Friday, March 13, 2015

Chelsea itatwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England Msimu huu kwa mujibu wa Meneja wao makeke Jose Mourinho.
Juzi Jumatano Chelsea ilitupwa nje ya UEFA CHAMPIONS LIGI na Paris St-Germain lakini kwenye Ligi Kuu England wao ni Vinara wa Ligi wakiwa Pointi 5 mbele ya Timu ya Pili Manchester City ambao ni Mabinngwa Watetezi waliocheza Mechi 1 zaidi. Leo, akiongea na Wanahabari kwa ajili ya Mechi yao ya Ligi yaJumapili dhidi ya Southampton itakayochezwa Uwanjani Stamford Bridge, Jose Mourinho amesema: "Watu waliotolewa Jumatano ndio hao hao ambao wako juu kwenye Ligi tangu ya Siku ya kwanza. Ndio hao hao waliotwaa Capital One Cup na ndio hao hao watatwaa Ligi Kuu!"Diego akiwa chini ya ulinzi mkali wa beki David Luiz.
Soma Zaidi Hapa »

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog