Tuzo ya mchezaji bora wa mwezi ni tuzo
ambayo Ligi nyingi duniani huwa wanayo hata katika Ligi Kuu soka
Tanzania bara huwa ipo, December 8 ndio siku ambayo Ligi Kuu Hispania ilitangaza tuzo ya mchezaji bora wa mwezi, Neymar anayekipiga katika klabu ya FC Barcelona ndio mchezaji aliyefanikiwa kutwaa tuzo hiyo kwa mwezi November.
Tuzo ya mchezaji bora wa mwezi ya Neymar inaingia katika rekodi za staa huyo, kwani stori kutoka fcbarcelona.com zinaeleza kuwa Neymar ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa FC Barcelona kuwahi kutwaa tuzo hiyo, rekodi ya Neymar sio tu ya kutwaa tuzo hiyo kwa mara ya kwanza kwa upande wake ila ni mchezaji wa kwanza wa FC Barcelona kuwahi kutwaa tuzo hiyo rekodi ambayo haiwezi kuvunjwa.
Tuzo hiyo ya mchezaji bora wa mwezi ya Laliga
imeanza kutolewa toka msimu wa 2013/2014, hivyo huu ni msimu wake wa
tatu toka ianze kutolewa na imetolewa mara 21 hadi sasa, kwa maana hiyo Neymar ambaye ana magoli 14 katika msimamo wa wafungaji wa Ligi Kuu Hispania, ameweka rekodi ambayo haiwezi kuvunjwa kamwe na mchezaji wa FC Barcelona kwani hata mchezaji mwingine wa FC Barcelona akishinda tuzo hiyo Neymar ataendelea kuwa na rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa FC Barcelona kushinda tuzo hiyo.