Friday, October 16, 2015


Ofisa Biashara wa Manispaa ya Kinondoni, Ananias Kamundu (wa tatu kushoto), akipata maelezo kuhusu bidhaa za kampuni mpya ya simu za mkononi ya Halotel katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Viettel Tanzania wamiliki wa Halotel, Nguyen Thanh Quang na wageni wengine waalikwa. Ofisa Biashara wa Manispaa ya Kinondoni, Ananias Kamundu (kushoto), na Mkurugenzi wa kampuni mpya ya simu za mkononi wa Halotel Mkoa wa Kinondoni, Alex Thiem (kulia), wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kampuni hiyo nchini jijini Dar es Salaam leo. Katikati Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Viettel Tanzania wamiliki wa Halotel, Nguyen Thanh Quang .Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Viettel Tanzania wamiliki wa Halotel, Nguyen Thanh Quang akizungumza katika hafla hiyo.

Biashara wa Manispaa ya Kinondoni, Ananias Kamundu akizungumza akimwakilisha mkuu wa wilaya hiyo aliyetarajiwa kuwa mgebni rasmi.

Ofisa Biashara wa Manispaa ya Kinondoni, Ananias Kamundu (kushoto), akiagana na Mkurugenzi wa kampuni mpya ya simu za mkononi wa Halotel Mkoa wa Kinondoni, Alex Thiem mara baada ya kumalizika kwa shughulia za uzinduzi rasmi wa kampuni hiyo.

Wasanii wa kikundi cha Mama Afrika wakitoa burudani katika uzinduzi huo.

waliotembelea blog