Friday, March 13, 2015


TIMU ya Polisi Morogoro imekatisha mkataba na kocha wake Mkuu, Mohamed Adolph Rishaard kutokana na timu hiyo kucheza chini ya kiwango na kupoteza michezo kwenye ligi Kuu..
Akizungumza kwa njia ya simu Mwenyekiti wa klabu ya Polisi Moro, Zuberi Chambera alisema kuwa kocha, Mohamed Adolph Richard amesitisha mkataba naye wa kuifundisha timu kutokana na kufanya vibaya na kusema maamuzi hayo yakifikiwa na kikao cha kamati ya utendaji ya timu.
“Ni kweli kocha wetu Mohamed Adolph Rishard amesimamishwa kufundisha kutokana na sababu zilizotolewa na kupitishwa na kamati tendaji ni baada ya kucheza chini ya kiwango tofauti na makubaliano yaliyofikiwa wakati wa mkataba wetu”, alisema Chembera.
Polisi Moro imepoteza michezo minne, imetoka sare nane na kushinda michezo minne ya ligi kuu Tanzania bara na sasa timu ipo itanolewa na kocha msaidizi, John Tamba wakati wakisaka kocha mkuu mwenye sifa za kufundisha.
Naye Mohamed Rishard alisema kuwa kusitishiwa mkataba wake amelipokea kwa mikono miwili kutokana na timu kufanya vibaya kwani lilikuwepo moja ya kipengele kwenye mkataba kilitamka wazi endapo timu ingepoteza michezo mitatu kamati itamwita na kumhoji na wametekeleza kipengeleza

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog