Wednesday, April 8, 2015


MUDA mfupi uliopita kumefanyika mkutano wa waandishi wa habari na uongozi wa African Stars wana Twanga Pepeta. Mkutano huo uliofanyika Nemax Hotel, Kinondoni, Dar es Salaam, mwanamuziki wa siku nyingi aliyekuwa akiendesha bendi yake ya Extra Bongo ametangaza kuwa anarudi kwenye bendi yake ya zamani ya African Stars maarufu kwa Twanga Pepeta. Pamoja na Ally Chocky waliokuweko katika mkutano huo ni Mkurugenzi wa Twanga Bi Asha Baraka, kiongozi wa bendi Luiza Mbutu, na mcheza shoo mkongwe Nyamwela ambaye pia ndie Mwenyekiti wa chama cha wacheza show Tanzania. Onyesho la kwanza la Chocky katika bendi hiyo litakuwa tarehe 18 mwezi huu wanne, japo ukumbi utakuwa upi haijatajwa lakini Chocky alisema kuwa tayari ana tungo tatu atakazoanza nanzo nazo ni Usiyaogope maisha, Kichwa chini, na No discussion.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog