Anawindwa: Javier Hernandez (kushoto)
yupo katika rada za Southampton ambao wamepanga kutumia paundi milioni
70 majira haya ya kiangazi.
Southampton wanapanga kutumia paundi
milioni 70 siku chache zijazo ili kusajili wachezaji wataoziba nafasi za
nyota wao walioondoka.
Saints wanatarajiwa kuwasajili baadhi ya wachezaji watakaoachwa na Manchester United wakati huu wanaoimarisha kikosi chao.
Klabu hiyo inamhitaji mshambuliaji wa
Mexico, Javier Hernandez na Wilfried Zaha au Ashley Young kutegemeana na
winga gani Louis Van Gaal atamuacha.
Bosi mpya wa Saints, Ronald Koeman pia
anaziwinda saini za waholanzi wawili, Ron Vlaar wa Aston Villa na Virgil
van Dijk wa Celtic, wakati huo huo kipa wa Celtic Fraser Forster naye
yupo katika rada zake.
Tatizo la Southampton ni kwamba klabu
nyingine zitawasumbua kwenye dau la uhamisho kwasababu zinajua timu hiyo
imepata paundi milioni 100 baada ya kuuza wachezaji watano wa kikosi
cha kwanza.
Kwenye rada: Wilfried Zaha (kulia) pia anawindwa na Southampton
0 maoni:
Post a Comment