MENEJA wa Chelsea Jose Mourinho ameusapoti msimamo wa Arsene Wenger kwamba Ballon d'Or ifutiliwe mbali
Mwezi Januari, Wenger, ambae ni Meneja wa Arsenal, aliiponda Tuzo hiyo ya FIFA anaetunukiwa Mchezaji Bora Duniani wa Mwaka na kusisitiza kuwa angepewa nafasi ya kupiga Kura asingekubali.
Hata hivyo, Wenger hana nafasi ya kumpigia Kura Mgombea wa Tuzo hiyo kwa vile Washiriki wake ni Makocha wa Timu za Taifa na Manahodha wake pamoja na Jopo maalum la Wanahabari.
Cristiano Ronaldo, ambae aliwahi kucheza chini ya Mourinho alipokuwa Real Madrid, ndie anaeshikilia Tuzo hiyo kwa sasa baada ya kuitwaa kwa mara ya 3 Mwezi Januari.
Akiongea hapo jana, Mourinho alisema Tuzo hiyo inavuruga Soka kwa kuweka msisitizo kwa Mtu binafsi badala ya Timu.
Mourinho alisema: "Nadhani Wenger alisema kitu cha maana, anapinga Ballon d’Or, na nadhani yuko sahihi kwa sababu kwa sasa Soka linapoteza mvuto wa Kitimu na kutilia mkazo Mtu binafsi!"
Mourinho alinena: "Sasa tunatizama ubinafsi. Fulani na takwimu zake kwamba alikimbia umbali mrefu. Kwa sababu kwenye Gemu umekimbia Kilomita 11 na mie nimekimbia 9 wewe ndio umefanya kazi nzuri? Pengine siyo! Labda Kilomita zangu 9 ni muhimu kuliko zako 11! Kwangu mie Soka ni Kitimu. Mtu binafsi anakaribishwa ikiwa anataka kufanya Timu yetu iwe bora!''Aliongeza: "Mchezaji mkubwa akiwasili anaikuta Timu ipo. Si yeye anaeigundua Timu kama vile Columbus alivyoivumbua Amerika. Wewe unakuja kutusaidia tuwe bora zaidi. Kama Meneja kila Siku inabidi utoe ujumbe huu!"