Wednesday, October 14, 2015

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma na kuvikwa skafu tayari kuongoza maadhimisho ya Kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu2015 na kumbukumbu ya miaka 16 ya kifo cha  Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.Kauli mbiu ya mwaka huu ni “ Tumia haki yako ya kidemokrasia kupiga kura katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

 Baadhi ya wakazi wa mji wa Dodoma waliohudhuria sherehe za kilele cha maadhimisho yam bio za mwenge wa Uhuru.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika jukwaa malum akipigiwa wimbo wa taifa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma kuongoza maadhimisho yam bio za mwenge.



Licha ya kuwa ilishafuzu kucheza Euro 2016 nchini Ufaransa, Ubelgiji imeendelea vipigo katika mechi za kuwania kufuzu kwa kuichapa Israel 3-1.

Ushindi huo wa mabao ya Eden Hazard na De Bruyne umeifanya Ubeigiji kushika namba moja kwa viwango vya Fifa dunia.
Ubelgiji imeiangusha Argentina na Ujerumani zilizokuwa zinashika nafasi ya pili na tatu.
Ubelgiji ilikuwa katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 1387, lakini sasa ndiyo kinara duniani.
Belgium: Mignolet, Vertonghen, Lombaerts, Kompany (Meunier 58), Alderweireld, Nainggolan, Fellaini (Witsel 65), Hazard, De Bruyne, Mertens, Romelu Lukaku (Origi 65).
Subs Not Used: Sels, Bakkali, Boyata, Kums, Depoitre, Cavanda, Chadli, Jordan Lukaku, Gillet.
Booked: De Bruyne,Lombaerts.
Goals: Mertens 64,De Bruyne 78,Hazard 84.
Israel: Marciano,Ben Haroush,Tibi, Ben Haim I, Dgani, Kayal (Damari 66),Yeini (Vermouth 77), Peretz, Ben Haim II (Reikan 59), Hemed, Zahavi.
Subs Not Used: Levy, Davidadze, Elkayami, Melikson, Dabour, Tzedek, Kahat, Haimov.
Booked: Reikan.
Goal: Hemed 88.
Ref: Tasos Sidiropoulos (Greece












Beki wa kimataifa wa Ufaransa Patrice Evra ambaye amewahi kuitumikia klabu ya Manchester United ya Uingereza kwa kipindi cha miaka nane, October 14 amezungumzia uamuzi wa Man United kumuacha aondoke timu hiyo na kutimkia klabu ya Juventus ya Italia.
Patrice Evra ambaye amedumu katika klabu ya Manchester United kwa kipindi cha miaka nane, hakufurahishwa na uamuzi wa Man United kumuuza kwenda Juventus ya Italia kwa dau la pound milioni 1.5. Licha ya kushinda mataji kadhaa akiwa katika klabu yake mpya ya Juventus, Evra anasema uhamisho wa yeye kuondoka Man United ulilazimishwa na wala haukuwa uamuzi wake.
BERLIN, GERMANY - JUNE 06: Patrice Evra of Juventus in action during the UEFA Champions League Final between Juventus and FC Barcelona at Olympiastadion on June 6, 2015 in Berlin, Germany. (Photo by Shaun Botterill/Getty Images)
“Bado ni ngumu kuzungumzia kuondoka kwangu Man United lakini siku moja nitakapokuwa nimestaafu soka nitakuwa tayari kuzungumzia hili kwa kina. Nilikuja Turin kwa ajili ya familia yangu sababu Man United waliingiza kifungu ambacho kilibadili kila kitu, kitu ambacho kilinikera”>>> Evra
“Lakini sijutii uhamisho huu ambao mwisho wake umekuja kuwa na mrejesho zaidi ya chanya kwangu, najisikia furaha Serie A licha ya kuwa uhamisho huu ulikuwa wa bahati mbaya kuliko chaguo langu. Kwa sasa malengo yangu ni kuhakikisha nashinda mataji Juventus na timu yangu ya taifa ya Ufaransa”>>> Evra
MUNICH, GERMANY - APRIL 09: Patrice Evra of Manchester United celebrates his goal during the UEFA Champions League Quarter Final second leg match between FC Bayern Muenchen and Manchester United at Allianz Arena on April 9, 2014 in Munich, Germany. (Photo by Shaun Botterill/Getty Images)
Beki huyo wa zamani wa klabu ya Manchester United ya Uingereza, akiwa na Man United amecheza jumla ya mechi 379 na kutwaa mataji matano ya Ligi Kuu Uingereza, moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya na mataji mengine tisa hiyo ni kwa muda wa miaka nane aliyodumu katika klabu hiyo.

waliotembelea blog