Mwanzo mzuri: Joe Allen akipongezwa na Rickie Lambert baada ya kuifungia bao la kuongoza Liverpool dhidi ya AC Milan.
LIVERPOOL wametinga fainali ya
mashindano ya kimataifa ya maandalizi ya msimu nchini Marekani na sasa
watakabiliana na wapinzani wao wakubwa Manchester United siku ya
jumatatu.
Hii inatokana na ushindi wa mabao 2-0 waliopata dhidi ya AC Milani huko Charlotte.
Mabao ya Liverpool yalifungwa na Joe
Allen na Suso na yaliwafanya Liverpool washinde mechi tatu kati ya tatu
walizocheza kwenye mashindano hayo.
Majogoo hao wa jiji walikuwa na uhakika
wa kumaliza katika nafasi ya juu ya kundi lao kufuatia Manchester City
kufungwa kwa penati 5-4 dhidi ya Olympiacos baada ya kutoka sare ya 2-2
katika dakika za kawaida.
Hata hivyo katika mchezo huo, Rickie Lambert alikosa mkwaju wa penalti.
Kinda nyota: Raheem Sterling akijaribu kuchukua m[ira dhidi ya kiungo wa AC Milan Michael Essien
Rickie Lambert alikosa mkwaju wa penalti lciha ya Liverpool kushinda.
Kikosi cha LIVERPOOL: Mignolet, Kelly (Johnson 60), Toure (Sakho 60), Coates (Skrtel 60), Robinson Enrique 60), Lucas (Gerrard 60), Henderson (Suso 46), Allen (Can 60), Lambert (Peterson 60), Ibe (Coutinho 60), Sterling (Coady 46).
Wafungaji wa magoli: Allen (17), Suso (89).
Kikosi cha AC MILAN: Abbiati
(Gabriel 46), Abate (Zapate 80), Bonera, Rami (Mexes 66), De Sciglio,
Essien (Cristante 66), Muntari (Poli 80), Saponara, Niang, Pazzini
(Balotelli 46), El Shaarway (Honda 66).
Mwamuzi: David Gantar
0 maoni:
Post a Comment