Friday, March 13, 2015

Ajali hii imetokea leo asubuhi eneo LA airport Arusha ambapo basi la Arusha express likielekea MBEYA kugongana na Lori lkn hakuna aliyepoteza Maisha Ingawa watu Wamejeruhiwa na Kupelekwa hospitali ya Mkoa Mt Meru...
Ajali hii imetokea baada ya dereva wa basi kujaribu ku-overtake na kukutana na lori mbele yake. Habari zinasema kuwa  abiria wa Lori ndiyo wameumia na kukimbizwa Hospitali


 


RATIBA:
Jumamosi Machi 14

15:45 Crystal Palace vs QPR
18:00 Arsenal vs West Ham
18:00 Leicester vs Hull
18:00 Sunderland vs Aston Villa
18:00 West Brom vs Stoke
20:30 Burnley vs Man City
Jumapili Machi 15
16:30 Chelsea vs Southampton
19:00 Everton vs Newcastle
19:00 Man United vs Tottenham
 

Jumatatu Machi 16
23:00 Swansea vs Liverpool


WASHINDI WA LIGI KUU ENGLAND TANGU 1992-1993 MPAKA MSIMU HUU 2013-2014
In 2014-15 Premier League is the 23rd season of the English Premier League. The 22 Premier League champions are:
  SEASON  CHAMPIONS RUNNERS-UP
1992-93 Manchester United Aston Villa
1993-94 Manchester United Blackburn Rovers
1994-95 Blackburn Rovers Manchester United
1995-96 Manchester United Newcastle United
1996-97 Manchester United Newcastle United
1997-98 Arsenal Manchester United
1998-99 Manchester United Arsenal
1999-2000 Manchester United Arsenal
2000-01 Manchester United Arsenal
2001-02 Arsenal Liverpool
2002-03 Manchester United Arsenal
2003-04 Arsenal Chelsea
2004-05 Chelsea Arsenal
2005-06 Chelsea Manchester United
2006-07 Manchester United Chelsea
2007-08 Manchester United Chelsea
2008-09 Manchester United Liverpool
2009-10 Chelsea Manchester United
2010-11 Manchester United Chelsea
2011-12 Manchester City Manchester United
2012-13 Manchester United Manchester City
2013-14 Manchester City Liverpool
Chelsea itatwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England Msimu huu kwa mujibu wa Meneja wao makeke Jose Mourinho.
Juzi Jumatano Chelsea ilitupwa nje ya UEFA CHAMPIONS LIGI na Paris St-Germain lakini kwenye Ligi Kuu England wao ni Vinara wa Ligi wakiwa Pointi 5 mbele ya Timu ya Pili Manchester City ambao ni Mabinngwa Watetezi waliocheza Mechi 1 zaidi. Leo, akiongea na Wanahabari kwa ajili ya Mechi yao ya Ligi yaJumapili dhidi ya Southampton itakayochezwa Uwanjani Stamford Bridge, Jose Mourinho amesema: "Watu waliotolewa Jumatano ndio hao hao ambao wako juu kwenye Ligi tangu ya Siku ya kwanza. Ndio hao hao waliotwaa Capital One Cup na ndio hao hao watatwaa Ligi Kuu!"Diego akiwa chini ya ulinzi mkali wa beki David Luiz.
Soma Zaidi Hapa »



MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha kuwa Alex Oxlade-Chemberlain atakaa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki nne kutokana na majeruhi ya msuli wa paja. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 alipata majeruhi hayo katika mchezo wa Kombe la FA Jumatatu iliyopita ambao Arsenal iliifunga Manchester United kwa mabao 2-1. Sasa Chamberlain anatarajiwa kukosa mechi za Ligi Kuu kati ya timu yake dhidi ya West Ham United, Newcastle United na Liverpool pamoja na mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Monaco wiki ijayo. Wenger amesema ni vigumu kutabiri muda gani haswa Chamberlain atakaa nje lakini anadhani itakuwa ni kati ya wiki tatu hadi nne. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa litakuwa jambo la kuhuzunisha kwa mchezaji huyo lakini msimu huu amecheza mechi nyingi na kuonyesha umuhimu wake.
Soma Zaidi Hapa »


KIINGILIO cha chini katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika baina ya Yanga SC na Platinum FC ya Zimbabwe kitakuwa na Sh. 5,000 kwa jukwaa la viti vya rangi bluu na kijaniYanga wataikaribisha Platinum FC ya Zimbabwe katika mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, jumapili.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro alisema kwamba, katika jukwaa la viti vya Rangi Chungwa itakuwa Sh, 7000, VIP C Sh. 15,000, VIP B Sh. 20,000, na VIP A Sh 30,000.
Muro amesema tiketi zitaanza kuuzwa Jumamosi Saa 2:00 asubuhi katika vituo vya Karume (Ofisi za TFF), Mgahawa wa Steers (Posta Mpya), Oilcom (Buguruni), BigBon (Kariakoo), Olicom (Ubungo), Dar Live (Mbagala), Uwanja wa Uhuru, Kivukoni (Ferry) na Makumbusho (kituo cha mabasi).

