Sunday, August 3, 2014


Keita compares Garcia to Guardiola


SEYDOU Keita amemfananisha kocha wa Roma, Rudi Garcio na kocha wake wa zamani akiwa Barcelona, Pep Guardiola.

Kiungo huyo wa zamani wa Barca alijiunga na timu hiyo ya Seria A kwa mkataba wa mwaka mmoja majira haya ya kiangazi kufuatia kumalizana na Valencia.
 Nyota huyo mwenye miaka 34 anajiimarisha ili kutafuta nafasi chini ya Garcia na amezifananisha mbinu za Mfaransa huyo na Guardiola ambaye alicheza chini yake katika dimba la Camp Nou.

Keita ameliambia La Gazzetta dello Sport:  “Nimekuja katika kikosi kikubwa na kuungana na wachezaji wazuri”.
“Kucheza na wachezaji kama Francesco Totti, Daniel De Rossii, Morgan De Sanctis, Mehdi Benatia, Miralem Pjanic na nina uhakika ninawasahau wengine, tuna kila kitu na tunachosubiria ni msimu mzuri,”
“Pep alikuwa ananisema sana nikiwa Barcelona kwasababu siku zote alikuwa anatambua mchango wangu kwa klabu. Garcia ni sawa na yeye na ananikumbusha enzi za Pep, anatamani kuona timu yake inacheza mpira wa kuvutia na kumiliki”.

“Wana mbinu sawa sawa: matokeo yanapatikana kupitia mpira mzuri”.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog