obin van Persie yupo FIT kwa derby dhidi ya majirani zao Man city
Na Anwar binde,
Robin van Persie amejitangaza kuwa yupo vizuri kwa mchezo wa jumapili dhidi ya wapinzani wao wa jadi Manchester city.
Van Persie amekosekana michezo sita ya Manchester united kutokana na kuumia enka wakati man utd walipooteza kwa 2-1 dhidi ya Swansea tarehe 21 mwezi wa pili.
Kocha Louis van Gaal wiki iliyopita alisema hakutegemea van Persie kupona kwa haraka hivyo na kua vizuri kupambana na city jumapili ijayo pale Old Traffod,lakini Van Persie mwenyewe alijitangaza kwa mashabiki na kuwaambia yupo vizuri.
Hata kama van Gaal akifikiria kumpa nafasi katika mechi yao ya upinzani wa jadi dhidi ya city bado ni ngumu sana kuona jinsi gani ataendana na kasi na mfumo wa sasa ya kitika kikosi cha kwanza
Pengo la mholanzi ambae amefunga magoli 10 tu msimu huu halikuonekana kabisa pale alipoumia,na tangu alipoumia man united imepoteza mchezo mmoja tu tena dhidi ya mabosi wake wa zamani Arsenal kombe la FA.
United walipata ushindi katika ratiba ngumu dhidi ya Tottenham na Liverpool na jumamosi iliyopita ushindi wa 3-1 dhidi ya Aston Villa ushindi uliofanya kuwa juu ya city kwa pointi moja.
Wyne Rooney alifunga goli moja matata kwa mkwaju wa haja,kapteni huyo wa united amekua na kiwango bora kabisa pale mbele katika mfumo wa 4-3-3 akisaidiana na Ashley Young na Juan Mata ambae aliingia nyavuni mara mbili katika ushindi wa 2-1 pale Anfield wiki mbili na nusu zilizopita.
Marouane Fellaini pia anatoa mchango mkubwa katika majukumu ya kiungo na ushambuliaji sehemu ambayo kwa sasa imetulia sana kwenye kikosi hicho cha Manchester united.
Ushindi dhidi ya city iliyopoteza mwelekeo na kuwa chini ya kiwango utaongeza wigo wa pointi kufikia nne na kuongeza matumaini ya Van Gaal kucheza ligi ya mabingwa msimu ujao.
- Mshambuliaji Robin van persie amepona kabisa kwa mchezo wa jumapili
- Alikosekana tangu tarehe 21 mwezi wa pili
- Si rahisi kwa van Persie kuanza kikosi cha kwanza dhidi ya city.