timu kwa kipindi fulani. Jurgen Klopp ametambulishwa Ijumaa ya October 9 hii ikiwa ni siku moja imepita toka asaini mkataba wa miaka 3 wenye kipengele cha kuongezewa mwaka mmoja zaidi, kocha huyo amesaini mkataba wenye thamani ya pound milioni 21.
2D3A48B900000578-3266211-There_was_time_for_Klopp_Werner_and_Ayre_to_share_a_joke_at_the_-a-29_1444387955704
Jurgen Klopp ambaye alianza kazi ya ukocha katika klabu ya Mainz 05 mwaka 2001 – 2008 ambapo alihamia katika klabu ya Borussia Dortmund. Moja kati ya kauli zinazovutia wengi alizozungumza katika mkutano na waandishi wa habari ni kuwa yeye ni kocha wa kawaida kauli ambayo ilihusishwa kama kijembe kwa Jose Mourinho ambaye anajiita ‘the special one’.
2D3A78AB00000578-0-image-a-25_1444384875520
” Ni heshima kubwa kuwa kocha katika moja kati ya klabu kubwa duniani, hii ni fursa kwangu ya kujaribu na kuisaidia klabu, haukuwa muda sahii kwa mimi kujiunga lakini naweza sema ni wakati mzuri kwangu. Sitajiita jina lolote sabau mimi ni  mtu wa kawaida na mama yangu anatazama huu mkutano kupitia Tv akiwa nyumbani, ila kama utapenda kuniita jina itakuwa vizuri ukiniita ‘the normal one’ ” >>> Jurgen Klopp
2D3AB05200000578-0-image-a-28_1444384887414
2D39944F00000578-0-image-a-30_1444384909995


Michuano ya mechi za kuwania kufuzu michuano ya Euro 2016 bado inaendelea kwa michezo kadhaa kupigwa, kwa upande wa timu ya taifa ya Ureno ambao walishinda kwa goli 1-0 dhidi ya timu ya taifa ya Denmark . Baada ya ushindi huo Ijumaa ya October 9 Cristiano Ronaldo alipiga picha za mlo wake wa mchana.
Cristiano Ronaldo alipost picha ya msosi wake wa mchana aliyokula wakati ambao alikuwa anajiandaa kurudi kwao ni diet ambayo imekamilika kwa kiwango kikubwa, kwani kulikuwa na mayai, viazi, nyama, matunda, maji ya kunywa juisi. Baada ya kuweka picha hiyo katika account yake ya instagram mtandao wa dailymail.co.uk ulichambua kila aina ya chakula kilichomo katika diet hiyo.
2D3C80B500000578-0-image-a-96_1444395445042
Katika ratiba ya chakula cha mchana cha Ronaldo hakuna chakula ambacho kina asili ya sukari nyingi lengo linatajwa kuwa ni kulinda mwili wake ili kuendelea kuwa sawa kwa michuano mingine. Ureno walicheza mechi dhidi ya Denmark na kuibuka na ushindi wa goli 1-0, huu ukiwa ushindi wao wa sita katika mechi zao saba za kuwania kufuzu michuano ya Euro 2016.
2D35A11600000578-3266440-Ronaldo_right_looks_to_escape_the_attentions_of_Lars_Jacobsen_du-a-104_1444396967061



Baada ya klabu ya Liverpool kumfukuza kazi aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Brendan Rodgers kutokana na mwenendo mbovu wa timu yao, watu mbalimbali katika uchambuzi wa masuala ya soka wamekuwa wakizungumza mitazamo tofauti tofauti kuhusiana na maamuzi hayo.
October 9 kocha wa klabu ya Arsenal ya Uingereza Arsene Wenger amezungumzia kuhusiana na mtazamo wake juu ya uamuzi wa viongozi wa Liverpool kumfuta kazi Brendan Rodgers, Wenger ambaye timu yake ya Arsenal iliwahi kupitia katika wakati mgumu kwa miaka kadhaa ila hakufukuzwa kazi.
2D3C29B300000578-0-image-a-27_1444390674750
Wenger na Rodgers wakipeana mikono katika mechi timu zao zilipo kutana.
Wenger ana amini Rodgers angepewa zaidi ya mechi nane za kuendelea kuifundisha timu hiyo ili klabu iweze kuamua >>>”walikuwa katika nafasi nzuri ya kuwania ubingwa katika miaka miwili iliyopita lakini sasa sielewi kwa nini wamefanya hivi, sioni sababu za msingi za kufanya uamuzi wa haraka namna hii, kwangu mimi ni ngumu kuelewa”
2D2D6C4A00000578-3266324-image-a-1_1444399238639
Klabu ya Liverpool ya Uingereza haijawahi kutwaa ubingwa wa Uingereza toka mwaka 1990, lakini katika historia imetwaa taji hilo mara 18, lakini klabu hiyo ni moja kati ya vilabu vilivyotwaa taji la Ligi Kuu Uingereza mara nyingi zaidi. Hivyo kwa sasa klabu ya Liverpool imemchagua Jurgen Klopp.


Michuano ya kuwania kufuzu kucheza Euro 2016 imeendelea kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja mbalimbali, moja kati ya mechi zilizochezwa usiku wa October 9, timu ya taifa ya Uingereza ilikuwa mwenyeji wa timu ya taifa ya Estonia.
1444421746643_lc_galleryImage_Football_England_v_Estoni
 Mechi ambayo ilikuwa ngumu kwa Uingereza kuweza kupata nafasi ya kufunga goli kutokana na timu ya taifa ya Estonia kuwa imejiandaa vyema kuwakabili waingereza hao, uwezo wa kuhimiri mashambulizi ya waingereza ulidumu kwa dakika 44 kabla ya dakika ya 45 Theo Walcott kupachika goli la kwanza na kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0 dhidi ya Estonia.
1444420076294_lc_galleryImage_SPT_ITE_091015__UEFA_Euro
Uingereza walirudi uwanjani kipindi cha pili wakiwa na faida ya goli moja kitu ambacho kiliwapelekea Estonia kujaribu kutafuta nafasi ya kusawazisha goli hilo ila Raheem Sterling aliwakatisha tamaa ya kusawazisha goli hilo ambalo lingeweza kuwafanya waondoke na Point moja, Sterling alipachika goli la pili dakika ya 85 ya mchezo na kufanya mechi imalizike kwa Uingereza kuibuka na ushindi wa goli 2-0.
1444416882249_lc_galleryImage_England_s_defender_Nathan

waliotembelea blog