Wednesday, October 14, 2015

Beki wa kimataifa wa Ufaransa Patrice Evra ambaye amewahi kuitumikia klabu ya Manchester United ya Uingereza kwa kipindi cha miaka nane, October 14 amezungumzia uamuzi wa Man United kumuacha aondoke timu hiyo na kutimkia klabu ya Juventus ya Italia.
Patrice Evra ambaye amedumu katika klabu ya Manchester United kwa kipindi cha miaka nane, hakufurahishwa na uamuzi wa Man United kumuuza kwenda Juventus ya Italia kwa dau la pound milioni 1.5. Licha ya kushinda mataji kadhaa akiwa katika klabu yake mpya ya Juventus, Evra anasema uhamisho wa yeye kuondoka Man United ulilazimishwa na wala haukuwa uamuzi wake.
BERLIN, GERMANY - JUNE 06: Patrice Evra of Juventus in action during the UEFA Champions League Final between Juventus and FC Barcelona at Olympiastadion on June 6, 2015 in Berlin, Germany. (Photo by Shaun Botterill/Getty Images)
“Bado ni ngumu kuzungumzia kuondoka kwangu Man United lakini siku moja nitakapokuwa nimestaafu soka nitakuwa tayari kuzungumzia hili kwa kina. Nilikuja Turin kwa ajili ya familia yangu sababu Man United waliingiza kifungu ambacho kilibadili kila kitu, kitu ambacho kilinikera”>>> Evra
“Lakini sijutii uhamisho huu ambao mwisho wake umekuja kuwa na mrejesho zaidi ya chanya kwangu, najisikia furaha Serie A licha ya kuwa uhamisho huu ulikuwa wa bahati mbaya kuliko chaguo langu. Kwa sasa malengo yangu ni kuhakikisha nashinda mataji Juventus na timu yangu ya taifa ya Ufaransa”>>> Evra
MUNICH, GERMANY - APRIL 09: Patrice Evra of Manchester United celebrates his goal during the UEFA Champions League Quarter Final second leg match between FC Bayern Muenchen and Manchester United at Allianz Arena on April 9, 2014 in Munich, Germany. (Photo by Shaun Botterill/Getty Images)
Beki huyo wa zamani wa klabu ya Manchester United ya Uingereza, akiwa na Man United amecheza jumla ya mechi 379 na kutwaa mataji matano ya Ligi Kuu Uingereza, moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya na mataji mengine tisa hiyo ni kwa muda wa miaka nane aliyodumu katika klabu hiyo.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog