Louis van Gaal amejipa nafasi ya kutwaa kombe la kwanza akiwa Manchester United ikiwa ni wiki tatu tu tangu aanze kazi.
Kushindi kombe la kimataifa la
maandalizi ya msimu nchini Marekani sio sababu ya kusema Man United
itakuwa kali na kufuta machungu ya miezi 12 ya David Moyes, lakini
utakuwa mwanzo mzuri kwa Mholanzi huyo katika dimba la Old Trafford kama
timu yake itashinda fainali siku ya jumatatu mjini Miami.
Man United jana usiku imefanikiwa
kuifunga Real Madrid mabao 3-1, huku Cristiano Ronaldo akianzia benchi
dhidi ya timu yake ya zamani.
Bao la kwanza la Man United lilifungwa
na Ashley Young katika dakika 20. Katika dakika ya 27, Real Madrid
walisawazisha bao hilo kwa mkwaju wa penalti uliotiwa kambani na Gareth
Bale.
Katika dakika ya 37 kipindi hicho cha
kwanza, Young aliifungia United bao la kuongoza na katika dakika ya 80,
Javier Hernandez 'Chicharito' akaifungia United bao la tatu.
Shujaa wa United: Ashley Young alifunga mawili katika ushindi wa 3-1
Watazamaji 109,00 waliitazama mechi kwenye uwanja wa Michigan mjini Ann Arbor
MATCH FACTS
KIKOSI CHA MANCHESTER UNITED (3-4-1-2): De
Gea 7; Keane 5.5, Jones 7, Evans 6 (Blackett 45mins 6); Valencia 5.5
(Lingard 61mins 6.5), Herrera 7 (Cleverley 45mins 6), Fletcher 7.5,
Young 7 (Shaw 45mins 6.5); Mata 6.5 (Kagawa 61mins 6.5); Welbeck (Zaha
41mins 5.5), Rooney 6 (Hernandez 61mins 7).
Mfungaji wa magoli: Young 20, 37, Hernandez 80.
KIKOSI CHA REAL MADRID (4-1-4-1):
Casillas 6; Arbeloa 6 (Ronaldo 73mins 6), Pepe 6, Ramos 6.5, Fernandez
7; Alonso 7(De Tomas 55mins 7.5); Carvajal 6.5, Illarramend 6, Modric 6,
Bale 7; Isco 6.
Mfungaji: Bale (pen) 27.
Kadi ya njano: Arbeloa, Isco.
Mwamuzi: Hilario Grajeda 7.
Alivunja ngome: Young alimtungua kwa umakini mkubwa kipa wa Real Madrid, Iker Casillas
0 maoni:
Post a Comment