Thursday, November 26, 2015


FC Barcelona na Neymar zinakaribia kusaini Mkataba mpya ambao utamfanya Kepteni huyo wa Brazil kuzoa Euro Milioni 15 kwa Msimu.
Donge hilo nono litamfanya awe Mchezaji wa 3 Duniani anaelipwa Mshahara wa juu kabisa akiwa nyuma ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.
Hivi sasa Neymar inasemekana analipwa Euro Milioni 8.8 kwa Mwaka.
Habari hizi zimetobolewa na Jarida la Marca huko Spain ambalo limesema Mkataba huo mpya utaongeza juu Dau lake ikiwa Klabu nyingine itataka kumnunua ndani ya Mkataba kutoka Euro Milioni 180 za sasa na kufikia Euro Bilioni 1 ingawa Wawakilishi wa Neymar wanataka Kipengele hicho kigote kwenye Euro Milioni 250.

Mkataba huo mpya utamweka Neymar, mwenye Miaka 23, Klabuni Barca hadi Juni 2021.

Hivi karibuni kulikuwa na minong’ono kuwa Neymar ataondoka Barca kutokana na kuwepo Kesi inayohusisha Uhamisho wake kutoka Klabu ya Brazil Santos kwenda Barca ambayo Baba yake Mzazi Neymar nae amehusishwa kwenye njama zinazodaiwa Barca ilifanya ili kukwepa kulipa Kodi huko Spain kwa kuficha gharama halisi za Uhamisho huo.

Hivi sasa Neymar anang’ara mno kiasi ambacho Wachambuzi wanatambua muda si mrefu atatwaa Ballon D'Or hasa ukizingatia umri wake ni mdogo ukilinganisha na Messi na Ronaldo ambao sasa wanaanza ‘kuzeeka’ Kisoka.



Jana klabu ya Manchester City ilikubali kipigo cha bao 1-0  dhidi ya Juventus ikiwa ni ligi ya mabingwa Ulaya.
Kiungo wa Juve Paul Pogba jana usiku alionesha uzalendo kwa taifa lake hilo baada ya kuvalia viatu maalumu vyenye rangi ya bendera ya Ufaransa kama sehemu ya kuwaenzi wahanga wa shambulio la kigaidi lililotokea katika jiji la Paris, Ufaransa.
Football Soccer - Juventus v Manchester City - UEFA Champions League Group Stage - Group D - Juventus Stadium, Turin, Italy - 25/11/15 Juventus' Paul Pogba's boots Action Images via Reuters / Andrew Couldridge Livepic EDITORIAL USE ONLY.
Kiungo huyo alikuwa mmoja wa watu waliokuwepo uwanjani wakati magaidi wanafanya mashambulizi nje ya uwanja wa Stade de France wiki iliyopita huku watu wasiopungua 124 wakipoteza maisha.


Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea na timu ya Taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba amesema matarajio yake ya sasa ni kuona anarudi kwenye klabu yake ya zamani ya Chelsea kama kocha.
Drogba, ambaye kwa sasa anacheza soka ya kulipwa ya Montreal Impact huko Canada, aliifungia Chelsea jumla ya mabao 164 wakati akiitumikia klabu hiyo.
Mshambuliaji huyo amesema angependa kuihudumia klabu hiyo baada ya kukamilika kwa kipindi chake cha  uchezaji.
”Tayari nimekubaliana na wakurugenzi wa klabu hiyo kuwa ninaweza kurejea kuwa meneja kwa sababu klabu hiyo ilinisaidia sana, pia imenikuza katika kipaji changu cha mpira”..
Drogba ndiye aliyeifungia Chelsea bao lililoipa ushindi na taji la mabingwa wa bara Ulaya mwaka wa 2012 pia aliisaidia Chelsea kunyakuwa mataji 4 ya ligi kuu ya Uingereza kabla ya kuhamia Canada kujiunga na klabu ya Montreal Impact.

waliotembelea blog