Aidha, amesema magari yenye vibali maalum ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia ndani ya Uwanja siku hiyo.
Yanga SC imefika hatua hii baada ya kuitoa BDF XI ya Botswana, wakati Platinum iliing’oa Sofapaka ya Kenya.
Wakati huo huo: Kikosi cha Platinum kilichotarajiwa kuwasili Saa 2:00 usiku wa leo, hakijawasili na wenyeji wao, Yanga SC wameshangaa kwa sababu hawana taarifa nyingine.
BEKI wa Paris Saint-Germain, David Luiz amewaomba radhi Chelsea baada ya kushangilia bao alilofunga ambalo lilisaidia kuing’oa timu yake hiyo ya zamani katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Luiz alifunga bao la kusawazisha katika dakika ya 86 ya mchezo huo na kusababisha mchezo huo kwenda katika muda wa nyongeza. Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 27 amesema anaomba radhi kwa kuonyesha hisia zake kwani ilikuwa vigumu kujizuia kutokana na furaha aliyokuwa nayo. PSG ilisonga mbele katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo kwa faida ya bao la ugenini baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 katika mchezo huo. Luiz amewahi kuichezea Chelsea mechi 143 katika mashindano yote na kufunga mabao 12 kabla ya kuhamia PSG kwa kitita cha paundi milioni 40 Juni mwaka jana.


TIMU ya Polisi Morogoro imekatisha mkataba na kocha wake Mkuu, Mohamed Adolph Rishaard kutokana na timu hiyo kucheza chini ya kiwango na kupoteza michezo kwenye ligi Kuu..
Akizungumza kwa njia ya simu Mwenyekiti wa klabu ya Polisi Moro, Zuberi Chambera alisema kuwa kocha, Mohamed Adolph Richard amesitisha mkataba naye wa kuifundisha timu kutokana na kufanya vibaya na kusema maamuzi hayo yakifikiwa na kikao cha kamati ya utendaji ya timu.
“Ni kweli kocha wetu Mohamed Adolph Rishard amesimamishwa kufundisha kutokana na sababu zilizotolewa na kupitishwa na kamati tendaji ni baada ya kucheza chini ya kiwango tofauti na makubaliano yaliyofikiwa wakati wa mkataba wetu”, alisema Chembera.
Polisi Moro imepoteza michezo minne, imetoka sare nane na kushinda michezo minne ya ligi kuu Tanzania bara na sasa timu ipo itanolewa na kocha msaidizi, John Tamba wakati wakisaka kocha mkuu mwenye sifa za kufundisha.
Naye Mohamed Rishard alisema kuwa kusitishiwa mkataba wake amelipokea kwa mikono miwili kutokana na timu kufanya vibaya kwani lilikuwepo moja ya kipengele kwenye mkataba kilitamka wazi endapo timu ingepoteza michezo mitatu kamati itamwita na kumhoji na wametekeleza kipengeleza
1
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe Benson Mpesya juu ya madhara makubwa ya mali na maisha ya watu wakati wa ziara maalum ya kutoa pole kwa wahanga wa mvua iliyoandamana na mawe na kusababisha upotevu wa maisha ya watu na uharibifu mkubwa wa mali katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.

 6
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na  familia zilizoathirika na mvua kali iliyoandamana na mawe na kusababisha upotevu wa maisha ya watu na uharibifu mkubwa wa mali katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa
7
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua baadhi ya makazi ya dharura kwa  familia zilizoathirika na mvua kali iliyoandamana na mawe na kusababisha upotevu wa maisha ya watu na uharibifu mkubwa wa mali katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.
2
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pole kwa familia zilizoathirika na mvua kali iliyoandamana na mawe na kusababisha upotevu wa maisha ya watu na uharibifu mkubwa wa mali katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.
8 9
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwapa mkono wa pole waalimu wa shule ya msingi ya Mwakata, wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga, ambao pia ni waathirika wa  mvua kali iliyoandamana na mawe na kusababisha upotevu wa maisha ya watu na uharibifu mkubwa wa mali katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.
10
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia mamia ya wananchi baada ya kutembelea na kuzifariji  familia zilizoathirika na mvua kali iliyoandamana na mawe na kusababisha upotevu wa maisha ya watu na uharibifu mkubwa wa mali katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.
11 12 13

