Friday, March 13, 2015


KIINGILIO cha chini katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika baina ya Yanga SC na Platinum FC ya Zimbabwe kitakuwa na Sh. 5,000 kwa jukwaa la viti vya rangi bluu na kijaniYanga wataikaribisha Platinum FC ya Zimbabwe katika mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, jumapili.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro alisema kwamba, katika jukwaa la viti vya Rangi Chungwa itakuwa Sh, 7000, VIP C Sh. 15,000, VIP B Sh. 20,000, na VIP A Sh 30,000.
Muro amesema tiketi zitaanza kuuzwa Jumamosi Saa 2:00 asubuhi katika vituo vya Karume (Ofisi za TFF), Mgahawa wa Steers (Posta Mpya), Oilcom (Buguruni), BigBon (Kariakoo), Olicom (Ubungo), Dar Live (Mbagala), Uwanja wa Uhuru, Kivukoni (Ferry) na Makumbusho (kituo cha mabasi).

Aidha, amesema magari yenye vibali maalum ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia ndani ya Uwanja siku hiyo.
Yanga SC imefika hatua hii baada ya kuitoa BDF XI ya Botswana, wakati Platinum iliing’oa Sofapaka ya Kenya.
Wakati huo huo: Kikosi cha Platinum kilichotarajiwa kuwasili Saa 2:00 usiku wa leo, hakijawasili na wenyeji wao, Yanga SC wameshangaa kwa sababu hawana taarifa nyingine.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog