Meneja
wa zamani wa Manchester United na Uholanzi Louis van Gaal amesema
amestaafu kazi ya ukufunzi baada ya miaka 26 katika taaluma yake. Van
Gaal, 65, hajafanya kazi uwanjani tangu alipopigwa kalamu na United saa
chache baada ya kushinda kombe la FA mwezi Mei 2016.
Akiongea na jarida la Telegraaf la nchini Uholanzi Van Gaal amesema ”Mambo
mengi yametokea kwa familia yangu, unakuwa binadamu kwa mara nyingine
kwa kukiri ukweli, kwa fikra zangu nilidhani nitastaafu, nikafikiria pia
itakuwa ni mapumziko ya muda, lakini kwa hivi sasa sidhani kama
nitarudi kwenye kazi ya ukocha,” Van Gaal
Van
alitangaza uamuzi wake siku ya Jumatatu baada ya kupata tuzo ku katika
taaluma yake kutoka kwa serikali ya Uholanzi kwa mchango wake katika
soka. Alisema shida za kifamilia ndizo zilichangia uamuzi wake huo, huku
gazeti la De Telegraaf likisema uamuzi wake ulichangiwa na kifo cha
mkwe wake mwezi Disemba.
Van Gaal
pia alikuwa kocha wa klabu ya Ajax, Barcelona, Bayern Munich, AZ na
Manchester United ambayo ilikuwa club yake ya mwisho kuifundisha msimu
uliopita. Mbali na kuwa kocha, Van Gaal pia amewahi kuzichezea club za
Ajax, Royal Antwep, Telstar, Sparta Rotterdam na AZ.
Raia huyo
muholanzi ameweka wazi kuwa alikataa nafasi nzuri za kuendeleza taaluma
yake kwa kukataa kazi mataifa ya Mashariki ya Mbali.