Tuesday, December 8, 2015


DROO ya Raundi ya 3 ya Kombe kongwe Duniani, FA CUP, ambalo sasa linaitwa Emirates FA Cup kwa sababu za kiudhamini, imefanyika Usiku huu ikihusisha Timu zote za Ligi Kuu England na Daraja la Championship ambazo huanzia hapa.
Droo hii, ambayo imeibua Mechi 5 za Timu za Ligi Kuu England kuvaana wenyewe kwa wenyewe, imefanyika huko Sport Wales National Centre Mjini Cardiff, na kuhusisha Timu 64 na Mechi zake zitachezwa kati ya Ijumaa Januari 8 na Jumatatu Januari 11.

Arsenal, ambao ndio Mabingwa Watetezi baada ya kulitwaa Kombe hili kwa mara ya pili mfululizo Mwezi Mei Mwaka huu, watakuwa kwao Emirates kucheza na Sunderland wakati Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu England, Chelsea, wapo kwao Stamford Bridge kucheza na Mshindi kati ya Timu za Madaraja ya chini Leyton Orient v Scunthorpe United.
Manchester United wapo kwao Old Trafford kucheza na Sheffield United wakati Man City wako Ugenini kucheza na Norwich City.
Liverpool wako Ugenini kuivaa Exeter City huku Mechi tamu iko White Hart Lane ambako Tottenhma watavaa Vinara wa Ligi Kuu England Leicester City. 

Droo ya Raundi ya Tatu:
Watford v Newcastle
West Brom v Bristol City
West Ham v Wolves
Salford/Hartlepool v Derby
Exeter City v Liverpool
Northampton Town v MK Dons
Peterborough v Preston
Colchester v Charlton
Tottenham v Leicester
Arsenal v Sunderland
Ipswich Town v Portsmouth
Newport County v Blackburn Rovers
Sheffield Wednesday v Fulham
Wycombe Wanderers v Aston Villa
Birmingham City v AFC Bournemouth
Oxford United v Swansea City
Brentford v Chesterfield or Walsall
Bury v Bradford City
Manchester United v Sheffield United
Everton v Dagenham and Redbridge/Whitehawk
Southampton v Crystal Palace
Carlisle United v Yeovil Town
Nottingham Forest v QPR
Eastleigh v Bolton Wanderers
Chelsea v Leyton Orient/Scunthorpe United

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog