Mabingwa Watetezi wa England, Manchester United, walishinda Bao 2-0 na kujikongoja Nafasi moja juu na sasa kukamata Nafasi ya 6.
Hadi Mapumziko Mabao yalikuwa 0-0.
Kipindi cha Pili, katika Dakika ya 62, Robin van Persie aliipatia Man United Bao la Kwanza kwa Penati iliyotolewa na Refa Michael Oliver baada Patrice Evra kuangushwa ndani ya Boksi na Marouanne Chamakh.
Bao la Pili lilifungwa Dakika ya 68 kifundi na Wayne Rooney baada ya kupokea pasi safi toka kwa Evra.
Mechi inayofuata kwa Man United ni huko Ugiriki hapo Jumanne Usiku watakapocheza na Olympiacos katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONS.Van Persie akishangilia...
Wakati Rooney anataka kupiga kona alirushiwa shilingi na hapa akimpatia Mwamuzi wa mchezo huoR