Thursday, October 22, 2015


  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akionyesha waandishi wa habari leo (hawapo pichani) kitabu cha maadili ya uchaguzi kilichosainiwa na viongozi wa vyama vya siasa waliosimamisha wagombea katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25.

 Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Jeshi la Polisi leo Mkuu wa Jeshi hilo IGP Ernest Mangu amesema kuwa ulinzi utaimarishwa maeneo yote kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha kuwa taifa linapita salama katika kipindi hiki cha kupiga kura, kuhesabu na kutangaza matokeo ya uchaguzi.

 Ametoa rai kwa wananchi kujitokeza kupiga kura siku  hiyo bila wasiwasi wa aina yoyote ili kuweza kutumia haki yao ya kikatiba kuchagua viongozi.
(Picha na Francis Dande)
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akionyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) kitabu cha maadili ya uchaguzi kilichosainiwa na viongozi wa vyama vya siasa waliosimamisha wagombea katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 ambapo amewataka watu wote kutii sheria bila shuruti wakati wa uchaguzi.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akifafan jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)


 Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati Airtel ilipozindua  smartifoni mpya ijulikanayo kama Magnus Bravo Z10zitakazopatikata katika maduka yote ya Airtel zikiwa zimeunganishwa na ofa ya Smartifonika  kutoa  muda wa maongezi wa dakika 150, 150MB na SMS 150 kwa kipindi cha miezi sita. Kulia ni bi Anethy Muga meneja masoko wa Airtel. Hafla ya uzinduzi imefanyika jana katika makao makuu ya Airtel Dar es salaam
 Meneja Masoko wa Airtel Bi Anethy Muga akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati Airtel ilipozindua  smartifoni mpya ijulikanayo kama Magnus Bravo Z10 zitakazopatikata katika maduka yote ya Airtel zikiwa zimeunganishwa na ofa ya Smartifonika  kutoa  muda wa maongezi wa dakika 150, 150MB na SMS 150 kwa kipindi cha miezi sita. Kushoto ni Afisa Matukio wa Airtel Bi, Dangio Kaniki wakati wa Hafla ya uzinduzi iliyoyika jana katika makao makuu ya Airtel Dar es salaam.
 Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki (kushoto) akiwa na  Meneja masoko wa Airtel Anethy Muga (kulia) wakionyesha simu mpya zilizoingizwa sokoni zikiwa na ofa ya Airtel smartifonika aina ya Mgnum Bravo Z10 wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika makao makuu ya Airtel leo
Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki akijaribu kupiga picha kwa kutumia kamera ya mbele ya simu mpya aina ya Magnus Bravo Z10 inayopatikana katika maduka ya Airtel kuanzia sasa ikiwa na ofa ya Smartifonika, uzindunzi wa kuingiza sokoni simu hii yenye uwezo wa kutumia  laini mbili umefanyika jana katika makao makuu ya Airtel.

  AIRTEL  Tanzania leo imezindua smartifoni mpya na yenye ubora zaidi ijulikanayo kama Magnus Bravo Z10 ambapo zinapatikata sasa hivi  kwenye maduka yote ya Airtel nchini zikiwa zimeunganishwa na ofa ya Smartifonika  inayompatia mteja muda wa maongezi wa dakika 150, 150MB na SMS 150 kwa kipindi cha miezi sita.

Akiongea na waandishi wa habari Meneja masoko wa Airtel Tanzania Aneth Muga amesema “Airtel tumekuletea Simu mpya ya Magnus Bravo Z10 ili kukuwezesha mteja wetu kuendelea kufurahia huduma zote za Airtel na zile huduma zote za kisasa za smartifoni ukiwa mahali popote
 “Magnus Bravo Z10 toka Airtel inatumia laini mbili, ina radio, kioo (screen) kubwa ili kukupa raha zaidi kuona vyema unapokuwa unaitumia, pia imewekewa kamera zenye uwezo mkubwa mbele na nyuma za 5mp ili kukupa taswira au picha nzuri utakazopiga karibu au mbali ukiwa na ndugu, jamaa na marafiki” alielezea Bi Muga
“Vilevile ili  uweze kufurahia huduma zote za mitandao, Airtel tumehakikisha tayari simu hii inamitandao yote ya kijamii kama facebook, Instagram, twitter na mingine mengi” . Alisema Bi Muga
Simu hii inapatikana sasa katika maduka yote ya Airtel nchini kwa gharama nafuu kuliko zote ya sh. 75,000  tu.


Kiungo wa kimataifa wa Ujerumani anayeichezea klabu ya Manchester United ya Uingereza Bastian Schweinsteiger October 22 ameingia katika headlines baada ya mtengenezaji wa midoli wa kichina kutengeneza mdoili unaofanana na yeye na kuita jina lake.
Bastian-Schweinsteiger-lookalike-Nazi-doll-named-Bastian
Mdoli huyo ambaye ametengenezwa kwa muonekano wa sura ya Bastian Schweinsteiger na mtengenezaji wa mdoli huyo amempa jina la ‘Bastian’ sawa na jina halisi la kiungo huyo wa Man United, kingine cha jamaa wa kichina aliyetengeneza sanamu hiyo kaiweka katika mavazi ya jeshi la Nazi.
Bastian-Schweinsteiger-lookalike-Nazi-doll-named-Bastian (1)
Hata hivyo kiungo huyo aliyeisaidia Ujerumani kutwaa Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil tayari amewasiliana na mwanasheria wake na wapo katika mpango wa kuishitaki kampuni iliyotengeneza mdoli huo, licha ya kuwa kampuni hiyo imekana kutengeneza mdoli huyo kwa kumfananisha na kiungo huyo na kwa upande wa jina wanasema ‘Bastian’ ni jina ambalo linatumika sana Ujerumani na hawajamlenga Bastian Schweinsteiger.
Bastian-Schweinsteiger-lookalike-Nazi-doll-named-Bastian (2)


Klabu ya Manchester City ya Uingereza ambayo usiku wa October 21 ilicheza mechi dhidi ya klabu ya Sevilla katika uwanja wake wa nyumbani wa Etihad. Kabla ya kuanza kwa mchezo huo ambao klabu ya Manchester City iliibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Sevilla kuna tukio lilijitokeza ambalo huenda litaigharimu Man City.
Usiku wa mechi hiyo kabla ya kuanza kwa mchezo wakati wimbo wa UEFA unaimbwa mashabiki wa klabu ya Man City walizomea wimbo huo, hivyo  tukio hilo lazima Man City watapigwa faini kutoka kwa shirikisho la soka barani Ulaya. Man City inatajwa kupigwa faini ila bado haijajulikana kama itatozwa kiwango cha kawaida au zaidi.


Kama ambavyo katika mitandao ya kijamii watu mbalimbali hupenda kuweka TBT pichaz zao siku ya Alhamisi na kujikumbushia wapi walipotokea. Kama kawaida mtu wangu wa nguvu huwa si ruhusu upitwe na kitu, nakusogezea karibu yako TBT pichaz za kocha wa sasa wa FC Barcelona Luis Enrique, kocha wa FC Bayern Munich  Pep Guardiola, kocha wa Man United Louis van Gaal na kocha wa Chelsea Jose Mourinho.
10a82c20-7d25-402a-bdc9-33f31283b3d7-1020x612
Jose Mourinho na Louis van Gaal
Van-Gaal-Mourinho
Louis van Gaal na Jose Mourinho wakati wapo FC Barcelona wakiwa sehemu ya benchi la ufundi la FC Barcelona
Pep player
Pep Guardiola enzi hizo akiwa mchezaji na nahodha wa FC Barcelona
1430896976_extras_noticia_foton_7_1
Kocha wa FC Barcelona Luis Enrique na kocha wa FC Bayern Munich Pep Guardiola enzi hizo wakiwa katika klabu ya FC Barcelona
CCkGME1WgAAgvEg
Pep Guardiola akiwa na Jose Mourinho enzi hizo FC Barcelona


Christian Benteke mazoeziniWachezaji wa Liverpool wakijifua tayari kwa mtanange wao wa Europa LeagueMeneja mpya KloppKlopp na Viongozi wake wasaidiziJurgen KloppKila kitu kinawezekana kwenye mpira.



Katibu wa Kamati ya Taifa Stars, Teddy Mapunda leo amefanya makutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Karume, ambapo ametumia nafasi hiyo kutangaza namba za simu za uchangiaji kwa Watanzania kwa ajili ya timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Akiongea na waandishi wa habari, Teddy amesema watanzania wanaweza kuichangia Taifa Stars kiasi chochote cha fedha kuanzia shilingi mia moja (TZS 100) kwenda namba 0654-888868 (Tigo Pesa) na 0789-530668 (Airtel Money) ambazo zitatumika kwa ajili ya motisha kwa wachezaji, uhamasishaji/masoko na maboresho ya kambi za ndani na nje ya nchi.

Aidha Teddy amesema Kamati ya Taifa Stars inaandaa utaratibu kwa ajili ya washabiki watakaotaka kusafiri kuelekea nchini Algeria katika mchezo wa marudiano, waweze kuchangia gharama za usafiri ili waweze kwenda kuipa sapoti Stars katika mchezo wa marudaiano Novemba 17, 2015.

“KamatI inaendelea na mchakato wa kukamilisha suala la kambi ya Taifa Stars, na mpaka sasa tunasubiri majibu kutoka katika vyama vya soka vya vya nchi tunazotaka kuweka kambi ambazo ni Afrika Kusini, Dubai na Oman kabla ya kutangaza rasmi kambi itakapokuwa” Alisema Teddy.

Kamati inawaomba watanzania, wadau, washabiki na wapenzi wa mpira miguu nchini kuichangia timu ya Taifa kupitia namba zilizotolewa na pia kujitokeza kwa wingi kuujaza uwanja wa Taifa siku ya mchezo wa tarehe 14 Novemba, 2015


MASTAA wa zamani wa Manchester United, Paul Scholes na Rio Ferdinand, wamesikitishwa na jinsi Timu yao ilivyocheza huko Moscow Jumatano Usiku na kutoka Sare 1-1 na CSKA Moscow katika Mechi ya Kundi B la UEFA CHAMPIONS.
Katika Mechi hiyo, Man United walicheza ovyo Kipindi cha Kwanza na kufungwa Bao la Penati lakini Kipindi cha Pili Man United walizinduka na kusawazisha kwa Bao la Chipukizi Anthony Martial.
Scholes na Rio, wakiwa Wachambuzi wa Mechi hiyo kwenye TV ya BT Sport huko England, walisikitishwa na uchezaji wa Man United na Scholes kutaja kasoro za Kepteni wao Wayne Rooney ambae alidorora kabisa.

Katika Mechi hiyo Rooney alicheza kama Sentafowadi na pembeni kushoto alicheza Martial na kulia Jesse Lingard.
Scholes alieleza: "Rooney si mzuri kama hana Watu wenye kasi wanaomzunguka. Hata mie nilikuwa hivyo!"
Hata hivyo, Scholes alikiri kupata Sare kwenye Uwanja wenye baridi kali mno huko Moscow si matokeo mabaya.
Nae Rio Ferdinand alisema; "Tulipatwa na wasiwasi jinsi Man United walivyocheza Kipindi cha Kwanza. Walipooza, hawakuwa na spidi wala mashambulizi!"
Lakini Rio alisifia uchezaji wa Kipindi cha Pili ambapo Wachezaji waliongeza bidii, spidi ikaonekana na kuingia kwenye boksi mara kwa mara.
Wachambuzi hao walibainisha kuwa kwenye Mechi hiyo Rooney aligusa Mpira mara 40 tu ukilinganisha na mara 47 za Fellaini alieingizwa Kipindi cha Pili.
Mechi ijayo kwa Man United ni huki Old Trafford hapo Jumapili Oktoba 25 ikiwa ni


UEFA EUROPA LIGI Usiku huu ina Mechi zake za 3 za Makundi yake na Klabu za England, Liverpool na Tottenham, zipo dimbani.
Liverpool wapo kwao Anfield kucheza na Rubin Kazan hii ikiwa ni Mechi yao ya kwanza kabisa chini ya Menejqa mpya Jurgen Klopp hapo Anfield.
Klopp alianza kazi yake na Liverpool Wikendi iliyopita alipopata Sare huko White Hart Lane walipocheza na Tottenham katika Mechi ya Ligi Kuu England.
Kwenye Kundi B, Liverpool wametoka Sare Mechi zao 2 za kwanza.

Tottenham wao wako Kundi J na wameshinda Mechi 1 na Sare 1 na Leo wako Ugenini huko Belgium kwa kucheza na RSC Anderlecht.
UEFA EUROPA LEAGUE
RATIBA
Alhamisi Oktoba 22
GROUP A

2205 Fenerbahçe v Ajax
2205 Molde v Celtic
 

GROUP B
2205 Bordeaux v FC Sion
2205 Liverpool v Rubin Kazan

GROUP C
1800 FK Qabala v Bor Dortmd
2205 PAOK Salonika v FK Krasnodar

GROUP D
2205 FC Midtjylland v Napoli
2205 Legia Warsaw v Club Brugge

GROUP E
2205 SK Rapid Vienna v Viktoria Plzen
2205 Villarreal v Dinamo Minsk

GROUP F
2205 Slovan Liberec v FC Groningen
2205 Sporting Braga v Marseille

GROUP G
2000 Dnipro Dnipropetrovsk v St Etienne
2000 Lazio v Rosenborg

GROUP H
2000 Lokomotiv Moscow v Besiktas
2000 Sporting v Skenderbeu Korce

GROUP I
2000 FC Basel v Belenenses
2000 Fiorentina v Lech Poznan

GROUP J
2000 Monaco v FK Qarabag
2000 Anderlecht v Tottenham

GROUP K
2000 Apoel Nic v Asteras Tripolis
2000 Schalke v Sparta Prague

GROUP L
2000 AZ Alkmaar v FC Augsburg 

2000 Partizan Belgrade v Ath Bilbao

waliotembelea blog