Mashabiki 21 wa Westham na Newcastle wamekamatwa na polisi mjini Dusseldorf (picha ya juu haihusiani na tukio).
POLISI nchini Ujerumani wamewatia
mbaroni mashabiki 21 wa klabu za Westham na Newcastle baada ya
kuanzishaji fujo na kuzichapa 'kavukavu' huko Dusseldorf.
Mapigano hayo yalizuku baina ya mashabiki hao hasimu jana mchana na polisi 100 walipelekwa eneo la tukio kutuliza ghasia.
Timu hizo mbili zitachuana katika kombe la Schalke 04 mwishoni mwa wiki hii huko Gelsenkirchen.
Msemaji wa polisi wa Polizeipräsidium Düsseldorf alisema:
"Kulikuwa na mashabiki 300 wa Uingereza katikati ya mji".
"Mashabiki kutoka klabu zote walikutana
na awali ya yote walikuwa na bia na walipokutana walianza kurushiana
maneno na baadaye kuamua kupigana".
"Tulituma polisi 100 katikati ya mji ili
kutuliza mambo na zoezi hilo lilifanikiwa haraka na kwa muda mfupi
tuliwatia mbaroni mashabiki 21",
Mwishoni mwa wiki hii klabu za Newcastle na West Ham zinachuana katika kombe la Schalke 04
0 maoni:
Post a Comment