Thursday, January 30, 2014

  

 
Hii ni nyumba aliyokuwa anaishi Babu enzi za kale



.

 Mitambo

Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha  Adam Kigoma Malima alifanya ziara ya siku mbili mkoani Kagera na kukagua miradi ya ujenzi wa vituo vya umoja wa  ushuru na forodha (One Stop Border Post)Rusumo na Mtukula  na ujenzi  wa daraja la Kimataifa la Rusumo kati ya Tanzania na Rwanda.
Naibu Waziri Adam Malima  alifanya ziara hiyo mkoani Kagera kuanzia tarehe 29 -30 Januari, 2014 na kutembelea mpaka wa Rusumo Wilayani Ngara na Mtukula Wilayani Missenyi pia kuongea na wananchi na wafanyabiashara na kutatua kero zao.
Katika mradi wa ujenzi  wa Kituo cha pamoja cha ushuru na forodha  Rusumo mpakani mwa Tanzania na Rwanda Naibu Waziri alikagua ujenzi unavyoendele ikiwa ni pamoja ujenzi wa daraja la kimataifa la Rusumo ambalo ni la kisasa.
Daraja hilo llitakalokuwa na urefu wa kilometa 2 na upana wa meta 10.5 linajengwa kwa gharama ya Yeni za Kijapani blioni 2.9 na kila nchi (Tanzania na Rwanda) zinachangia fedha za Japani  Yeni bilioni 1.4 kila nchi mpaka daraja kukamilika ujenzi wake.
Kwa upande wa Tanzania mradi wote (Kituo cha pamoja cha ushuru na forodha na daraja)  umefadhiliwa na Serikali ya Japani kwa gharama  ya fedha za Japani Yeni bilioni 1.8 na  unajengwa na Kampuni ya Kijapani iitwayo DAIHO COOPERATION abapo ujenzi wake umefikia  asilimia 68.
Baada ya kukagua na kujionea ujenzi unavyoendelea Naibu Waziri Malima aliwahakikishia wananachi na wafanyabiashara kuwa serikali itahakikisha mradi huo unatekelezwa na kukamilika kwa muda uliopangwa ambapo ulianza 2 Machi, 2012 na unatarajia kukamilika 15 Novemba, 2014
Naibu Waziri  Malima aliwahakikishia wananchi na wafanyabiashara katika mpaka huo kuwa mara baada ya ujenzi wa Kituo cha pamoja cha ushuru na forodha kumilika na daraja la kimataifa kukamilika mpaka wa Rusumo  utaanzan kufanya kazi kwa masaa 24 kutoka 16 ya sasa.
Aidha akisikiliza kero za wananachi wa Rusumo waliolalamika kuhusu huduma ya maji na umeme katika mpaka huo, Naibu Waziri Malima alisema ili kituo cha pamoja cha ushuru na forodha  kifanye kazi masaa 24 ni lazima kuwepo na umeme wa uhakika katika eneo husika  na kufikia muda wa mradi kukabidhiwa kila kitu kinachohitajika kitakuwa tayari kimetekelezwa na serikali.
Katika Wilaya ya Missenyi Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima alitembelea na kukagua Kituo cha pamoja cha ushuru na forodha Mtukula kwenye mpaka wa Tanzania na Uganda ambacho kimekamilika ujenzi wake kwa asilimia 100 na kuanza kutoa huduma..
Kero kubwa iliyokuwa inaleta kelele nyingi katika mpaka huo ilikuwa ni umeme ambapo Naibu Waziri Malima alihakikishiwa na Meneja wa TANESCO mkoa wa Kagera Bw. Martin Maduro kuwa kufikia  tarehe 28/02/2014 umeme utakuwa tayari unawaka katika mpaka huo na mafundi wanaendelea na kazi.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri Malima aliwaagiza Mamlaka ya Mapato nchini kuwajibika kwa uwazi mfano kutoza ushuru katika bidhaa mbalimbali ili kuondoa malalamiko ya wananchi  na wafanyabiashara  ambao ndiyo wateja wao au walipa kodi.
Wafanyabiashara wa Mazao walilalamika kuhusu vibali vya kusafirisha mazao kuwa vinapatikana Wizarani Dar es Salaam tu jambo ambalo linawafanya kuongeza gharama katika mazao hayo bila sababu na kumwomba Naibu Waziri Malima kuwa  vibali hivyo vipatikane katika Wilaya zao.
Akijibu suala hilo Naibu Waziri Malima alisema kuwa wizara Fedha  ikishirikiana na Wizara ya Biashara na Viwanda, na Wizara ya Kilimo wataweka utaratibu mzuri wa kuhakikisha  vibali hivyo vinapatikana kilahisi ili kupunguza gharama na usumbufu kwa wafanyabiashara mipakani kwa nchi nzima.
Naibu Waziri Malima alimalizia kwa kuwahawahakikishia wafanyakazi wa mipakani katika idara zote zinazohusika katika kituo cha pamoja cha ushuru na forodha (One Stop Border Post) kuwa serikali imeanza  kutafuta ufumbuzi wa kero ya makazi yao katika mipaka ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa masaa 24 bila kuhathili utoaji wa huduma katika mipaka hiyo.
Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiwa na mchumba wake.
Chanzo makini kimepenyeza habari kuwa, safari za mara kwa mara za Shilole nchini Uingereza zimekuwa zikisababishwa na mchumba huyo wa Kizungu ambaye huwa anamuita kufurahia penzi lao pamoja na kumtafutia shoo mbalimbali.
“Ukweli ni kwamba Shilole ana mchumba wa Kizungu na walikutana kwenye shoo ya mara ya kwanza aliyoenda kufanya nchini Uingereza na hivi karibuni ataenda tena na amealikwa na huyo mchumba wake,” kilisema chanzo hicho.
Gazeti hili limekuwa la kwanza kunasa picha kadhaa za Shilole akiwa katika mapozi tofauti ya kimahaba na Mzungu huyo.
Baada ya chanzo hicho kumwaga ‘upupu’ huo, mapaparazi wetu walimtafuta Shilole ili aweze kufunguka ambapo bila kuumauma maneno, alikiri kuwa amepata mchumba huyo aliyemtambulisha kwa jina la Ankar.
Akizidi kumwaga data za boifrendi wake huyo, Shilole alisema awali walikutana kwenye moja ya shoo zake nchini humo ndipo urafiki ulipoota mizizi na kufikia hatua ya kuwa wapenzi.
“Kweli nina mchumba Mzungu ambaye ni raia wa Uingereza, nilipokuwa napataka nimefika, sipindui tena. Unajua muziki wangu na mauno yangu yanawavutia sana watu, siku ya kwanza aliniona kwenye shoo akanipenda ndipo tukaanzisha urafiki.
“Hivi karibuni nina safari ya kwenda nchini humo kwa mwaliko maalum alionipa, nitaenda peke yangu kwani safari nyingine zote zilizopita nilikuwa naenda na watu,” alisema Shilole.

 MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho ameponda aina ya uchezaji wa timu ya West Ham United na kudai kuwa ni wa karne ya 19 kufuatia timu yake kutoa sare ya bila ya kufungana katika Uwanja wa Stamford Bridge. Chelsea walifanya kila wanaloweza kuhakikisha wanapenya ngome ya West Ham wanaonolewa na Sam Allardyce lakini walishindwa na kujikuta wakigaana alama hivy kushindwa kuwafikia Arsenal ambao wameshuka mpaka nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza. 

 Akihojiwa Mourinho amesema kuwa mchezo waliocheza West Ham wa kizamani na haufanani na timu iliyokuwa katika Ligi Kuu. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa ni ngumu kucheza mechi wakati timu moja pekee ndio inayotaka kucheza huku nyingine ikifanya kazi ya kuzuia pekee.

MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho ameponda aina ya uchezaji wa timu ya West Ham United na kudai kuwa ni wa karne ya 19 kufuatia timu yake kutoa sare ya bila ya kufungana katika Uwanja wa Stamford Bridge. Chelsea walifanya kila wanaloweza kuhakikisha wanapenya ngome ya West Ham wanaonolewa na Sam Allardyce lakini walishindwa na kujikuta wakigaana alama hivy kushindwa kuwafikia Arsenal ambao wameshuka mpaka nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza.

 





Julian Draxler: The €30million man?Welcome with open arms: Newcastle are in the chase for Clement Grenier Seal the deal? Yevhen Konoplyanka is Liverpool's chief targetDani Osvaldo: Is the Saints striker on his way to Juventus?Mirko Vucinic: is he Gunner join Arsenal?
Is Kurt Zouma heading to Chelsea?













 

 

 

 

waliotembelea blog