Tabasamu 'bab kubwa': Ashley Young
akiungana na wachezaji wenzake Wayne Rooney na Danny Welbeck kwenye
mazoezi ya Manchester United.
LOUIS van Gaal atawachana macho kwa
macho wachezaji wake ambao wataachwa na Manchester United baada ya
kumaliza ziara ya Marekani ambapo amewapa nafasi ya kumuonesha viwango
vyao.
Anderson, Nani, Javier Hernandez, Shinji
Kagawa na Marouane Fellaini ni miongoni mwa majina makubwa yaliyopo
katika mstari mwekundu kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.
Lakini inafahamika kuwa Van Gaal hatakuwa na huruma kabisa ingawa hajafanya maamuzi ya hadharani.
'Nitafikia maamuzi baada ya ziara hii,' alisema. Nimewapa nafasi ya kucheza wachezaji wote na najua zaidi hata kabla ya ziara.
Louis van Gaal atawaambia wachezaji asiowahitaji kuwa wapo tayari kutafuta timu nyingine.
'Kwa sasa nimefikia maamuzi kidogo,
lakini kwenye mpira wa miguu lazima uamue. Unatakiwa kuwapa nafasi
wachezaji kufanya usajili pale unapoona hawana nafasi ya kucheza kwenye
kikosi chako.
'Unatakiwa kusema mapema kwasababu ni
mbali sana baada ya Agosti 31. Nitawaambia wachezaji baada ya ziara hii,
lakini nitawaambia wao na sio ninyi.'
Van Gaal aliyasema hayo wakati akiongea
na waandishi wa habari mjini Miami jana kuelekea mechi ya fainali ya leo
usiku ya kombe la kimataifa nchini Marekani dhidi ya mahasimu wao
wakubwa England, klabu ya Liverpool.
0 maoni:
Post a Comment