Thursday, June 4, 2015

mooo
Mapema wiki hii millardayo.com iliandika stori ya ajali ya lori la mafuta kuua zaidi ya watu 90 Nigeria ikiwa ni baada ya kuwa kwenye mwendo mkali na kugonga watu na magari yaliyokuwa kwenye kituo cha abiria.
station
Muonekano wa kituo cha mafuta baada ya kulipuka
Lakini leo Ghana nayo imeingia kwenye headlines baada ya kituo cha mafuta kulipuka na kuua watu wanaokadiriwa kuzidi 90 katika mji mkuu wa nchi hiyo Accra.
Mlipuko huo umetokea baada ya mvua kubwa iliyosababisha mafuriko katika maeneo mengi ya mji huo ambapo pia imewaacha watu wengi bila makazi huku sehemu kubwa ya mji ikiwa gizani kutokana na kukatika kwa umeme.
mtoto
Mwili wa mtoto ukiokotwa katika eneo la kituo hicho
Idadi ya watu waliofariki huenda ikaongezeka kwani watu wengi wamepoteza maisha baada ya kuwepo kituoni hapo wakijikinga na mafuriko yaliyotokea na huenda idadi ikaongezeka kutokana na baadhi ya miili kuwa bado haijapatikana.


Kocha msaidizi wa Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Salum Mayanga, (kushoto) akiongea na wandishi wa habari leo. Katikati ni kocha Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Mart Nooij na kulia ni kocha msaidizi wa Taifa stars, Mecky Mexime.
KOCHA wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Mart Nooij, amesema atatumia kambi ya Ethiopia kujiandaa na mchezo wa Misri kwani vijana wapo katika hali nzuri na wameahidi kupambana kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo huo.
Mart Nooij aliyasema hayo leo wakati ametangaza kikosi cha wachezaji 23 walioondoka jana jioni kuelekea Addis Ababa Nchini Ethiopia kuweka kambi ya wiki moja kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri
“Nitatumia kambi ya Ethiopia kujiandaa na mchezo wa Misri, kwani wachezaji wapo katika hali nzuri na wameahidi kupambana kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo huo na baadae kufuzu katika fainali za Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2017”, alisema Nooij
Mchezo kati ya Misri na Tanzania wa kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2017
unatarajiwa kuchezwa Juni 14, katika uwanja wa Borg El Arab jijini Alexandria.
Kikosi cha Stars kiliondoka jana saa 11 jioni kwa Shirika la ndege la Ethiopia ambapo kitawasili jiji la Addis Ababa majira ya saa 1 jioni kwa saa za Afrika Mashariki kina wachezaji 23, benchi la ufundi la watu wanne na wajumbe wawili wa kamati ya Utendaji ya TFF ambao ni Vedastus Lufano na Geofrey Irick Nyange “Kaburu”.


Steve McClaren anatarajiwa kuthibitishwa kuwa Meneja mpya wa Klabu ya Ligi Kuu England Newcastle Wiki ijayo.
McClaren, mwenye Miaka 54, ni Meneja wa zamani wa England na pia aliwahi kuwa Meneja Msaidizi chini ya Sir Alex Ferguson huko Manchestet United.
Mwezi uliopita McClaren alutimuliwa kama Kocha wa Derby County inayochezea Ligi ya chini Championship.
Mara mbili McClaren amewahi kuigomea Newcastle kuwa Meneja wake na mara ya kwanza ilikuwa Desemba iliyopita wakati Alan Pardew alipoondoka na mara ya pili ni wakati Newcastke wakibakisha Mechi 3 za Ligi Msimu ulioisha Mei huku wakiwa hatarini kuporomoka Daraja lakini mwishoni walipona baada ya kuipiga West Ham 2-0 Siku ya mwisho ya Ligi.
Tangu alipoondoka Alan Pardew Newcastle ilikuwa chini ya John Carver ambae nae aliomba kushika wadhifa wa Meneja lakini sasa ameukosa lakini amebakishwa kama mmoja wa Makocha wa Klabu hiyo.

Mmoja wa wengine waliowania kuwa Meneja Newcastle ni Mchezaji wa zamani wa Newcastle Patrick Viera ambae hata hivyo alitoka mapema kwenye kinyang'anyiro baada ya kutoafikiana kuhusu masuala ya Uhamisho na Ununuzi wa Wachezaji.


Barcelona na Juventus Wikiendi hii mojawapo inaweza kuwa Klabu ya 8 Barani Ulaya kutwaa Trebo.
Huko Ulaya Klabu inayofanikiwa kuwa Bingwa wa Nchi yake na pia kutwaa Kombe la Nchi hiyo na kisha kufanikiwa kubeba Kombe la UEFA CHAMPIONS LIGI kwenye Msimu mmoja huo huo husemwa imetwaa Trebo.
Hivi karibuni Barcelona waliifunga Athletic Bilbao kwenye Fainali na kubeba Copa del Rey na hiyo inafuatia kuubeba Ubingwa wa Spain wa La Liga.
Nao Juve tayari wameshatia kabatini Kombe la Ubingwa wa Italy baada kushinda Ligi ya Serie A na pia kuchukua Coppa Italia.
Timu hizi mbili zinapambana huko Berlin, Germany kesho kutwa jumamosi Juni 6 kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI na Mshindi atakuwa na Trebo kibindoni.
Wakati Barca ikiwania kutwaa Trebo kwa mara ya pili na kuwa Klabu ya kwanza kufanya hivyo, Juve itakuwa mara yao ya kwanza.
Klabu iliyoanza kutwaa Trebo kwa mara ya kwanza baada ya Kombe la Klabu Bingwa Ulaya kubadilishwa mfumo na jina na kuitwa UEFA CHAMPIONS LIGI ni Manchester United hapo 1999.
Man United bado inaongoza kwa England kutwaa trebo mpaka sasa!
KLABU ZILIZOWAHI KUTWAA TREBO NI:
-CELTIC 1966/67
-AJAX 1971/72
-PSV EINDHOVEN 1987/88
-MAN UNITED 1998/99
-BARCELONA 2008/09
-INTER MILAN 2009/10
-BAYERN MUNICH 2012/13


Mascherano vs. TevezGiorgio Chiellini kuikosa Fainali ya Jumamosi dhidi ya Barcelona kutokana na Majeraha, Hivyo kutocheza mchezo huo kumfanya asikutane na mbaya wake Louis Suarez.


www.bukobasports.comShirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF leo limezindua jezi mpya za timu za Taifa, zitakazokuwa zikitumika na timu za Taifa katika michuano mbali mbali itakayokua inazikabili.
Uzinduzi huo wa jezi mpya uliofanyika katika ukumbi wa Kilimanjaro jengo la Golden Jubilee uliambatana na uziduzi wa tovuti mpya ya shirikisho, uliongozwa na mgeni rasmi Mh. Said Mtanda, mbunge wa jimbo la Mchinga na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya jamii.
Katika uzinduzi huo, kulizunduliwa jezi aina tatu, ambazo ni jezi za ugenini, jezi za nyumbani na jezi zitakazokuwa zikitumika kwa ajili ya mazoezi.
Ifuatayo ni hotuba ya Rais wa TFF , Jamal Malinzi aliyoisoma wakati wa uzinduzi wa jezi mpya za timu za Taifa, uzinduzi wa tovuti mpya ya TFF na kutunuku vyeti kwa viongozi mbalimbali, makocha, wachezaji na wadhamini.
Mh Said Mtanda Mbunge wa Jimbo la Mchinga na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii
Mzee Said el Maamry Mwenyekiti Msataafu wa FAT
Ndugu Leodeger Tenga Mjumbe wa Kamati ya utendaji ya CAF na Rais mstaafu wa TFF
Ndugu wageni waalikwa
Ndugu waandishi wa habari
Mabibi na mabwana
Salam aleikum.

Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutufikisha hapa leo na kwa mafanikio mbali mbali ambayo tumekuwa tukiyapata.Ninakushukuru sana ndugu mgeni rasmi kwa kuacha shughuli zako kuja kujiunga nasi asubuhi hii katika shughuli hii.
Ndugu mgeni rasmi,tarehe 08 oktoba 1964 Tanzania ilipata uanachama rasmi wa shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA. TFF tuliona jambo zito kama hili hatuwezi kuliacha lipite hivi hivi.Hivyo mwaka jana tuliamua kuenzi maadhimisho ya miaka 50 ya kujiunga na FIFA kwa kufanya mambo mambo matatu makubwa.
La kwanza ni kutoa vyeti maalum kwa watu binafsi na taasisi mbali mbali kwa kutambua mchango wao uliotukuka katika kuendeleza mpira wa miguu Tanzania.

Leo hii ndugu mgeni rasmi tutakuomba ukabidhi vyeti hivi kwa wawakilishi wa makundi kadhaa kwa niaba ya wenzao.Makundi haya ni pamoja na viongozi wa kitaifa wastaafu,mawaziri wa michezo wastaafu,viongozi waliopita wa TFF?
FAT,wakurugenzi wa idara ya michezo,wenyeviti na makatibu wa baraza la michezo la taifa,Timuya Taifa iliyocheza fainali za Afrika mwaka 1980,waamuzi,makocha,wachezaji wa timu ya Taifa na watangazaji mahiri wa michezo.Jumla tumetunuku vyeti 194.
Kiuhalisia idadi hii ni ndogo sana ukilinganisha na wingi na uzito wa michango ya wadau mbali mbali wa mpira katika miaka 50 iliyopita.
Tunaomba Watanzania wenzetu watuelewe katika hili kuwa hawa tutakaowatunuku vyeti hivi ni wawakalilisha wa wadau wote wa mpira Tanzania.
Ninaomba tusimame kwa muda mfupi tuwaombe ewadau wenzetu na viongozi wa mpira wa miguu ambao wako katika orodha hii na wametangulia mbele ya haki.
Ndugu mgeni rasmi katika kuenzi miaka 50 ya Tanzania kujiunga na FIFA leo hii pia tutatoa mchango wa fedha kwa makundi yenye mahitaji katika jamii.
Pesa hizi zinatokana na makusanyo mbali mbali ikiwemo makusanyo ya mechi ya ngao ya hisani ifanyikayo kila mwaka. Makundi haya ni pamoja na walemavu wa viuongo,walemavu wa ngozi na wasioona.
Kitendo hii ni moja ya juhudi za TFF kurudisha katika jamii kile tunachokusanya. Kila kundi litapewa shilingi milioni tano na tunaendelea kupokea maombi toka makundi mbali ya kijamii na tukiyapitisha tutaendelea kugawa fedha hizi.
Jambo la tatu tutakalolifanya leo litakuwa ni kuzindua rasmi tovuti mpya ya TFF (www.tff.or.tz). Tumeamua kufanya jamabo hili katika kuenzi miaka hamsini ya kujiunga na FIFA ili kutoa msisitizo kuwa sasa TFF na sisi tunajiunga Na kuendeleza mpira kisasa kulingana na teknolojia iliyopo.

MATUKIO YA MAZISHI YA MHE. SAMWELI NTAMBALA LWANGISA LEO JUMATANO JUNI 3, 2015 KITENDAGURO-BUKOBA. MAMIA WAJITOKEZA KUMUAGA!

Na Faustine Ruta, Bukoba
Mamia ya Waakazi wa Mji wa Bukoba na Vitongoji vyake wakiwemo na Wageni mbalimbali kutoka nje ya Mkoa huu na nje ya Nchi wamejitokeza kwa wingi kumzika marehemu Samuel Luangisa leo Jumatano juni 3, 2015 nyumbani kwake Kitendaguro nje kidogo na Mji wa Bukoba. Marehemu Samuel Luangisa ni miongoni mwa waasisi wa Taifa na katika vipindi tofauti alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Ziwa Magharibi(Kagera) Mbunge na Meya wa Manispaa ya Bukoba pamoja na nyadhifa nyingine.

Mbunge wa muleba kusini Prof Anna Kajumulo Tibaijuka
Baadhi ya Viongozi wa dini(katikati) ni Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini
Taswira za picha enzi ya uhai wa Marehemu Mhe. Samuel LuangisaMerehemu Samwel Lwangisa alizaliwa mwaka 1932 na mauti yalimkuta New York Marekani tarehe 25.05.2015 na kuzikwa leo Jumatano juni 3, 2015 Nyumbani kwake Kitendaguro Bukoba.
Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini

Mwanae na Marehemu akitoa neno lake
Wanakwaya Mbalimbali walihudhuria Mazishi hayo
(katikati) ni Mzee Masabala

Jeneza lililobeba Mwili wa Marehemu Mhe. Samuel Ntambala Luangisa
Kushoto ni Mkuu wa Mkoa Kagera Mkuu wa Mkoa wa Kagera John Mongella akiwa sambamba na Mbunge wa Bukoba Mjini kwa tiketi ya CCM, Khamis Sued Kagasheki katika Mazishi Mhe. Samwel Ntambala Lwangisa leo Nyumbani kwake KItendaguro Nje kidogo ya Mjini wa Bukoba. Picha na Faustine Ruta

Le Mutuz nae alikuwepo katika Mazishi hayo ya Mhe. Samweli Ntambala Lwangisa.

waliotembelea blog