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Alhamisi, Machi 12, 2015, amefanya ziara maalum ya kutoa pole kwa wahanga wa mvua iliyoandamana na mawe na kusababisha upotevu wa maisha ya watu na uharibifu mkubwa wa mali katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.
Rais Kikwete amewasili mjini Kahama kiasi cha saa nane mchana baada ya ndege yake kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Mgodi wa Buzwagi na kwa muda wa kiasi cha saa tatu ametembelea familia ambazo zimepata madhara makubwa zaidi kutokana na mvua hiyo iliyonyesha kwa kiasi cha saa moja tu kuanzia saa nne usiku Machi 3, mwaka huu, 2015 na kuambana na upepo mkali na mawe.
Watu 47 walipoteza maisha, 112 wakaumia, nyumba 657 zikabomolewa ama kuharibiwa na kaya 468 kuathirika katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata na tokea siku ya maafa, Serikali imetoa huduma za dharura za chakula, sehemu za kulala, huduma za afya na huduma nyingine muhimu kwa binadamu.
Baada ya kupatiwa maelezo ya kina na uongozi wa Mkoa wa Shinyanga chini ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Ali N. Lufunga, Rais Kikwete ameanzia ziara yake katika Kijiji cha Maghuhumwa, nyumbani kwa Bwana Masemba Maburi, ambaye alipoteza watoto watano katika maafa hayo. Rais Kikwete ametoa pole kwa wafiwa na kuzungumza na wananchi waliokuwepo kwenye msiba.
Bwana Maburi ambaye sasa anaishi katika nyumba ya jirani pamoja na familia yake na familia nyingine tatu amemweleza Rais Kikwete jinsi nyumba mbili ambako watoto hao na mama yao walipokuwa wamelala zilivyoanguka na mama huyo akalazimika kukimbilia nje kwa nia ya kutafuta msaada lakini watoto wakazidiwa na kupoteza maisha.
“Sijawahi kuona mvua kubwa, kali na yenye upepo mkali kiasi kile katika maisha yangu. Mvua ilianza saa nne usiku na ikanyesha kwa muda mfupi sana, nyumba zikaanguka ama kubomolewa. Jameni tusaidie kwa sababu tumekwazika,”Bwana Maburi amemwambia Rais Kikwete.
Baada ya kutoka katika Kijiji cha Maghuhumwa, Rais Kikwete amekwenda katika Kijiji cha Nhumbi ambako amempa pole Bwana Zacharia Limbe na familia yake ambayo ilipoteza wajukuu wanne katika maafa hayo ya mwanzoni mwa mwezi huu.
Akiwa nyumbani kwa Bwana Limbe, Rais Kikwete ametembea na kujionea makazi mapya ya dharura ya familia ambayo yamejengwa kwa msaada wa Serikali.
Baada ya kuondoka kwa Bwana Limbe, Rais Kikwete ametembelea eneo la makazi ya walimu wa Shule ya Msingi ya Mwakata, ambako walimu hao wamehifadhiwa katika fremu za maduka kutokana na athari za maafa hayo. Rais Kikwete amewapa pole walimu hao na kuwaambia: “Pole sana. Tuko pamoja. Tutaendelea kusaidiana kuona jinsi gani mnavyoweza kurejea katika maeneo yenu ya makazi ya kawaida.”


Meneja wa West Bromwich Albion Tony Pulis amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa mwezi Februari Ligi England Barclays Premier League ambaye alichaguliwa kukinoa Kikosi hicho  tangu Mwezi Januari mwaka huu 2015 na kuiongoza Timu hiyo pasipo kufungwa mwezi Februari.
Tony Pulis ameiongoza  West Brom na Mwezi jana Januari hakufungwa hata bao moja.
MICHEZO YA MWEZI FEBRUARI YA WEST BROM
Feb 8: Burnley 2-2 West Brom
Feb 11: West Brom 2-0 Swansea
Feb 21: Sunderland 0-0 West Brom
Feb 28: West Brom 1-0 Southampton

Straika wa West Brom Brown Ideye akishangilia walipoitandika Swansea City bao 2-0 mwezi huo Januari na hapa akishangilia na mwenzie Morrison.



Harry Kane mchezaji wa Spurs amechaguliwa kuwa mcezaji bora mwezi jana Februari ambaye kwa mwezi uliopita ameiwezesha Tottenham kufufuka na kuweza kupanda juu kwenye ligi Kuu England. Akizibamiza timu kadhaa kama Arsenal, na Akikunga bao waliponyukwa 3-2 na Liverpool huku wakitoka sare na West Ham ya 2-2.

Kane akishangilia bao baada ya kuwanyoosha Arsenal bao 2-1 walpocheza kwenye Uwanja wa Nyumbani White Hart Lane Feb. 7, 2015.


Zimbabwe wameondolewa kushiriki Kombe la Dunia ambalo Fainali zake zitafanyika huko Russia Mwaka 2018.
Kamati ya Nidhamu ya FIFA jana imewajulisha ZIFA, chama cha Soka Zimbabwe, kwamba hawataruhusiwa kucheza Mashindano hayo ambayo wao walipaswa kucheza Mechi za Mchujo za Bara la Afrika ambalo hutoa Nchi 5 zinazocheza Fainali.
Kupigwa marufuku huku kumetokana na Nchi hiyo kushindwa kulipa Deni lao kwa aliekuwa Kocha wao Jose Claudinei Georgini.

Kocha huyo alilalamika kwa FIFA kupitia Kamati ya Hadhi za Wachezaji ambayo iluamuru Kocha huyo ana haki ya kulipwa.
Hata hivyo ZIFA ilishindwa kulipa Deni na Kocha huyo kwenda Kamati ya Nidhamu ya FIFA ambayo Aprili 2013 iliamua kuipiga Faini ZIFA na kuipa Siku 60 kulipa Nusu ya Deni na kulimaliza lote baada ya Siku 120.

waliotembelea blog